Kero za barabarani baada ya Kangi Lugola kutumbuliwa

Uzoefu wa kusafiri barabarani kabla, baada na wakati Kangi Lugora akiwa waziri wa mambo ya ndani unahusika.

Kangi Lugora alipoteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani, alileta mageuzi makubwa chanya katika idara ya polisi na hasa kwenye kitengo cha usalama barabarani.

Bambika bambika ya makosa yasiyokuwa na kichwa wala miguu vilipungua sana. Wenye vyombo vyama moto pamoja na madereva wakageuka kuwa wadau badala ya kuwa watuhumiwa wa uhalifu sugu na wahanga wakubwa wa rushwa tokea kwa maofisa polisi hawa wa usalama barabarani.

Kwenye haya ikumbukwe mabilioni ya shilingi ya faini ambayo kabla polisi usalama barabarani walikuwa wakijitanabaisha nayo kila leo kama mafanikio ya utendaji wao.

Matokeo ya haya yalikuwa kuchukiwa mno kwa polisi na hata serikali ya awamu ya tano.

Alipoingia mh. Kangi Lugora mambo yalibadilika ghafla. Uonevu na dhuluma za polisi zikashughulikiwa. Matangazo ya pesa za makusanyo yakakoma. Matochi ya kupiga kwa nyuma yakasitishwa. Matumizi ya simu binafsi za mkononi na picha za matochi zikastishwa. Ikawa ni lazima picha ya tochi iwe kwenye tochi si kwenye simu. Ubovu wa gari ukawa ni kosa moja, si tairi, taa, wiper, nk kama makosa tofauti.

Wananchi wakashangilia polisi wakachukia na wakamchukia mno mh. Kangi Lugora.

Hakuna shaka kuwa ni kwa nini wengine leo tunapo sikitika na kuondoka kwa Kangi Lugora polisi hawa wanashangilia na kufanya sherehe nzito maana dua zao zimemfika mwewe.

Hivi sasa hali ni mbaya labda kuliko kabla ya Kangi Lugora. Matochi ya kubambika yamerejea kwa kasi mno. Haya ni yote ya kupigwa mbele na nyuma na picha kutumwa hata umbali wa zaidi km 100 . Makosa ya kunyumbulisha ubovu wa gari yamerejea tena. Rushwa inadaiwa kama deni. Yaani ni vurugu mechi kweli kweli. Tutakimbilia wapi siye?

Inaonekana hawa ndugu wako busy kufidia walichokosa wakati wa Kangi.

Yote haya ni ajabu na kweli. Ina maana labda yote mema aliyofanya Kangi Lugora aliondoshwa nayo?

Shida kweli kweli.

Waziri Simbachawene kazi unayo. Hawa jamaa si wema yawezekana hata mh. Kangi Lugora alitengenezewa zengwe tu kutokana na chuki binafsi.
Hv Kati ya polis na raia na anamshawish rushwa mwenzie??? Tuanzie hapo ifikie kipind nyuma ya keyboard tusiongee unafk wakat tukikamatwa na makosa wenyew ndio tuna waanza Sasa wao wafanyaje??? Bas tuache tusiwape watugonge fine tu za kutosha huu unafki ifikie kipind uishe ushaona polisi anakushawish umpe pesa Bali ss wenyewe na vielf tano vyetu ndio tunawashawish.

Hebu achen hzo mambo mnadhan hyo elfu thelathin Ni ndogo aiseee Bora umpoze ya maji mzee baba unasonga mbele kuliko 30 kwa wiki 37500 ikipita

kilicho akilini kitumie
 
Ndiyo maana nikasema wema wako hausafishi ubaya wako. Tenda mema 1000 lakini baya 1 tu linafuta mema yako yooote

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kwani wewe nani jitambulishe tukufahamu ili siku nyingine tukunukuu kwa maana waswahili wanasema 'kosa moja halifukuzishi mke'. Mwisho wa kunukuu.

Waswahili - kiwakilishi cha waungwana.

Bila shaka na 'kosa moja' unaloliongelea ni zengwe la kutengenezewa.

Kangi kaenda tuliokoshwa na utendaji wake tutamkumbuka. Hakika lilikuwa dume.
 
Hv Kati ya polis na raia na anamshawish rushwa mwenzie??? Tuanzie hapo ifikie kipind nyuma ya keyboard tusiongee unafk wakat tukikamatwa na makosa wenyew ndio tuna waanza Sasa wao wafanyaje??? Bas tuache tusiwape watugonge fine tu za kutosha huu unafki ifikie kipind uishe ushaona polisi anakushawish umpe pesa Bali ss wenyewe na vielf tano vyetu ndio tunawashawish.

Hebu achen hzo mambo mnadhan hyo elfu thelathin Ni ndogo aiseee Bora umpoze ya maji mzee baba unasonga mbele kuliko 30 kwa wiki 37500 ikipita

kilicho akilini kitumie

Polisi msiwafanye wengine wajinga. Kwani hizi faini za kubambikiza makosa sita sita - si kuwa mna njaa kali tu kama ya mzee fisi na mnachotaka kimsingi ni rushwa tu?

Kuwa wa kulaumiwa ni wahanga wenu? You must be kidding!

Mbona Kangi mlimchukia ya kuwa kawaletea njaa?
 
Si leo tu. Rejea nyuzi mbalimbali. Ilifahamika toka day 1 polisi walishangilia hali wahanga wao wakigumia.
Hakuna walio mtegemea Kama lugola Mana alikuwa Ni polis mwenzao na mkewe alikuwa Ni polis pia kwahyo lugola alikuwa anajua shida zote za polisi

Kuanzia makaz,mishahara,vitendea Kaz na majengo ya ofsi

Na kilichotokea Ni tofauti alivyokuwa anatetea kabla ya kuwa waziri.na kwa taarifa yako lugola alilewa madaraka haraka Sana na ndio maana Kuna mengne alikuwa akiyafanya hayako katika sheria na kanuni za miongozo ya majeshi aliokuwa akiyaongoza katika wizara husika.

Hayo makosa yote yapo katika notification paper na mpaka baiskeli iko na makosa yake sis madereva wa kitambo tunajua ubovu wa gari na tair chakavu sijui reflector kila kosa Lina kifungu chake kwa hyo lugola alikuwa ana lazima liwe kosa moja kitu ambacho kisinge wezekana na huo ukweli anaujua.

Yeye lugola alipaswa kukaa na viongoz wa polis,wanasheria,na wadau wa usalama barabaran kuangalia wapi pakuongeza na kupunguza bila kuathiri sheria mama Kisha wapeleke muswada bungeni Kisha zijadiliwe na rais apitishe ili ziwe rasm.

Kwa mantik hyo lugola alikuwa too much talkative na mbwa anae bwekabweka tu kwa sababu anafanya kitu kisicho kuwa na maana na Cha muda tu.

kilicho akilini kitumie
 
Polisi msiwafanye wengine wajinga. Kwani hizi faini za kubambikiza makosa sita sita - si kuwa mna njaa kali ya mzee fisi na mnachotaka kimsingi ni rushwa tu?

Kuwa wa kulaumiwa ni wahanga wenu?

Mbona Kangi mlimchukia kuwa kawaletea njaa?
Wew mtoto hujui uchungu wa pesa Ni Bora nimpe polis elfu tano kuliko 30 kwa sis madereva wa root za rwanda ,kongo Zambia ndio tunajua

kilicho akilini kitumie
 
Hakuna walio mtegemea Kama lugola Mana alikuwa Ni polis mwenzao na mkewe alikuwa Ni polis pia kwahyo lugola alikuwa anajua shida zote za polisi

Kuanzia makaz,mishahara,vitendea Kaz na majengo ya ofsi

Na kilichotokea Ni tofauti alivyokuwa anatetea kabla ya kuwa waziri.na kwa taarifa yako lugola alilewa madaraka haraka Sana na ndio maana Kuna mengne alikuwa akiyafanya hayako katika sheria na kanuni za miongozo ya majeshi aliokuwa akiyaongoza katika wizara husika.

Hayo makosa yote yapo katika notification paper na mpaka baiskeli iko na makosa yake sis madereva wa kitambo tunajua ubovu wa gari na tair chakavu sijui reflector kila kosa Lina kifungu chake kwa hyo lugola alikuwa ana lazima liwe kosa moja kitu ambacho kisinge wezekana na huo ukweli anaujua.

Yeye lugola alipaswa kukaa na viongoz wa polis,wanasheria,na wadau wa usalama barabaran kuangalia wapi pakuongeza na kupunguza bila kuathiri sheria mama Kisha wapeleke muswada bungeni Kisha zijadiliwe na rais apitishe ili ziwe rasm.

Kwa mantik hyo lugola alikuwa too much talkative na mbwa anae bwekabweka tu kwa sababu anafanya kitu kisicho kuwa na maana na Cha muda tu.

kilicho akilini kitumie

Lugora alikuwa polisi kama alivyokuwa mkewe. Aliwajua polisi vilivyo. Aliwezesha dhamana kuwa 24x7 kinyume na matakwa ya polisi. Alileta nidhamu katika utendaji wa polisi dhidi raia wema.

Testimony ya haya Kangi alipotumbuliwa:

Polisi walishangilia na kufanya tafrija wahanga wao wataendelea kumkumbuka.

Kwetu sisi ambao polisi mnatukera mno, Kangi Lugora ni shujaa be it ni waziri na hata kama ni jamaa tu - yaani hata kama ni 'lumpenproletariat'.
 
Suala inatakiwa madereva wasitembee na cash, kwenye milango iandikwe hakuna pesa iliyobebwa kwasababu yote hayo wanafanya ili kujitengenezea mianya ya kupata rushwa au ni mpango wa serikali kukusanya kodi au pesa ya uchaguzi..

Haiwezekani serikali kwa rasilimali zote walizo nazo washindwe kuondoa rushwa.

NB. Kuto kubeba cash ikiwa ni sheria, matumizi ya technology yasiachwe nyuma, vile vile wananchi tusiogope kupelekwa kwenye mamlaka husika kuliko hawa wahuni wanaobambikia kesi ovyo...

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu jaribu tu kuwaza kwa sauti kutoa Elfu 5 ama kushinda mahakamani miezi 6 ili upate haki yako tena bila fidia ya kupoteza muda wako!ya kaisari mwachie kaisari
N.B,hapa duniani hakujawahi kuwa na haki

Sent using IPhone X
 
Je angeachwa aendelee na uaziri kisa kawadhibiti traffic polisi?

Ukiwa mzuri kwa upande mmoja na upande mwingine ukawa mbovu wewe unahesabiwa kuwa una dhambi. Hivyo kangi kuwadhibiti traffic kama uanvyodai wewe huku akihujumu uchumi wa nchi bado ni mkosaji kama wakosani wengine.

Lakini pia usihukimu kuwa askari polisi pekee ndiyo wamefurahia kutumbuliwa kwa Lugola. Nina imani ya dhati ww kwa njia moja au nyingine ulikuwa na manufaa na uaziri wa Lugola

Mimi siyo polisi lakini binafsi nilishukuru kufukuzwa uaziri mh huyo. Kilichokuwa kinanichukiza kwa mh huyo ni tabia ya kuwadharau aliyokuwa akiwaongoza na kuwaona kama vinyago fulani na akasahau hao watu wamesomea kazi yao lakini yeye hakuwa amesomea uaziri. Lakini pia akasahau mkuu wa polisi, magereza, fire na uhamiaji anaweza kuwa waziri lakini yeye hawezi kuajiliwa katika nyadhifa zao.

Kwa ujumla Lugola alikuwa na dharau ya kupindukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huna lolote,wewe ni Askari usizuge.Kudharauliwa kwao wewe ilikuathiri Nini kimaisha?.Hapa tunazungumzia kero ambazo zimerudi kwetu sisi wananchi baada ya Lugola kuondolewa.Kama aliwadharau ni juu yenu.Kwanza mi naona alikuwa sawasawa alivyokuwa akiwapelekesha.Nyie Askari Polisi ni kizazi Cha Nyoka.Mnakera mno

Unapata kero gani wakati humiliki hata baiskeli!!

Wewe mpigie kampeni lakini ujue hata ubunge hapati. Kuwaheshimu wa chini yako ni jambo la muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naitwa mpinga mafisadi
Mkuu kwani wewe nani jitambulishe tukufahamu ili siku nyingine tukunukuu kwa maana waswahili wanasema 'kosa moja halifukuzishi mke'. Mwisho wa kunukuu.

Waswahili - kiwakilishi cha waungwana.

Bila shaka na 'kosa moja' unaloliongelea ni zengwe la kutengenezewa.

Kangi kaenda tuliokoshwa na utendaji wake tutamkumbuka. Hakika lilikuwa dume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madereva hasa hasa wa masafa marefu amabao ndo waanga hasaa wa malori na mabasi ungananeni mkapinge huo uonevu kwa pamoja au kupitia vyama vyenu! Mmoja mmoja akilalamika haitasaidia!

Ni suala la muda tu. Waungwana wanasema - just a matter of time.

Acha wajidanganye kuwa itakuwa hivi hadi Yesu Kristo arudi.
 
Hili nililisema mapema sana! Hata Mh rais alisema vizara inayomyima usingizi Ni hii ya MAMBO YA NDANI
MAONI.
Nashauri kitengo hiki cha usarama Barabarani kiondolewe police kianzishwe kitengo special km walivyo wa mizani
Kiukweli hili la rushwa linahitaji mbinu mbadara zaidi ya hapo hata tukilalamika tunapoteza mda
Mizani ya barabarani iko chini ya Tanroad, Tanroad ndo msimamizi wa barabara,
Suala la police ili lidhibitiwe lazima kiwepo kikosi cha kuwachunguza hao askari wa Usalama barabarani miaka Fulani Kenya walianzia hiyo ikaleta kelele sana namna askari walivyokuwa wanashikwa na rushwa barabarani
 
Hii post yako akiiona dereva wa lori anayetegemea mizigo ya mishemishe njiani kujiongezea kipato atakuona mchawi tuu mana watabanwa kila kona.
Mfaidika wa hizo rushwa ndogo ndogo nazan ni dereva mwenyewe.

Back
Top Bottom