Kero ya misafara ya viongozi wakuu wa serikali: Mwananchi atoa neno zito "Ole wao dada yangu akipoteza maisha!"

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Kichwa cha uzi ni nukuu ya kauli ya jamaa yangu mmoja ambaye sasa hivi yupo likizo huko kijijini kwao mkoani Songwe.

Jamaa yangu huyu ananitaarifu kuwa asubuhi ya leo alikuwa amejihimu mapema kumuwaisha hospitali ya mkoa dada yake ambaye usiku mzima wa kuamkia leo amekuwa mahututi.

Jamaa anasema walipokaribia kufika mahali pa kuingia kwenye barabara kuu ya kutokea Tunduma kuelekea Mbeya, wakakuta msafara wa magari kwenye barabara yao umezuiwa na askari wa usalama barabarani (almaarufu "matrafiki") kuingia barabara kuu hiyo. Walipouliza why wakaambiwa eti misafara yote ya magari ya wananchi kuingia barabara kuu isubiri msafara wa rais upite kwanza.

Basi wakasubiri hapo weee hadi baada ya masaa 2 ndipo magari mengine ya wananchi yakaruhusiwa.

Jamaa yangu huyu ameudhiwa sana na kitendo hiki kwani anasema wakati wakisubiri msafara wa rais upite, hali ya mgonjwa wao iliendelea kuteteleka zaidi na hadi sasa familia ina wasiwasi sana juu ya mustakabali wa afya ya ndugu yao huyo.

"Ninaapa, dada yangu akipoteza maisha, nitakula sahani moja na wote watakaokuwa wamesababisha kifo chake!"... jamaa ametamka kwa uchungu sana, bila kufafanua zaidi.

Ukimsikiliza huyu jamaa anavyosikitika kwa uchungu kwa kweli badala ya kumhurumia, na wewe lazima utapata hasira kama mimi. Hasira ndiyo iliyonisukuma kupandisha huu uzi.

Maoni yangu:

Hii misafara ya viongozi wakuu wa serekali imekuwa ikisababisha kero kubwa sana kwa wananchi. Kwa nini kwa mfano tusijifunze kutoka nchi jirani kama Uganda (ambako arguably amani na usalama vipo chini kuliko Tanzania) msafara wa rais huwa unaachiwa lane moja ya kupita lakini misafara ya wananchi haizuiwi?

Mimi mwenyewe mwaka jana nilikuwa mhanga mahali fulani huko kanda ya ziwa tulistopishwa barabarani kupisha msafara wa rais, ikapelekea mimi kukosa flight ya kurudi Dar siku hiyo, nikalazimika kuondoka siku 2 baadae.

Hakuna wakati niliochukia misafara ya rais kama ilivyo chini ya awamu hii.

Tundu Lissu akiingia Magogoni October tafadhali arekebishe hii kitu fasta.
Najua chini ya awamu hii si rahisi kurekebisha kutokana na wakalia kiti kupenda kutukuzwa kama miungu.

ANNOYED.
 
Back
Top Bottom