Kero: Mafundi kuweni wastaarabu

Kero: Mafundi kuweni wastaarabu

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
15,126
Reaction score
35,515
Habari,

Mafundi ni moja ya watu muhimu katika maisha yetu ya kila siku ila wengi wenu mmekuwa na mambo sio ya kistaarabu sana inabidi mbadilike;

1.Unapeleka gari litengenezwe,Fundi anaingia chini kumwaga oil au kucheki tatizo akitoka huko nguo ina michanga na oil anaingia hivyohivyo ndani ya gari anakaa kwenye siti nyeupe anaanza kuwashawasha kwanini basi usiweke nguo kuzuia uchafu kwenye siti?

2.Unamwachia fundi gari atengeneze,anakwambia njoo badae,akimaliza kutengeneza anaenda nayo misele yake kisa ipo majaribio na ina mafuta.

3.Unampelekea Fundi Tv flat screen anaicheki anakwambia njoo siku fulani anaitupia kwenye makorokocho yake inakwaruzika kioo na vumbi hata ukienda kuichukua imetengemaa ila ina hali mbaya.

4.Unapeleka simu itengenezwe,anaweka kwenye meza ina michanga na vumbi,kweli inapona ila imekwaruzwa hata kama mpya inaonekana imechoka,kwanini usiweke kitambaa safi au cover laini?

5.Fundi unafungua laptop unatawanya nati unaweka sehemu mbalimbali,ukija kurudishia zinabaki nati 3 hazijulikani za wapi,kirahisi tu unasema hizi hazina shida zilikuwa na kushikilia tu,ina maana walioweka hawana akili?

6.Unapeleka redio itengenezwe,unafungua mifuniko unakuta labda kuna buibui mle ndani wamejenga au nyigu wameweka wamejenga,ukimaliza kurekebisha unarudishia hivyo hivyo,kwani ukifuta mle ndani ili kuzuia wasijenge zaidi utapungukiwa nini?

Mafundi jitahidini kujali vitu mnavyoletewa kwenu,tuwaamini kwa kazi yenu ila boresheni mazingira,mtu akiacha kifaa kina hali nzuri akija kuchukua akikute kipo hivyohivyo.

Mwisho muwe mnatoa ahadi za kweli,mambo ya njoo kesho yanachosha.

Mengine mtaongeza.

Ahsante.
 
Fundi ashakula siku yangu
Mwingine Tv niliipokelea kiruo cha polisi,hawa watu ukipeleka kifaa usiwape nafasi!!
Sijui wanashindwa nini kuwa wakweli?
 
gari lazima itestiwe weweee.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]namafuta yanapigwa nyoka
[emoji3][emoji3][emoji3],huo sio ustaarabu fundi anaona ndio muda wa kupeleka mboga nyumbani,mara kwenda site nk
 
[emoji3][emoji3][emoji3],huo sio ustaarabu fundi anaona ndio muda wa kupeleka mboga nyumbani,mara kwenda site nk
yaa halafu baadae bos anapigiwa simu utaskia hebu tuma elfu 50 hapo tununue mafuta tutesti gari Mana ishakua sawa.
 
Habari,

Mafundi ni moja ya watu muhimu katika maisha yetu ya kila siku ila wengi wenu mmekuwa na mambo sio ya kistaarabu sana inabidi mbadilike...
Hiyo namba moja nilitaka kumnasa dogo mmoja vibao, ila alikua humble nikatulia tuu.

Aliitwa kuja kutoa bolt imekatikia sehemu ya kufungia compressor.

Akagalagala huko uvunguni weee.

Baada ya masaa matatu akamaliza, muda huo me nimeenda kula. Kwahiyo anavosubiri nije nimlipe akaingia kukaa ndani na lile vumbi na nguo zake za kazi kama tunavozijua, zina maoil machafu.

Aisee nilitamani nianze kuwaka kutokea ng'ambo ya barabara

Yani kaja kufanya kazi ya elf 15, kwa masaa matatu tu, kaacha uchafu ambao nimeenda kuosha kwa elf 10.
 
Back
Top Bottom