black hawk87
JF-Expert Member
- Jan 25, 2020
- 678
- 1,243
Hv Kati ya polis na raia na anamshawish rushwa mwenzie??? Tuanzie hapo ifikie kipind nyuma ya keyboard tusiongee unafk wakat tukikamatwa na makosa wenyew ndio tuna waanza Sasa wao wafanyaje??? Bas tuache tusiwape watugonge fine tu za kutosha huu unafki ifikie kipind uishe ushaona polisi anakushawish umpe pesa Bali ss wenyewe na vielf tano vyetu ndio tunawashawish.Uzoefu wa kusafiri barabarani kabla, baada na wakati Kangi Lugora akiwa waziri wa mambo ya ndani unahusika.
Kangi Lugora alipoteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani, alileta mageuzi makubwa chanya katika idara ya polisi na hasa kwenye kitengo cha usalama barabarani.
Bambika bambika ya makosa yasiyokuwa na kichwa wala miguu vilipungua sana. Wenye vyombo vyama moto pamoja na madereva wakageuka kuwa wadau badala ya kuwa watuhumiwa wa uhalifu sugu na wahanga wakubwa wa rushwa tokea kwa maofisa polisi hawa wa usalama barabarani.
Kwenye haya ikumbukwe mabilioni ya shilingi ya faini ambayo kabla polisi usalama barabarani walikuwa wakijitanabaisha nayo kila leo kama mafanikio ya utendaji wao.
Matokeo ya haya yalikuwa kuchukiwa mno kwa polisi na hata serikali ya awamu ya tano.
Alipoingia mh. Kangi Lugora mambo yalibadilika ghafla. Uonevu na dhuluma za polisi zikashughulikiwa. Matangazo ya pesa za makusanyo yakakoma. Matochi ya kupiga kwa nyuma yakasitishwa. Matumizi ya simu binafsi za mkononi na picha za matochi zikastishwa. Ikawa ni lazima picha ya tochi iwe kwenye tochi si kwenye simu. Ubovu wa gari ukawa ni kosa moja, si tairi, taa, wiper, nk kama makosa tofauti.
Wananchi wakashangilia polisi wakachukia na wakamchukia mno mh. Kangi Lugora.
Hakuna shaka kuwa ni kwa nini wengine leo tunapo sikitika na kuondoka kwa Kangi Lugora polisi hawa wanashangilia na kufanya sherehe nzito maana dua zao zimemfika mwewe.
Hivi sasa hali ni mbaya labda kuliko kabla ya Kangi Lugora. Matochi ya kubambika yamerejea kwa kasi mno. Haya ni yote ya kupigwa mbele na nyuma na picha kutumwa hata umbali wa zaidi km 100 . Makosa ya kunyumbulisha ubovu wa gari yamerejea tena. Rushwa inadaiwa kama deni. Yaani ni vurugu mechi kweli kweli. Tutakimbilia wapi siye?
Inaonekana hawa ndugu wako busy kufidia walichokosa wakati wa Kangi.
Yote haya ni ajabu na kweli. Ina maana labda yote mema aliyofanya Kangi Lugora aliondoshwa nayo?
Shida kweli kweli.
Waziri Simbachawene kazi unayo. Hawa jamaa si wema yawezekana hata mh. Kangi Lugora alitengenezewa zengwe tu kutokana na chuki binafsi.
Hebu achen hzo mambo mnadhan hyo elfu thelathin Ni ndogo aiseee Bora umpoze ya maji mzee baba unasonga mbele kuliko 30 kwa wiki 37500 ikipita
kilicho akilini kitumie