Ushahidi wote uliopo ni kwamba ni kweli hao Nguza na wanawe walifanya huo ufirauni. Sijui sababu yao ya kufanya hivyo ilikuwa nini. Wanaharakati wa haki za watoto na za binadamu walishiriki pia kwenye hiyo kesi, na kuna mafaili ya kutisha sana. Watoto waliofanyiwa hivyo wapo na walitoa ushahidi, ambao kisheria ili kulinda haki za mtoto aliyelawitiwa na kumkinga dhidi ya unyanyapaa, haipaswi kufanywa hadharani na wala majina yao hayatolewi kwenye vyombo vya habari. Mafaili ya Muhimbili walikopimiwa hao watoto na ripoti za madaktari zipo. Yaani hii ilikuwa soo, hawakuwa na jinsi ya kukwepa.
Na huy si wa kwanza. Miaka ya mwisho ya 1980's alitokea fundi mshona nguo akiitwa Ali Maumba, alikuwa akiwafanyia watoto mchezo huohuo, na alilawiti zaidi ya 100, ila wengine wazazi wao waliwazuia wasijitokeze ili kukwepa aibu kwa familia zao. Ile kesi Maumba alihukumiwa kifungo, lakini alipokata rufaa alishinda kutokana na ushahidi "dhaifu" wa madaktari. Na ile kesi ya Maumba hadi leo inatumika kama reference ya kuwakumbusha madaktari umuhimu wa "ushahidi wa kitaaluma" (expert witness) kuandikwa vizuri. Rafiki zangu wanaharakati wamei-cite mara nyingi sana kwenye papers zao.
Hii ya kina Babu Seya, wanasheria walijaribu sana wakakosa pa kutokea. Na hata wakati wa rufaa, haikuwezekana, akaendelea kubaki hatiani.
Hizo habari za kuwasingizia kina nani sijui ni uvumi tu, kungekuwa na ukweli tungeshapata japo chembe ya ushahidi. Hao mnaowataja wakati huo hawakuwa na mamlaka yoyote dhidi ya mahakama, na hata katika kesi hakuna wakili au yeyote aliyeleta ushahidi wa kuwahusisha. Kama ni rushwa, sijui ni rushwa gani watu wangetembeza kila mahali kuanzia kwa watoto wa shule ya msingi, walimu wao, wenyeviti wa serikali za mitaa, askari polisi kwenye posts hadi kwa waendesha mashtaka, wanaharakati wa haki za watoto, mawakili, wafanyakazi wa idara za hospitali (wauguzi, watu wa records, maabara,madaktari, ili ati wote wafoji habari zinazoendana), hakimu mkazi kisutu, majaji wa mahakama kuu, majaji waheshimiwa sana wa mahakama ya rufaa, woote hao utawahonga vipi? Kazi ya ku-organize na ku-stage plot kama hii ni kubwa na haiwezi kuwa siri, lazima ziwepo flaws, hata kama ni fiction unatunga wasomaji wataona tu uongo ulipo!
Kwa hiyo sioni cha kujadili kuhusu Babu Seya na wanawe, alipata haki yake ya fair trial, akawa convicted, na sheria ikachukua mkondo wake. Akatumia pia haki yake ya appeal, nako hatukusikia malalamiko ya unfair trial, akabakia guilty as charged. Basi.