Mimi CRDB tawi la Mlimani City:
Nawambia naomba kufungua akaunti, nikakutana na kadada kazushi mezani kakasema "Nione ID zako", nikasema kwani benki inahitaji ID gani? Akasema "wewe una nini? " Nikasema nataka ni assess nitumie zipi kwa mujibu wa policy za benki, kadada kakasema Annh, akaanza kuzitaja kwa kubahatisha bahatisha...Nikamwambia naomba sehemu iliyoandikwa hiyo policy, Dada akashtuka ile mbaya. "Unasemaje?" Yani kashangaa kinoma. Nikamwambia basi nipe fomu za kujaza mi nitarudi. Dada akasema katafute kwanza wadhamini wawili. Nikamwambia oooh, hell no, niwabebe niwalete hapa ndio unipe fomu? Kidada kikasema excuse me? Nikamwambia nipe fomu nikapeleke kwa wadhamini, unataka niwapandishe bajaji niwalete hapa? Kidada kikanuna kama kimekula matunda nyoka. Akaniuliza we umetoka Marekani? Nikamwambia dunia ina nchi mbili tu, Tanzania na Marekani? Kidada kikaanza kulia haki ya nani... Nikaanza mbele...