Kero za daladala

jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,075
684
Katika jiji la Dar es Salaam nadhani hili linaongoza hasa kwa wale tunaotumia usafiri huu ambao ustaarabu ni zero, unakuta mtu umesimama kituoni masaa mawili kusubiri daladala, alhamudulilah linakuja unapigana kupata siti unaingia hapo uko hoi unajilaza kwenye siti angalau upumzishe mwili na akili baada ya pilika pilika za siku nzima na uchovu wa kusubiri daladala unakuta limtu linawasha redio au anasikiliza mziki kwa simu alafu anaweka loud...:confused::confused::confused::confused:

Bahati mbaya simu ni zile za ef 10 can you imagine zile kelele
unamwambia angalau apunguze kidogo yani hapo ndo unachokoza anaweza kutukana njia nzima hadi anashuka.

Kwakweli mjirekebishe wenye hio tabia, muwe wastaarab tumieni headfones.
 
Hizo kero zilikuwepo,zipo na zitaendelea kuwepo kwa sababu dala dala ni usafiri wa umma. Wale wanaokereka mara nyingi wanatumia yale magari madogo yenye namba ubavuni au ya kwao.
 
Hizo kero zilikuwepo,zipo na zitaendelea kuwepo kwa sababu dala dala ni usafiri wa umma. Wale wanaokereka mara nyingi wanatumia yale magari madogo yenye namba ubavuni au ya kwao.

Hapana mkuu, hata kama ni usafiri wa umma na wa watu wengi, lazima kuwe na utaratibu na ustaarabu. Kila mtu akifungua radio kwa sauti itakuwaje.

Kushindwa kupanda taxi au kumiliki gari isiwe sababu ya kunyanyasika kupita kiasi.
 
ni kweli hatuwezi kila mtu kua na gari lakin angalau tukiwa wastaarab inatosha.....yan wengine akipanda kwenye gar n vurugu akishuka mnahema
 
Mi sahv kero za kwenye daladala nishazizoea, maana nilikuwa nakereka sana na wale wadada wa kutegesha mizigo{In shekhe Kipoozeo's voice}. Sahv nikimwambia mdada sogea, kama hataki akinitegeshea mzigo na namsogezea dushe, nabambia mwanzo mwisho
 
Si ukodi Tax au nunua gari yako kama utaki kero

Mkuu, gari au tax hauzaliwi navyo, kuna hatua utapitia hadi uje kuvimiliki. Wewe unaweza kuwa uwezo, kumbuka una ndugu na jamaa wanautegemea huo usafiri wa daladala, tunachoongelea hapa ni kiwango kidogo tu cha ustaarab.
 
Kuna siku tulipanda daladala na RASTA ebhana Tulikuwa reggae mwanzo mwisho yaani RASTA haelewi full kurukaruka kwenye daladala Daaah nikiikumbuka hii siku sijui jamaa alishakula mjani
 
Hapana mkuu, hata kama ni usafiri wa umma na wa watu wengi, lazima kuwe na utaratibu na ustaarabu. Kila mtu akifungua radio kwa sauti itakuwaje.

Kushindwa kupanda taxi au kumiliki gari isiwe sababu ya kunyanyasika kupita kiasi.
Ni ustaarabu tu na si vinginevyo. Kulisema hadharani kama hivi ni moja ya njia ya kulitokomeza. Pole na hongera kwa kuweza kusema.
 
kama wewe unavokua umechoka na kuvurugwa unajipumzisha kwa kulala mwenzio kachoka zaidi na anapunguza mawazo kwa kusikiliza muziki, ndivyo ilivyo kwenye maroli yetu na dereva hii haimuhusu kabisa
 
kama wewe unavokua umechoka na kuvurugwa unajipumzisha kwa kulala mwenzio kachoka zaidi na anapunguza mawazo kwa kusikiliza muziki, ndivyo ilivyo kwenye maroli yetu na dereva hii haimuhusu kabisa

Hujaelewa mkuu inawezekana madereva n wastaarab ukimwambia punguza saut atapunguza ila sio abiria vichwa maji
 
Hapana mkuu, hata kama ni usafiri wa umma na wa watu wengi, lazima kuwe na utaratibu na ustaarabu. Kila mtu akifungua radio kwa sauti itakuwaje.
Wapanda dala dala ni watu wa aina tofauti, kuna wasomi na wasiosoma, kuna wastaarabu na wasiostaarabika, kuna wabishi, watukutu, wapole, wasemaji sana na wengineo wengi. Vile vile kuna dhana kuwa hakuna anayekufahamu (anonimity) hivyo kuchangia uwepo wa tabia za ajabu. Elimu kwa haya makundi inaweza kusaidia ila changamoto ni nyingi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom