Nadhani ni bora wangeonesha kwa uhalisia zaidi ili watu wasihangaike sanaaa kuzitafuta.
Kuna namna naamini kuwa kwa wao kufanya hivyo, tutazipata pengine tena zikiwa zimechakachuliwa kwa kukandamiza ccm hiyo hiyo, nina maanisha kuwa, maneno yatakolezwa kutokana na mihemko ya kiitikadi ya kivyama kutokana na mhusika ameelemea upande gani.
Namshauri huyu mpare mtani wangu, afanye kazi kulingana na taaluma yake na sio kulingana na waliompa madaraka.
Madaraka yameshamlewesha kiasi hakumbuki taaluma yake.
Chukua ushauri wa bure kwa aliyekuajiri baada ya kumfukuza Mzee Tido Mhando. "Akili za kuambiwa changanya na zako"
Mhando alinisababisha kuipenda TVT kwa muda mfupi baada ya yeye kuingia hadi akaibadilisha kuwa TBC ya sasa.
Alichokifanya ni kuruhusu uhuru wa chombo cha uma, kurusha habari za kisiasa majimboni kwa kuwaalika wagombea na kuwahoji jambo lililtusaidia sana wanachi kuwafahamu vizuri viongozi wetu kwa uelewa wao.
Ikumbukwe kati ya waliohojiwa kipindi kile hakuna hata mmoja wa ccm aliyechaguliwa. Makamba by then ndiye alikuwa Katibu Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Dar. akakataza mgombea yeyote wa chama chao kuhojiwa.
kilichofuata ni nini, Tido kufukuzwa kazi.
Huu ni uonevu usiovumilika, kwa kiongozi mkubwa kama huyu ambaye anaongoza Taifa la watu wenye itikadi ya vyama vingi.