Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Sina hakika kama issue ya Mzee Nguza Viking na wanae iliwahi kukatwa hapa, by then ilipokuwa hot nilikua sija join JF.

Kwanza kabisa lazima niseme kwamba sifagilii kabisa vitendo vichafu vya aina yoyote ile kwa watoto na kama kweli walifanya hayo wanayotuhumiwa kufanya- they deserve to rot in jail.

Wikiend hii nilibahatika kukutana na mtu ambaye alitoa ushahidi kwenye hii kesi (Mwanamuziki na rafiki wa karibu wa Papii) na my feelings kwamba hawa jamaa walikuwa stitched up zimezidi kukua.

Baadhi ya mambo aliyoniambia ni pamoja na kwamba baadhi ya tarehe na saa ambazo Papii anatuhumiwa kushiriki kwenye huo ufirauni- hakuwepo kabisa jijini Dar na hata pale alipokuwepo Dar, alikuwa yuko jukwaani akifanya kile anachopenda kufanya.

Jambo jingine la kushangaza pia ni usiri mkubwa wa jinsi ambavyo kesi hiyo iliendeshwa, na chanzo changu cha habari kinaamini kwamba kwa sababu hii ushahidi mkubwa na wa maana umetiwa kapuni. Hadi leo huyu jamaa anamtembelea Papii gerezani na anasema huwa anagoma kula kwa siku kadhaa na kushinda akilia tu, anatamani afe kuliko kuendelea kuishi na machungu ya uonevu aliofanyiwa yeye pamoja na nduguze.

Nimesikia mengi kuhusu hii kesi- ambalo ni common kwa wengi ni kwamba Mzee Nguza aliingia anga fulani za Waziri mmoja wa serekali ya sasa na waziri huyo aliahidi kumkomesha- yeye pamoja na familia yake. Kuna baadhi wanasema sio Waziri ni Balozi fulani.

Kwa jinsi nionavyo mimi, inawezekana labda watoto wakafanya kitu kama hiki peke yao bila baba yao and the vice versa is possible. Lakini kweli inaingia akilini kwa mzee mzima wa kiafrika kufanya huo upuuzi mbele ya wanae huku wakipokezana tena kwa kitoto kidogo?

Rumours zimekuwa nyingi kwenye hii kesi - kuna yeyote anayeujua ukweli wa hii kesi? I understand kwamba hawa jamaa walikata rufaa na ikatupwa, is there any other way anyone can help them?

=====
Kuhusu hukumu, soma Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu

UPDATE:

Hatimaye waachiliwa kwa msamaha wa Rais. Habari zaidi soma...

Breaking News: - Mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na Mwanaye Johnson Nguza (Papii Kocha), watoka jela kwa msamaha wa Rais Magufuli
 
me nilisikia ni anga za huyo mtalii muungwana dats why pia yasemwa jamaa kutoka may be awe anavyoomba kwa Mungu kuwa atoke pia awe anamuombea mtalii atoke madarakani either kwa kusinda uchaguzi au lolote baya else angalau wasubirie mpaka 2015
Rumours ni nyingi sana kuhusu hii kesi na inanuka uonevu mtupu, fingers crossed labda tutapata mtu mwenye ukweli humu atushushie vitu.
 
Ushahidi wote uliopo ni kwamba ni kweli hao Nguza na wanawe walifanya huo ufirauni. Sijui sababu yao ya kufanya hivyo ilikuwa nini. Wanaharakati wa haki za watoto na za binadamu walishiriki pia kwenye hiyo kesi, na kuna mafaili ya kutisha sana. Watoto waliofanyiwa hivyo wapo na walitoa ushahidi, ambao kisheria ili kulinda haki za mtoto aliyelawitiwa na kumkinga dhidi ya unyanyapaa, haipaswi kufanywa hadharani na wala majina yao hayatolewi kwenye vyombo vya habari. Mafaili ya Muhimbili walikopimiwa hao watoto na ripoti za madaktari zipo. Yaani hii ilikuwa soo, hawakuwa na jinsi ya kukwepa.

Na huy si wa kwanza. Miaka ya mwisho ya 1980's alitokea fundi mshona nguo akiitwa Ali Maumba, alikuwa akiwafanyia watoto mchezo huohuo, na alilawiti zaidi ya 100, ila wengine wazazi wao waliwazuia wasijitokeze ili kukwepa aibu kwa familia zao. Ile kesi Maumba alihukumiwa kifungo, lakini alipokata rufaa alishinda kutokana na ushahidi "dhaifu" wa madaktari. Na ile kesi ya Maumba hadi leo inatumika kama reference ya kuwakumbusha madaktari umuhimu wa "ushahidi wa kitaaluma" (expert witness) kuandikwa vizuri. Rafiki zangu wanaharakati wamei-cite mara nyingi sana kwenye papers zao.

Hii ya kina Babu Seya, wanasheria walijaribu sana wakakosa pa kutokea. Na hata wakati wa rufaa, haikuwezekana, akaendelea kubaki hatiani.

Hizo habari za kuwasingizia kina nani sijui ni uvumi tu, kungekuwa na ukweli tungeshapata japo chembe ya ushahidi. Hao mnaowataja wakati huo hawakuwa na mamlaka yoyote dhidi ya mahakama, na hata katika kesi hakuna wakili au yeyote aliyeleta ushahidi wa kuwahusisha. Kama ni rushwa, sijui ni rushwa gani watu wangetembeza kila mahali kuanzia kwa watoto wa shule ya msingi, walimu wao, wenyeviti wa serikali za mitaa, askari polisi kwenye posts hadi kwa waendesha mashtaka, wanaharakati wa haki za watoto, mawakili, wafanyakazi wa idara za hospitali (wauguzi, watu wa records, maabara,madaktari, ili ati wote wafoji habari zinazoendana), hakimu mkazi kisutu, majaji wa mahakama kuu, majaji waheshimiwa sana wa mahakama ya rufaa, woote hao utawahonga vipi? Kazi ya ku-organize na ku-stage plot kama hii ni kubwa na haiwezi kuwa siri, lazima ziwepo flaws, hata kama ni fiction unatunga wasomaji wataona tu uongo ulipo!

Kwa hiyo sioni cha kujadili kuhusu Babu Seya na wanawe, alipata haki yake ya fair trial, akawa convicted, na sheria ikachukua mkondo wake. Akatumia pia haki yake ya appeal, nako hatukusikia malalamiko ya unfair trial, akabakia guilty as charged. Basi.
 
kulikuwa na rumours kuwa ni mganga wa kienyeji ndio alitoa hayo masharti kwa babu seya na familia yake kuharibu watoto. Ni kweli ni rahisi kuwaza kuwa kwa mwafrika kufanya kitendo kama hicho kwa kushirikiana na watoto wake sio rahisi lakini kwa upande mwingine, kwa mwafrika kuamini maagizo ya mganga wa kienyeji ni rahisi kuliko kuamini ushauri wa daktari.

Amini usiamini waganga wa kienyeji wakitoa (kama mkwara)tamko leo kua kila aziniye atakufa baada ya siku saba, UKIMWI utakuwa ndio kwa heri.
 
Katika mambo ambayo nina mpango wa kuyafanya in 2008 ni kuwatembelea hawa mabwana huko gerezani walipo na nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuujua upande wao wa hii story na kuwaletea hapa. Kwa mazingira yetu ya bongo yalivyo,kama agizo limetoka juu, najua kila kitu kinawezekana coz kila mtu anataka kulinda kitumbua chake.
 
Nadhani,wana jf kwenye hii hoja wengi wetu tuko single minded,either kwa ushabiki tu ama kwa mahusiano binafsi na kina nguza,ni vigumu saana kuwa karirisha watoto ushahidi,na pia kama walivo sema wengine,huwezi kuhonga legal system yote kuna mahala utachemka tu,kikubwa hapa,kuna hali ya ushirikina,hawa mabwana,walidanganywa na mganga wao wa kienyeji,ambaye kwa sasa ni marehemu,kwamba wajifanya hivyo wabebe mabaki yanayotoka kwa watoto wampelekee watarudisha umaarufu wao ulioanza kupotea,and they did it,what happened later,wote tumashahidi.
 
Nadhani,wana jf kwenye hii hoja wengi wetu tuko single minded,either kwa ushabiki tu ama kwa mahusiano binafsi na kina nguza,ni vigumu saana kuwa karirisha watoto ushahidi,na pia kama walivo sema wengine,huwezi kuhonga legal system yote kuna mahala utachemka tu,kikubwa hapa,kuna hali ya ushirikina,hawa mabwana,walidanganywa na mganga wao wa kienyeji,ambaye kwa sasa ni marehemu,kwamba wajifanya hivyo wabebe mabaki yanayotoka kwa watoto wampelekee watarudisha umaarufu wao ulioanza kupotea,and they did it,what happened later,wote tumashahidi.
Kama nilivyosema mwanzo, rumours ni nyingi sana kuhusu hii issue, hata haya unayoyasema I believe umeyapata kwa utaratibu huohuo.
 
nachojua mie if someone is having some powers juu huko nothing is impossible alafu kitu chenyewe kikiwa kama kuhonga na kutoa rushwa tuu??what wud have been the price for all of those waliohusika kwenye kesi??kama kuna rushwa kwa ajili ya mikataba ya mabilioni na hata wakati wa uchaguzi ndio sembuse kuhonga watoto na family zao na mahakama ambapo kesi iliendeshwa kimya kimya mpaka mwisho ndo ikajulikana kilichokua cha take place ndani?

Ok pia siwezi kurule out hilo la uchawi na uganga wa kienyeji lakini ndugu zanguni hebu tuingie ubinadamu kweli kabsaa baba wa familia na wanawe wawafanyie vile vitoto ufirauni ulee kweli?

Tatu kulikua na appeal kwa ajili ya yule mtoto wa nguza mmoja ambae alikua under 18 sheria yasema mtoto under 18 hawezi hukumiwa kifungo cha maisha naomba nisaidiwe kuhusu hili ilikuaje nalo likamalizwa kichini chini?

As may be kuna sheriaz zingine hazitumiki?
 
nachojua mie if someone is having some powers juu huko nothing is impossible alafu kitu chenyewe kikiwa kama kuhonga na kutoa rushwa tuu??what wud have been the price for all of those waliohusika kwenye kesi??kama kuna rushwa kwa ajili ya mikataba ya mabilioni na hata wakati wa uchaguzi ndio sembuse kuhonga watoto na family zao na mahakama ambapo kesi iliendeshwa kimya kimya mpaka mwisho ndo ikajulikana kilichokua cha take place ndani?

Ok pia siwezi kurule out hilo la uchawi na uganga wa kienyeji lakini ndugu zanguni hebu tuingie ubinadamu kweli kabsaa baba wa familia na wanawe wawafanyie vile vitoto ufirauni ulee kweli?

Tatu kulikua na appeal kwa ajili ya yule mtoto wa nguza mmoja ambae alikua under 18 sheria yasema mtoto under 18 hawezi hukumiwa kifungo cha maisha naomba nisaidiwe kuhusu hili ilikuaje nalo likamalizwa kichini chini?

As may be kuna sheriaz zingine hazitumiki?

Hakuna mtu ambaye amelivalia hili suala njuga na kuamua kutafuta ukwel - labda kwa kuwa hakuna mwenye uchungu nao, na nahisi aliefanya huu uonevu alijua akifunga mmoja wengine watawaambia watu ukweli.

Ukifuatilia unaweza kuta labda hizo reports zimeandikwa na wakuu wa hizo Idara na sio watu ambao wanafanya hizo kazi kila siku- hii pia ni possibility, naamini kabisa kama order inatoka juu, kila kitu kinawezekana.

Tumeona jinsi 'special clearance' zilivyotumika kuchota billions tena siku ambayo hata sio ya kazi, unadhani hapa yule cashier wa kila siku ambaye hii ni kazi yake alihusishwa? siku hiyo Gavana anakua kwenye 'kidirisha'.
 
The case was held in camera utajuaje kuwa hao watoto walitoa ushahidi kikamilifu. mimi nawashangaa watu wengine wanauchambuzi hafifu. yani mtu mzima na akili zeka anaweza kusema ni vigumu kutoa rushwa kwa mtiririko wa watu. Huyu yupo dunia ipi???

the first thing u have to know my friend is ukitaka kumpa mtu kesi kubwa wewe msingizie ubakaji. kesi hizi zina hisia kwa makundi ya wanawake na wazazi pia watamsapot the fake victim. mtuhumiwa hautasikizwa na kesi yako hasikizwi kama nyengine (the case is heard in camera) maana wanamlinda aliyebakwa.

i dont support rape cases maana mimi kama mzazi napinga ubakaji ila sipendi mtu atumie loop hole amkandamize mwengine. na pia sifahamu kama babu seya yuko innocent ama guilty ila kesi yake ilikuwa na mapungufu mengi sana kwa mtazamo wangu.
 
Na huy si wa kwanza. Miaka ya mwisho ya 1980's alitokea fundi mshona nguo akiitwa Ali Maumba, alikuwa akiwafanyia watoto mchezo huohuo, na alilawiti zaidi ya 100, ila wengine wazazi wao waliwazuia wasijitokeze ili kukwepa aibu kwa familia zao. Ile kesi Maumba alihukumiwa kifungo, lakini alipokata rufaa alishinda kutokana na ushahidi "dhaifu" wa madaktari. Na ile kesi ya Maumba hadi leo inatumika kama reference ya kuwakumbusha madaktari umuhimu wa "ushahidi wa kitaaluma" (expert witness) kuandikwa vizuri. Rafiki zangu wanaharakati wamei-cite mara nyingi sana kwenye papers zao.

Zenj alitokea jamaa kama huyu miaka ya tisini na alijulikana kama Kitangi.
 
Kesi za kusingizia Ubakaji zipo Nyingi..Kuna kesi kama 2 za Maustadh wa madrasa walisingiziwa hizi issue za ubakaji. Waliofanya haya walikuwa ni watu wa DINI ya kikristo, as the way kesi zilivyokuwa zikienda utajua NCHI HII wenyewe kina NANI?

Bahati nzuri mmoja kesi ilichukua almost mwaka au zaidi kusikilizwa...moja mzazi aliesingizia hakuwa akija mahakamani atlast Mmoja akaachiwa..Huyu wa Pili alikwenda Segerea nafikiri alikaa mwaka 1, then akatoka

Kimsingi Bongo mwenye Nguvu yoyote anaweza kukufunga, unasingiziwa UBAKAJI basi utalala rumande. Najua Mahakama zetu zilivyo haki ni NADRA Sana kupatikana.
 
Issue za Nguza kuna hear say nyingi sana..lkn mwenye data ni nani akiwa hana hata ndugu alie NJE anaeweza alau kutoa au kusema lolote... Mnakumbuka wale waliosingiziwa kumpindua mwalim...wangeoza...Mzee Mwinyi aliwaacha HURU...ipo haja wenye MAMLAKA wakatumia vizuri MAMLAKA YAO....UADILIFU UWE NDIO SLOGAN YAO
 
Assalam aleykum ndg zanguni,leo nimekaa na kutafakali sana jinsi nchi yetu inavyokwenda,kuanzia uongozi wa chini(tawi) mpaka huko juu,kuna mambo mengi sana ya vioja yanayofanyika na serikali kukaa kimya ama kwa makusudi au kwa kujifanya hawaoni kwa kujua kwamba watanzania ni wepesi wa kusahau.na kitu hicho kipo hapa JF,

Kitu ambacho kinaniuma siku zote na kitaendelea kuniuma ingawa kimetokea kitambo ni jinsi babu seya (nguza viking) na wanawe (papii kocha,nguza mbangu na francis) jinsi walivyohukumiwa kifungo kikubwa kwa sababu tu kesi ilikuwa imetengenezwa na kusimamiwa kidete na mabwana wakubwa wa serikali(mahita na wenzake),haiingii akilini mpaka leo kwa mtu ambaye anaitwa ALHAJI kumwadhibu mtu na familia yake tena kwa SABABU anataka kuilalisha DHINAA(kadhulumiwa kimada wake),

hili jambo ingawa limetokea kitambo lakini lazima tufahamu kuwa wale ni viumbe ambao wanateseka gerezani kwa kesi ya kubambikwa hivyo wanaJF lazima tuwe na utaratibu wa kuyakumbushia na kuendelea kuyakemea mabaya yote ya serikali bila kujali kuwa ni muda gani umepita!
 
Karibu sana Mtimti,
Hii issue ilishakatwa hapa kwa kirefu, nadhani ulikuwa hujajoin bado.
 
Je kulisemwa nini na muhimu? Dataz za wakati ule nz za sasa unaweza kukuta ziko tofauti na hivyo kila kitu kuwa na sura tofauti. Mie wakati ule sikuwemo humu ndani ya JF. Ukiweza tujulishe kwa mbalimbali maana hata mimi nilisikia kuwa ule wimbo wa Seya tutoke wote ambazo Nguza anamvalisha mtoto PETE ulisababisha yote haya.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom