Kero za mafundi simu: Wengi wapo local sana

42774277

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
6,833
8,811
Sijui ni mimi tu mafundi niliowahi kutana nao au lah. Kama kule Kariakoo. Mitaa kama Aggrey na Uhuru zina mafundi simu wengi ila wengi kama siyo wote ni miyeyusho. Mikoani huko ndo kabisa.

1. Unakuta fundi hana hata hot air blower gun au hata kama anayo hajui matumizi yake. Unampelekea simu unataka kubadili battery. Simu ina back glass, anaanza kuforce kutoa back glass kwa kuingiza vitu mule pembeni. Sometimes anaishia kuivunja, ukiwasha moto unaanza kuonekana mkali.

2. Kuweka gundi. Yaani fundi simu anakuwekea magundi mengi kazi inakuwa mbaya hata haivutii. Mbaya zaidi anaweka hayo magundi halafu hata glass yenyewe haishiki.

Wengi wanatumia B7000 glue lakini sidhani kama tatizo ni B7000. Maana ni gundi ambayo ina review nzuri mitandaoni.

IMG_20220526_150540.jpg

Nadhani shida siyo gundi ila shida ni kuipa hiyo Gundi mazingira inayotaka ila ishike vizuri. Hiki kipengele wengi wanafeli.

Suggestion; Badala ya kutumia hizo gundi tumieni double wall Adhesive tapes. Hizi tapes zipo specific kwa ajili ya simu husika au zipo ambazo ni multipurpose. 1mm au 2mm inafaa sana. Zinabana vizuri kuliko hayo magundi na kazi inakuwa safi.

IMG_20220526_152118.jpg

3. Fundi anakubadilishia kioo au back glass akimaliza anabana na Rubber band. Serious?????

Fundi unakosa hata vitu kama hivi?

747956789-1832172237.jpg

Au hii

-386348723-164292191.jpg

Yapo mengi ila kwa leo hayo matatu.

Mimi simu zangu narekebishia home maana unaweza kujikuta umemnasa fundi vibao.
 
Hili NI tangazo tukuletee kazi ama...natania

Back to the topic naunga mkono hoja mafundi wengi uchwara ujanja ujanja tu inabidi serikali itafute walimu 100 China huko wapewe ajira za muda Kama za sensa waje kuwafundisha mafundi Hawa short course ya kutengeneza simu nadhani NI eneo lingine ambalo likirasimishwa serikali itakusanya maduhuri yake vzr na kuongeza Pato wapewe leseni wawe walipa kodi baada ya kufundishwa mwezi Kisha wasajiliwe wakopeshwe hivyo vifaa wapige kazi...
 
Mtaji wa chini kuwa fundi simu ni milioni 30. Hapo kuanzia vifaa na spare na kila kitu yani mteja akija sijui tuulize dukani bei ya kioo sijui nini.

sekta hii imevamiwa ndio maana hakuna mwenye uelekeo wa hii biashara japo inalipa vizuri.

ukitaka kuwa software fix za simu mtaji wachini ni milioni 45.
hakuna simu yoyote itasumbua na utanunua leseni za software za makampuni na kutambulika .

Apple certified tu wanaka usd 5600 kupata access na ukizi vigezo chungu mzima.

kiufupi ukiwa na milioni 100 kurudi kwa kasi kubwa ni kugusa.
 
Mtaji wa chini kuwa fundi simu ni milioni 30.hapo kuanzia vifaa na spare na kila kitu yani mteja akija sijui tuulize dukani bei ya kioo sijui nini...
Acha uwongo we chizi...hio million 30 NI duka la simu au?

Mimi nadhani kwa haraka haraka tasnia Ina muelekeo sio mbaya Sana ni kuboresha tu baadhi ya mambo almost mtaji wa million tano unatosha kabsa.

Labda nikuulize nitajie vifaa ambavho vina cost pesa nyingi kwenye ufundi simu

Note: Wabongo asilimia kubwa hatuna simu original hivyo mambo ya software sio tatizo Sana na uzuri memgi solution zake zinapatikana hata ukimpata Google ukapewa tips

Ishu NI kwenye hardware Kama alivyobainisha mtoa maada..mambo ya iPhone n.k kawaelekeze watu wa marekani
 
Ukishajiita fundi ukawa unarekebisha vifaa vya watu hautakiwi kuwa mbahatishaji

Kuna mafundi wakidwanzi sana pale machinga

Kuna siku nilipeleka PC yangu sijui ilifakisha kitu gani ila ilikuwa ukiwasha kwenye screen pale hai display ila taa na feni zote ziko on

Sasa nikamfata fundi wa kwanza nikamueleza kwa mdomo tatizo la PC kisha nikamuuliza kwa ugonjwa huo inawezekana kupona.

Fundi akaniambia kwa tatizo lako itakubidi utoe 30k nikamwambia fresh nikampa PC akaifungua yote halafu akatoa RAM akawa anazisafisha.

Mi nimesizi pembeni kwenye kiti namcheki tu anavyo taka kuniibia kunitajia 30k kwa tatizo la kuisafisha RAM wakati hata mimi nikiwa home wazo la kwanza liikuwa kutoa RAM kusafisha na nikajaribu ku replace RAM zingine lakini bado sikuweza ku solve.

Fundi akawa inairudishia PC kwa kuifunga baada ya kusafisha RAM akiwa anajua mimi sielewi chochote.

Anamaliza kufunga sasa kila akiwasha ngoma kimya, nikamwambia mzee nipatie PC yangu niende kwa mafundi wengine huko mbele maana hapa nimepoteza zaidi ya nusu saa na PC bado haijawaka.

Akasema fresh chukua PC yako ila lazima unitoe buku 3 ya ufundi

Nikastaajabu, buku 3 kwa ufundi gani na wakati tatizo nililokuambia utatue kwenye PC yangu bado liko vile vile?

Akasema hiyo buku 3 haihusiani na ufundi hiyo ni gharama ya kufungua tu PC hata kama sija solve swala lako.

Nikamwambia ofsa hapa nina 35k, 30 nimeitenga kwa ajili ya kutengenezea PC na 5k kwa ajili ya nauli kurudi hoke

Sasa fikiria napita kwa mafundi kumi kwa ajili ya ku solve tatizk, halafu kila fundi naye kutana naye awe anachukua tatu tatu

Yani 30k itaisha kwa kuwapa mafundi kwa kazi ya kufungua PC bila ku solve tatizo kitu ambacho hata ungekuwa wewe nakuhakikishia usingeweza kukubali

Kama ni tatizo lenye kuhitaji kifaa cha gharama niambie hata kama sina hela mi nitajipanga lakini sio nikupe hela wakati tatizo langu lililonileta hujaweza kulitatua.
 
siku hizi waoga,simu zimekuwa ngumu sana sio za kuparamia utalipishwa usiamini.

kuna mshikaji alitoka kununua iphone x kufika home anaitoa tu ktk box ikamponyoka na kubamiza kioo cha nyuma, kioo cha camera kikaenda na maji, nikamwambia peleka kwa fundi ila wahi maana camera ikikaa wazi inaingia ukungu na kuutoa kwa mafundi wetu wa upepo ni kasheshe, kaenda wale jamaa wamemuwekea kile kioo,ila kina alama za vidole(fingerprint)kwa ndani, picha zinakosa mng'ao kabisa,na wamempiga 30k,nikajisemea ndio maama apple hawawaamini mbuzi mbuzi kama hawa.

kwa sasa nenda makongoro street,ukiona simu imekataliwa pale,jigeuzie zako home ukalale utapata kesi ya kupiga mtu tu,pale wakikwambia hii simu haitengenezeki wanakwambia kwa uzoefu.
 
siku hizi waoga,simu zimekuwa ngumu sana sio za kuparamia utalipishwa usiamini.

kuna mshikaji alitoka kununua iphone x kufika home anaitoa tu ktk box ikamponyoka na kubamiza kioo cha nyuma,kioo cha camera kikaenda na maji,,nikamwambia peleka kwa fundi ila wahi maana camera ikikaa wazi inaingia ukungu na kuutoa kwa mafundi wetu wa upepo ni kasheshe,kaenda wale jamaa wamemuwekea kile kioo,ila kina alama za vidole(fingerprint)kwa ndani,picha zinakosa mng'ao kabisa,na wamempiga 30k,nikajisemea ndio maama apple hawawaamini mbuzi mbuzi kama hawa.

kwa sasa nenda makongoro street,ukiona simu imekataliwa pale,jigeuzie zako home ukalale utapata kesi ya kupiga mtu tu,pale wakikwambia hii simu haitengenezeki wanakwambia kwa uzoefu.
Makongoro ni wapi mkuu
 
Sijui ni mimi tu mafundi niliowahi kutana nao au lah. Kama kule Kariakoo....mitaa kama Aggrey na Uhuru zina mafundi simu wengi ila wengi kama siyo wote ni miyeyusho. Mikoani huko ndo kabisa....

1. Unakuta fundi hana hata hot air blower gun au hata kama anayo hajui matumizi yake. Unampelekea simu unataka kubadili battery. Simu ina back glass, anaanza kuforce kutoa back glass kwa kuingiza vitu mule pembeni. Sometimes anaishia kuivunja, ukiwasha moto unaanza kuonekana mkali.

2. Kuweka gundi. Yaani fundi simu anakuwekea magundi mengi kazi inakuwa mbaya hata haivutii. Mbaya zaidi anaweka hayo magundi halafu hata glass yenyewe haishiki.

Wengi wanatumia B7000 glue lakini sidhani kama tatizo ni B7000. Maana ni gundi ambayo ina review nzuri mitandaoni.

View attachment 2239376

Nadhani shida siyo gundi ila shida ni kuipa hiyo Gundi mazingira inayotaka ila ishike vizuri. Hiki kipengele wengi wanafeli.

Suggestion; Badala ya kutumia hizo gundi tumieni double wall Adhesive tapes. Hizi tapes zipo specific kwa ajili ya simu husika au zipo ambazo ni multipurpose. 1mm au 2mm inafaa sana. Zinabana vizuri kuliko hayo magundi na kazi inakuwa safi.

View attachment 2239388

3. Fundi anakubadilishia kioo au back glass akimaliza anabana na Rubber band. Serious?????

Fundi unakosa hata vitu kama hivi?

View attachment 2239391

Au hii

View attachment 2239392

Yapo mengi ila kwa leo hayo matatu.

Mimi simu zangu narekebishia home maana unaweza kujikuta umemnasa fundi vibao.
Hawawapiti wanasheria/mawakili.
 
Hili NI tangazo tukuletee kazi ama...natania

Back to the topic naunga mkono hoja mafundi wengi uchwara ujanja ujanja tu inabidi serikali itafute walimu 100 China huko wapewe ajira za muda Kama za sensa waje kuwafundisha mafundi Hawa short course ya kutengeneza simu nadhani NI eneo lingine ambalo likirasimishwa serikali itakusanya maduhuri yake vzr na kuongeza Pato wapewe leseni wawe walipa kodi baada ya kufundishwa mwezi Kisha wasajiliwe wakopeshwe hivyo vifaa wapige kazi...
Wala siyo tangazo after all mimi si fundi simu japo simu zangu zikizingua nilishaacha kupeleka kwa mafundi. Naagiza spare nafunga.
 
Mtaji wa chini kuwa fundi simu ni milioni 30.hapo kuanzia vifaa na spare na kila kitu yani mteja akija sijui tuulize dukani bei ya kioo sijui nini.

sekta hii imevamiwa ndio maana hakuna mwenye uelekeo wa hii biashara japo inalipa vizuri.

ukitaka kuwa software fix za simu mtaji wachini ni milioni 45.
hakuna simu yoyote itasumbua na utanunua leseni za software za makampuni na kutambulika .

Apple certified tu wanaka usd 5600 kupata access na ukizi vigezo chungu mzima.

kiufupi ukiwa na milioni 100 kurudi kwa kasi kubwa ni kugusa.
Mimi ninezungumza vitu basic tu ambavyo hata mtaji wa 300k kwa vifaa nilivyotaja haifiki.

Achana na mambo ya kuwa Apple Certified.
 
Kingine siachii fundi simu, kama haiwezekani kuisubiria bora nikalale nayo nyumbani ikiwa mbovu nitarudi kesho kuliko kuiacha halafu tuzungushane na kupigana kiswahili simu yangu hunipi dukani haupo mradi kuboana tu
 
Hahahahah
 
Mimi ninezungumza vitu basic tu ambavyo hata mtaji wa 300k kwa vifaa nilivyotaja haifiki.

Achana na mambo ya kuwa Apple Certified.

sawa ila kwa sasa kuendana na soko hapo utakuwa unachekesha.

zamani simu ilikuwa simple tasnia ya ufundi ila kila siku inazidi kuwa advance.nikuulize tu mfano iwatch imepata short kuna fundi gani hapa !.

na kozi hizo mtu anasafiri kwenda nje kusoma !

leo kuna simu zinafunguliwa na vifaa maalumu na kila siku matoleo yanatoka !

Kama utokubaliana na mimi utalalamika sana humu ujukwaani.
 
Nimeongea vitu basic sana mkuu ambavyo mafundi wengi hawana.

Acheni kutafuta kichaka cha kujifichia kwenye mambo sijui ya shoti.n.k.

I think hujanielewa.
 
Yangu imekufa IC ya Bluetooth/WiFi, nikapeleka KKOO wakanambia tu kuwa hii haiwezekani. Nikaamua ishi na nalo hivyo hivo
 
Ukishajiita fundi ukawa unarekebisha vifaa vya watu hautakiwi kuwa mbahatishaji

Kuna mafundi wakidwanzi sana pale machinga

Kuna siku nilipeleka PC yangu sijui ilifakisha kitu gani ila ilikuwa ukiwasha kwenye screen pale hai display ila taa na feni zote ziko on

Sasa nikamfata fundi wa kwanza nikamueleza kwa mdomo tatizo la PC kisha nikamuuliza kwa ugonjwa huo inawezekana kupona.

Fundi akaniambia kwa tatizo lako itakubidi utoe 30k nikamwambia fresh nikampa PC akaifungua yote halafu akatoa RAM akawa anazisafisha.

Mi nimesizi pembeni kwenye kiti namcheki tu anavyo taka kuniibia kunitajia 30k kwa tatizo la kuisafisha RAM wakati hata mimi nikiwa home wazo la kwanza liikuwa kutoa RAM kusafisha na nikajaribu ku replace RAM zingine lakini bado sikuweza ku solve.

Fundi akawa inairudishia PC kwa kuifunga baada ya kusafisha RAM akiwa anajua mimi sielewi chochote.

Anamaliza kufunga sasa kila akiwasha ngoma kimya, nikamwambia mzee nipatie PC yangu niende kwa mafundi wengine huko mbele maana hapa nimepoteza zaidi ya nusu saa na PC bado haijawaka.

Akasema fresh chukua PC yako ila lazima unitoe buku 3 ya ufundi

Nikastaajabu, buku 3 kwa ufundi gani na wakati tatizo nililokuambia utatue kwenye PC yangu bado liko vile vile?

Akasema hiyo buku 3 haihusiani na ufundi hiyo ni gharama ya kufungua tu PC hata kama sija solve swala lako.

Nikamwambia ofsa hapa nina 35k, 30 nimeitenga kwa ajili ya kutengenezea PC na 5k kwa ajili ya nauli kurudi hoke

Sasa fikiria napita kwa mafundi kumi kwa ajili ya ku solve tatizk, halafu kila fundi naye kutana naye awe anachukua tatu tatu

Yani 30k itaisha kwa kuwapa mafundi kwa kazi ya kufungua PC bila ku solve tatizo kitu ambacho hata ungekuwa wewe nakuhakikishia usingeweza kukubali

Kama ni tatizo lenye kuhitaji kifaa cha gharama niambie hata kama sina hela mi nitajipanga lakini sio nikupe hela wakati tatizo langu lililonileta hujaweza kulitatua.
Bongo njaaa sana, ufundi ni taaluma sio vitu vya kubumba, wengi njaa sana, ilaufundi ukawa expert wa kitu flan utapiga sana hela na utakuwa unaringa
 
Back
Top Bottom