Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=EqnvUKFZueA"]http://www.youtube.com/watch?v=EqnvUKFZueA[/ame]
 
Mimi sitoi habari za blaa blaa, nyie subilini tu,
Mkuu, ndio hutoi habari za blah blah lakini heading ya post yako ina mislead.....ilitakiwa iwe kama swali Re: Babu Seya na wanae kutoka jela? otherwise kwa namna ulivyopost you have already made a conclusion......
 
Naona Bi.Lyamuya alikosea kuwa hukumu sawa sawa, alitakiwa awahukumu kunyongwa washenzi hawa...ingelikuwa hadithi saivi...wakenda appeal wanaweza wakapunguziwa miaka ua wakatoka...na uhuni walioufanya kwa visichana vile ni mkubwa na wakishenzi...aaaagh!
 
Naona Bi.Lyamuya alikosea kuwa hukumu sawa sawa, alitakiwa awahukumu kunyongwa washenzi hawa...ingelikuwa hadithi saivi...wakenda appeal wanaweza wakapunguziwa miaka ua wakatoka...na uhuni walioufanya kwa visichana vile ni mkubwa na wakishenzi...aaaagh!

Kaka kukata Rufaa ni haki yao, na kama wakifanikiwa kutoka watakuwa wametoka kwa maamuzi ya mahakama na siyo kwa sababu wamependelewa, kwani ni wangapi wamefungwa kwa makosa ya kusingiziwa na jamii leo inawahesabu kuwa ni wahalifu wakubwa sana duniani? Punguza hasira, ingawa ni kweli kitendo hicho kinaumiza lakini vita subira nao watimize haki yao ya kukata rufaa. Isipokuwa kama nawe unaoushahidi endelea kuwashutumu na kuwaitwa waninii vileeee! Loo siwezi kurudia kutamka
 
Kaka kukata Rufaa ni haki yao, na kama wakifanikiwa kutoka watakuwa wametoka kwa maamuzi ya mahakama na siyo kwa sababu wamependelewa, kwani ni wangapi wamefungwa kwa makosa ya kusingiziwa na jamii leo inawahesabu kuwa ni wahalifu wakubwa sana duniani? Punguza hasira, ingawa ni kweli kitendo hicho kinaumiza lakini vita subira nao watimize haki yao ya kukata rufaa. Isipokuwa kama nawe unaoushahidi endelea kuwashutumu na kuwaitwa waninii vileeee! Loo siwezi kurudia kutamka
Sikusema kuwa hawana haki ya kukata rufani...lakini hata kama watashinda rufani hiyo haina maana kuwa na si lazima iwe hivyo, kuwa hawakufanya unyama ule...nafikiri kama sijakosea kuna memba hapa alituletea taarifa za kumbukumbu ya kesi ile na memba wengi wamesoma na wakakubali kuwa jamaa hawajaonewa wala hawajasingiziwa, ushahidi ulikuwa wazi na usio chembe ya shaka...na ndo maana hata mahakama kuu ika upheld uamuzi wa mahakama ya awali...na kwa kadiri nijuavyo, watakachofanya waheshimiwa majaji wa rufani ni kutazama kumbukumbu ya kesi tu na si kusikiliza kesi upya...na zaidi kwa kuwa wanapinga kutiwa hatiani...itatazamwa wapi maelezo ya kesi na sheria imekosewa...mpaka wakata rufani wakajihisi kuwa wametiwa hatiana isivyohalali...tusubiri lakini mpaka sasa tunahaki kuwaita...wahalifu, wabakaji...ndivyo mahakama za awali zilivyoamuwa na itabaki hivyo mpka mahakam ya juu ione vinginevyo.
 
Mmh nashindwa kuelewa jamani kama walishapelekwa congo wale tuliowaona wakiimba na kucheza pale ukonga ni akina nani?

Watu ni wazushi sana! Wote bado wako gereza la Ukongo na kwenye tamasha la wafungwa liliondaliwa na Shingongo mwaka jana tuliowana kwenye TV wakishiriki mpira wa miguu, mbio za mita mia moja na baadaye wakaangusha burudani ya muziki.

Ila kusema ukweli huwezi hata kumtambua Nguza ni yupi, watoto ni wepi. Maana wamechakaa sana! Maisha ya jela sio mchezo.
 
Hii inasikitisha sana na mara nyingi nikisoma hii taarifa ya Nguza Family natokwa na imani na viongozi wa nchi hii. Kwa kuwa sijui ukweli halisi wa hili, nadhani wako wenye data. wasiwasi wangu ni kwanini kesi hii ilendeshwa chemba sana.

Kama ni harakati za kuamsha ari ya kuwezesha rufaa ya Nguza nadhani ikianzia hapa JF naiamini JF ni wanaharakati wenye uhakika na kile wanachofanya.

Mimi binafsi bado nina imani na mahakama zetu. Maisha ya sirini ya mtu huwezi kuyajua kwa hiyo inawezekana ni kweli walikutwa na hatia ya kuwanajisi hao watoto.

Kuna mtu mmoja wa karibu sana na mimi anayefanya kazi mahakama ya Kisutu alishuhudia jinsi watoto wa kiume walivyoharibiwa sehemu zao za siri kwa kuingiliwa kimwili.

Hivi kuna mtu yeyote ambaye amewahi kujiweka kwenye nafasi ya mzazi wa mtoto mmojawapo wa walioharibiwa akahisi jinsi gani inauma?

Au tu kwa kuwa Nguza ni mtu mashuhuri na mnapenda muziki wake basi mnasahau kabisa kwamba kuna wazazi ambao watoto wao wameharibiwa wanaona hata hiyo adhabu waliyopewa kina Nguza haitoshi.

Tuangalie na upande wa pili wa shilingi. Tusiishie kwenye ''hearsays'' za vijiweni!
 
Kuna stori Global leo hii ya Francis Nguza, mwanaye Nguza, akisumbuliwa na ugojwa akiwa gerezani na msemaji wa gereza ndiye aliyenukuliwa kueleza hali ya Francis.

Kuhusu kesi yao, si siri hawa jamaa walifanya kweli huo mchezo mchafu wa kishenzi kwa visichana vile vidogo, watu watasema watakavyosema lakini Nguza alishaonywa kuhusu mchezo huo kwa kuwa hao watoto aliokuwa akiwafanya,walikuwa wakiwadithia wenzao.

Kuna tetesi (sina uhakika wake) kuwa Nguza akifanya upuuzi huo kama miiko ya kiganga ya kubaki katika chati au kulipia gharama za wakati akiwa katika chati kimuziki na inadaiwa na watoa tetesi hao(bado sijapata uhakika wa hii) kuwa alishamtoa mkewe kafara na wangefuata watoto...kuwa na bifu na Mkuu yeyote ni tetesi na hata hao watoa tetesi walidai hivyo

...upande wa pili kesi yenyewe ilivyokwenda mahakamani kila kitu kilikuwa hakina shaka na taarifa za faili ya kesi yao ukisoma hakuna mushkeli wowote kuwa jamaa alikuwa akivifisidi vitoto vya watu.


Rufani yake imepangwa tarehe 30 Novemba mwaka huu na majaji waliopangwa kusikiliza kesi yao ni Wah. N. Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Masati (aliyesikiliza na kutoa hukumu ya kuwaachia akina Zombe)
Ukweli na Uwongo wa madai hayo yatajuulikana baada ya si zaidi ya siku 60 kutoka sasa.

Time will tell...lets wait
 
Nyie nao mmezidi au hamjui kuwa sheria inafuata mkondo wake,hata wahusika wakashfa ya Richmond ipo siku yao.
 
Hapana ... hawakupakaziwa ... hawa watu walicheza mkanda wa mambo hayo na watoto .. mkanda ukauzwa nje ya nchi .. some foreign ambassodor to tanzania had gone back home on an errand ... akaufuma huu mkanda ambayo aliletewa akaambia see what is happening in Tanzania ... the ambassodor who knew the culprits came back to TZ ... called top officials and showed them the mkada ... luckily the guys were easily identified ... and the only thing to do was to pin them down ...wakatumia hizo mbinu as wale watoto waliyowachezea wasingepatikana .. this is why hii kesi no one could tamper with with it as there was recorded evidence ....

They are paying for their sins


Naima kidooogo naweza nikaamini amini haya maelezo yako.Lakini Mkuu kama unakijua kisa hiki nje ndani basi nisaidie kidogo na hili swali:
Kwanini wasingetumia hiyo tape unayodai katika hii kesi na badala yake wakaamua kuitengeneza upya kwa kumtegeshea Nguza na wanawe hivyo vitoto?I mean hiyo tape si ina kila kitu,sura za jamaa,hivyo vitoto,jinsi walivyokuwa wanafanya huo mchezo,hii haitoshi kuwafunga mpaka wamuwinde tena na kumtegeshea hivyo vitoto vingine?
Na kama wadau wengine walivyodai,iweje yule mwalimu aliyekuwa anawapeleka hao watoto aachwe huru>?
 
Sina hakika kama issue ya Mzee Nguza Viking na wanae iliwahi kukatwa hapa, by then ilipokuwa hot nilikua sija join JF. Kwanza kabisa lazima niseme kwamba sifagilii kabisa vitendo vichafu vya aina yoyote ile kwa watoto na kama kweli walifanya hayo wanayotuhumiwa kufanya- they deserve to rot in jail.

Wikiend hii nilibahatika kukutana na mtu ambaye alitoa ushahidi kwenye hii kesi (Mwanamuziki na rafiki wa karibu wa Papii) na my feelings kwamba hawa jamaa walikua stitched up zimezidi kukua.Baadhi ya mambo aliyoniambia ni pamoja na kwamba baadhi ya tarehe na saa ambazo Papii anatuhumiwa kushiriki kwenye huo ufirauni- hakuwepo kabisa jijini Dar na hata pale alipokuwepo Dar, alikua yuko jukwaani akifanya kile anachopenda kufanya.Jambo jingine la kushangaza pia ni usiri mkubwa wa jinsi ambavyo kesi hiyo iliendeshwa, na chanzo changu cha habari kinaamini kwamba kwa sababu hii ushahidi mkubwa na wa maana umetiwa kapuni.Hadi leo huyu jamaa anamtembelea Papii gerezani na anasema huwa anagoma kula kwa siku kadhaa na kushinda akilia tu, anatamani afe kuliko kuendelea kuishi na machungu ya uonevu aliofanyiwa yeye pamoja na nduguze.

Nimesikia mengi kuhusu hii kesi- ambalo ni common kwa wengi ni kwamba Mzee Nguza aliingia anga fulani za Waziri mmoja wa serekali ya sasa na waziri huyo aliahidi kumkomesha- yeye pamoja na familia yake.Kuna baadhi wanasema sio Waziri ni Balozi fulani. Kwa jinsi nionavyo mimi, inawezekana labda watoto wakafanya kitu kama hiki peke yao bila baba yao and the vice versa is possible.Lakini kweli inaingia akilini kwa mzee mzima wa kiafrika kufanya huo upuuzi mbele ya wanae huku wakipokezana tena kwa kitoto kidogo?

Rumours zimekua nyingi kwenye hii kesi - kuna yeyote anayeujua ukweli wa hii kesi? I understand kwamba hawa jamaa walikata rufaa na ikatupwa, is there any other way anyone can help them?

Jamani najua wote mmekuwa mna shauku ya kutaka kujua kama Babu seya kaonewa au la. Baada ya kutambua kuwa wengi wenu hamna taarifa za kutosha nimeonela leo baada ya kusita mno niwaletee Rufaa ya kesi ya Babu Seya katika mahakama kuu ambayo imekatiwa rufaa. Baada ya kusoma naomba wewe mwenyewe kwa nafasi yako ujiridhishe. Je ni kweli hawa watu walionewa?

Tafadhali tazama kiambatisho.
 

Attachments

  • Nguza-Vicking-High-Court.doc
    171.5 KB · Views: 148
hata mie nasema kweli hii kesi pamoja na kusema ina ushahidi wote kuwa walitenda kosa
haijawahi kuniingia kichwani na haitaniingia kamwe zaidi mwamuzi wa yote ni mungu kama ni kweli au si kweli
 
Nje ya mada kidogo, Bluray uko wapi mkuu?

Kuna sehemu kwenye hiyo attached doc wameandika:

voire dire examination

Lakini siamini kama ilitakiwa kuonekana hivyo, sio voir dire examination?

Well, ni ndefu sana (35 pages) lakini ni muhimu kuisoma kujua undani wa kesi yenyewe
 
Nje ya mada kidogo, Bluray uko wapi mkuu?

Kuna sehemu kwenye hiyo attached doc wameandika:

voire dire examination

Lakini siamini kama ilitakiwa kuonekana hivyo, sio voir dire examination?

Well, ni ndefu sana (35 pages) lakini ni muhimu kuisoma kujua undani wa kesi yenyewe

mie nimeprint nitasoma home ni ndefu sana
 
mie nimeprint nitasoma home ni ndefu sana
Haya maandishi ya wanasheria usihangaike kusoma yoooooooote, nimesome vipengele kadhaa na kupata kujua kuwa nini wamelenga... Wanazunguuuuka kufanya reference za kesi za miaka hiyo mfano ukurasa wa 4 mpaka 14 nadhani ni reference za kesi tu, unaachana nazo... Pia kuna errors kadhaa ambazo zinatakiwa kurekebishwa, uzuri ni kuwa Tanzania mtu akiandika 'gay' badala ya 'guy' hata mahakamani wanajifanya wamemwelewa kuwa alitaka kuandika 'guy' kakosea kidogo.

Nasubiri kuona wanasheria wetu wanasemaje kuhusiana na utetezi huu
 
kulikuwa na rumours kuwa ni mganga wa kienyeji ndio alitoa hayo masharti kwa babu seya na familia yake kuharibu watoto. Ni kweli ni rahisi kuwaza kuwa kwa mwafrika kufanya kitendo kama hicho kwa kushirikiana na watoto wake sio rahisi lakini kwa upande mwingine, kwa mwafrika kuamini maagizo ya mganga wa kienyeji ni rahisi kuliko kuamini ushauri wa daktari.

Amini usiamini waganga wa kienyeji wakitoa (kama mkwara)tamko leo kua kila aziniye atakufa baada ya siku saba, UKIMWI utakuwa ndio kwa heri.

Nani kakwambia kila Mwafrika anaamini waganga wa kienyeji ?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom