Evari77
JF-Expert Member
- Apr 25, 2015
- 769
- 800
Tupo mkoani Na Vifaa tunavyo mnaposema mafundi wa mkoani ndio bure sio kweli sisi si kanjanja kama hapo agrey
Tupo mkoani Na Vifaa tunavyo mnaposema mafundi wa mkoani ndio bure sio kweli sisi si kanjanja kama hapo agrey
Zamu yangu kutumia scrudreva...Screwdriver moja wanashare Mafundi 7 [emoji23]
Sasa mkuu kama ni kubadilisha vioo tu mashine ya kuchania vioo kwenye 200k si unabakiwa na chenji kidogo? Je, lamination machine ya vioo umeipigia hesabu kwenye hiyo 200k yako.Hizo gharama ulizotaja ni kubwa mno kwa Basic Phone Rapair kama kubadili vioo, betri, kufix speaker nk. Phone Repair Tool Kit haizidi 200k kama unaagiza.
Mkuu hongera kwanza, naona umewekeza hasa ni wachache wanaojua thamani ya kuwa na tools advanced.
Nipe list ya hizo tools basic ambazo hazizidi 200k harafu nije na list yangu mkuu.Mbona hivyo vyote bei zake Kkoo za kawaida, we hizo bei umezitoa wapi?
Umezungumzia upande wa kuweka vioo, ila sekta hiyo ili ufanye kazi iionekane nzuri inabidi uwe na hela mkuu.Kwenye uzi wangu nilispoke vitu ambavyo very basic.
Kuna mahali popote nilizungumzia kuchomelea?
Upo mkoa gani?
Mkuu hongera kwa kunyoosha maelezo vizuri. Mtoa mada analalamika kuwa mafundi simu wanafanya kazi vibaya na huku anatoa vifaa ambavyo kwa kazi havina msaada wa uprofasional anaoutaka.Naona kuna kutokuelewana baadhi ya wachangiaji kee huu uzi.
Inatupasa tutambue hili kutoa huduma bora inategemea na uwekezaji gani umefanya.
Uwekezaji ninaozungumzia hapa ni elimu ya huduma husika kama ni ufundi inabidi ujue vizuri simu unazo deal nazo, ufahamu vizuri mifumo ya sakiti na ufanyaji kazi wake, uweze kusoma circuit diagrams na kuelewa kwa undani ufanyaji wake wa kazi, hizi zote ni elimu huwezi kukwepa haya ukategemea utakua fundi mzuri.
Jambo la pili ni vitendea kazi huwezi kutoa hudum ya kumridhisha mteja kwa kutumia vitendea kazi hafifu au visivyo na uwezo.
Mfano mdogo kuna ic zina pin hadi 68 na zaidi na ni ndogo sanaaa huwezi kuitoa na kuirudisha kwa kutumia tweezer na hot hair station na utegemee uirudishie ikae kama ulivyoikuta ni kitu ambacho huwezi kufanya bila usaidizi wa mashine za kisasa ambazo ni gharama sana kuzimiliki.
Hivyo hivyo kwenye vioo na parts nyingine inakubidi uwekeze sana ili upate kurahisisha ufanyaji wa kazi katika viwango vya juu.
CHANGAMOTO
Hizi ni changamoto za kwanini watu hawapo tayari kuwekeza pakubwa kwa hivyo vitu hapo juu.
1. Hali ya kipato kuwa chini
Watanzania wengi wanatumia simu za gharama ya chini sana tena hapo wamejipiga kweli, unapofanya uwekezaji mkubwa lazima uwe na uhakika wa kupata soko na mazingira mazuri ya kujiendesha kwa biashara kulingana na aina ya uwekezaji umefanya, haiwezekani unatumia microscope ya 4000$ kisha mteja anataka huduma ya 5000 lazima gharama za services ziwe juu ili uione faida.
Naweka mfano mdogo hapa kuna kiwanda kipo pale EPZ wanazalisha jeans high quality ila ni for export only, kwanini hawajaamua kuuzia soko letu la ndani? Jibu ni kwamba purchasing power yetu ni ndogo ndio mana wanapeleka masoko ya Europe na America.
Jeans moja mpaka 200USD, kwa akili ya kawaida ukiweka kiwanda cha kuuza jeans moja 460,000 mpaka 500,000 kwa mazingira ya Tanzania tunategemea utafunga biashara punde mzigo utakapokaa sokoni na kuuza jeans 50 tu kati ya 10000 ulizozalisha.
2. Mafundi wengi wanachukua ujuzi kwa vitendo kwa kuangalia mafundi wenzao bila, ni vizuri kupata mafunzo ya vitendo lakini ni vizuri zaidi kupata elimu ya darasani juu ya huo ufundi wako, itakupunguzia kufanya kazi kwa kubahatisha mana utakua unajua jinsi mifumo ifanyavyo kazi bila kujaribu jaribu au kwa lugha ingine utapata pa kuanzia.
3. Ubobevu / Specialisation
Mafundi wengi ni jack of all trades master of none, yaani wanataka/wanapenda kufanya mambo mengi kumbe unaweza kujikita kwenye jambo moja tu ukalifanya kwa ufanisi wa 85% kuliko kufanya mengi kwa ufanisi wa 30%
Hapa nazungumzia kama ni software jikite kwneye sw kwa 100%
Kama ni hardware jikite kwenye hardware kwa %100
Kuna watu wapo makini sana kwenye disassembly na assembling jikite kwenye vioo kazi yako itaheshimika na kila mtu atakutambua kwenye ujuzi wako na utafanya bila hofu maana umekwiva huko.
Mwisho.
Acha uwongo we chizi...hio million 30 NI duka la simu au?
Mimi nadhani kwa haraka haraka tasnia Ina muelekeo sio mbaya Sana ni kuboresha tu baadhi ya mambo almost mtaji wa million tano unatosha kabsa.
Labda nikuulize nitajie vifaa ambavho vina cost pesa nyingi kwenye ufundi simu
Note: Wabongo asilimia kubwa hatuna simu original hivyo mambo ya software sio tatizo Sana na uzuri memgi solution zake zinapatikana hata ukimpata Google ukapewa tips
Ishu NI kwenye hardware Kama alivyobainisha mtoa maada..mambo ya iPhone n.k kawaelekeze watu wa marekani
Hapa bongo Kuna work shop ya fund sim kweli?huna uekewa ktk inshu za simu ndugu ndyo maana umepinga swala hilo ya work shop iliyo kamilika kila kitu vifaa vyote vya kutengeneza simu thamani yake ni zaidi ya hyo milioni 30 yani ukiwa na vifaa vya kisasa vyote hakuna simu utamwambia mteja sulimu imekufa mashine wala nini kila kitu kita kaa vzr
Zipo ila ni chache na gharama zao zimesimama. Kuna moja naifahamu wao wanatengeza iphone pekee hizi android labda simu iwe flagship ndo wanatengeneza.Hapa bongo Kuna work shop ya fund sim kweli?
Nahitaji kam! Hii mkuuSoldering Iron ya Laki 7 ndio ikoje?
View attachment 2264395
Hiyo kitu me nimenunua hata 70k haifiki, unachoma kwa mkono mmoja tu.
Huu mwaka wa pili naitumia ofisini kwangu(kuna kazi huwa zinahitaji soldering). Haina hata dalili ya kufa.,
Nilianza kwa ufundi simu kwa mtaji ambao haukufika hata milioni moja mwaka 2017. Vifaa pekee nilivyokuwa navyo ni hot air blower, soldering gun na screwdrivers. Nilifanya miaka minne mpaka 2022 na kuanizisha biashara tofauti kwa pesa niliyoingiza kupitia ufundi simu. Ile ofisi ya simu mpaka leo ipo na mdogo wangu ameiendeleza na kaikuza mpaka kufikia kwenda kupanga frem ya 250,000 wakati nilipoanza mimi ilikuwa fremu ya 100,000 tu.Mtaji wa chini kuwa fundi simu ni milioni 30. Hapo kuanzia vifaa na spare na kila kitu yani mteja akija sijui tuulize dukani bei ya kioo sijui nini.
sekta hii imevamiwa ndio maana hakuna mwenye uelekeo wa hii biashara japo inalipa vizuri.
ukitaka kuwa software fix za simu mtaji wachini ni milioni 45.
hakuna simu yoyote itasumbua na utanunua leseni za software za makampuni na kutambulika .
Apple certified tu wanaka usd 5600 kupata access na ukizi vigezo chungu mzima.
[emoji23] kiufupi ukiwa na milioni 100 kurudi kwa kasi kubwa ni kugusa.
I been doing this too.. yaani ni workshop maskani ya ku repair PC na simu zangu tu... Vitu na agiza AliExpress huko!Wala siyo tangazo after all mimi si fundi simu japo simu zangu zikizingua nilishaacha kupeleka kwa mafundi. Naagiza spare nafunga.