Kero tunazopata kwenye Nyumba za kupanga

Juzi kuna gari lilikua limebeba kuku broiler limepata ajali. Mimi nikaokota kuku saba kufika nyumbani nikamgawia mama mwenye nyumba wawili. mpangaji mwenzangu wawili na mimi watatu. baba mwenye nyumba aliposikia nimempa mkewe kuku wawili tena wazima. Aliwaka kama kifuu lakini kuku alikula. huyu mpangaji mwenzangu alihisi mkewe ni mchepuko wangu. alihama kesho yake na vijembe viingi tu. Baba mwenye nyumba haniamini tena.

Wewe ni jirani yangu. Habari ya kumgawia kuku mke wa mwenye nyumba tumeisikia. Ila kabla ya habari hiyo kulikua na habari nyingine tata kuhusu wewe kumgawia samaki huyo mama kila mumewe anaposafiri.pia kuna tetesi ya wewe kubaka watoto wadogo. Kwa kifupi hapa mtaani wote hatukutaki. Kwa faida yako naomba uhame leo leo kwani kesho vijana wa hapa wamepanga kukufanyia kitu mbaya sana
 
Kubaka mtoto mdogo ndio dhambi ya mwisho duniani. MUNGU aniepushe nayo. Hii ya kumkirimu mama mwenye nyumba sio kweli kwani ni vigumu mtu ukaange samaki sufuria zima halafu mke wa mkuu analumangia na kisamvu hakina hata wese.
 
Heri la kwako.kuna nyumba ni majini matupu.nilipanga nyumba Mbezi siku ya kwanza kulala nilipata shida sana nikasali usiku kucha.asubuhi mwenye nyumba kamfuata wife kamwambia ni marufuku kusali kuipmbea nyumba yangu kama mnataka kusali kapangeni kanisani. Kumbe mzee anafuga majini
 
Nimepanga chumba,Masharti niliyoyakuta nimeshachoka kuishi katika hii nyumba.

Kinachonichosha ni hiki wanakata umeme asubuhi saa mbili kuwasha saa kumi na mbili jioni.

Nilipokuwa nalipa kodi sikuambiwa mpaka mimi nilipoanza kuulizia kwa sababu kutokana na kazi yangu nachelewa kulala na kuamka pia.

Nyumba nayoish walitaka kuleta hilo suala nikakataaa,ikawa nikitoka wanazima,ila nikirud tu wanauwasha,maana nilishawaambia umeme kwangu ndio kila kitu ndo maana naish nyumba ya umeme,mdau hama hapo maana hawakukwambia,pia nimejifunza unapohamia kwenye nyumba,kwanza kagua choo,na usalama kwa ujumla,hoji kama kuna maji,na kama hayapo wanachota umbali gani???,pia bei ya mchango wa umeme na matumizi kwa ujumla,,,,,,,muhimu sana mdau
 
Binamu yangu alipanga Mwenge Survey kwa mchaga mmoja maarufu kama Kisima. Mkorofi fulani hawezi kuishi na mwanamke. Basi binamu yangu akaja nyumbani nikampa jogoo na mtetea ili apate mayai ya watoto. Jogoo alpokua akaanza kuwika basi Kisima akamwambia aondoe jogoo linamsumbua akipata chakula cha alfajiri. Visa kibao kumbe alikuwa anamtaka kwa kuwa binamu mume alikuwa masomoni . Nilifika siku hiyo na kumpakia binamu na kumwachia kodi ya miezi 3. Ilikuwa ndiyo mwanzo wa kupata kiwanja na kujenga. Wenye nyumba acheni roho mbaya.
 
Wewe ni jirani yangu. Habari ya kumgawia kuku mke wa mwenye nyumba tumeisikia. Ila kabla ya habari hiyo kulikua na habari nyingine tata kuhusu wewe kumgawia samaki huyo mama kila mumewe anaposafiri.pia kuna tetesi ya wewe kubaka watoto wadogo. Kwa kifupi hapa mtaani wote hatukutaki. Kwa faida yako naomba uhame leo leo kwani kesho vijana wa hapa wamepanga kukufanyia kitu mbaya sana

Mkuu umetisha. Mleta mada njoo huku kuna tuhuma. Panya Road wataku do.
 
Kubaka mtoto mdogo ndio dhambi ya mwisho duniani. MUNGU aniepushe nayo. Hii ya kumkirimu mama mwenye nyumba sio kweli kwani ni vigumu mtu ukaange samaki sufuria zima halafu mke wa mkuu analumangia na kisamvu hakina hata wese.

Ahaaa kwa hiyo we unaona raha kumsaidia baba mwenye nyumba? Unadhani ye aneshindwa kumnunulia?
 
Nyumba za kupanga noma hasa kama mwenye nyumba anaishi hapo hapo;

mie nilipokuja bongo nilipanga hapo sinza, mama mwenye nyumba alipoanza
kunizingua nilijenga chumba kimoja ndani ya mwezi mmoja nikahama, na kodi nikamwachia;
na kwa kumkomoa nikabeba na madirisha yake yalikuwa mle ndani;

Natamani asione hapa pengine atanikumbuka.
 
Ndiyo changamoto hiyo mkuu,jipange ujenge yako uondoke utumwani...

Kwani ukipata nyumba ya kupanga unaingia tu bila kuuliza terms?
Mi siku moja nilipata nyumba nzuri tu, nikauliza masharti kama yapo nikaambiwa marafiki hawaruhusiwi kabisa, si wakiume wala wakike., watu pekee wanaoweza kuja kwangu ni wazazi wangu tuu. Duh kuona vile kwa macho makavu nikamwambia hata wafungwa wanatembelewa, unles kwako ni Guantanamo, nikachapa lapa.
Nashukuru mdada ambaye nimepanga kwake na tunakaa naye kwenye compound moja ni Poa sana.
 
Juzi kuna gari lilikua limebeba kuku broiler limepata ajali. Mimi nikaokota kuku saba kufika nyumbani nikamgawia mama mwenye nyumba wawili. mpangaji mwenzangu wawili na mimi watatu. baba mwenye nyumba aliposikia nimempa mkewe kuku wawili tena wazima. Aliwaka kama kifuu lakini kuku alikula. huyu mpangaji mwenzangu alihisi mkewe ni mchepuko wangu. alihama kesho yake na vijembe viingi tu. Baba mwenye nyumba haniamini tena.

wewe ni mwizi! Haraka kamtafute aliyepata ajali, mrejeshee kuku wake! Ninyi ndio wale mnaowaaibia majeruhi/wahanga wa ajali. Kwepa laana maana umethubutu kukiri mbele za kadamnasi, jitakatifishe sasa kwa kuwarudisha!
 
duhh hapa kama kuna ukweli flani ivi
 
Back
Top Bottom