Waziri wa Fedha-Kenya: Serikali imeelemewa na Madeni, Mzunguko wa Fedha umekuwa mgumu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Waziri wa Fedha na Hazina wa Kenya, Njuguna Ndung’u ameiambia Kamati ya Fedha na Mipango ya Taifa kuwa Madeni ya Mikopo ya muda mfupi yanayoendelea kuiva, kushuka kwa thamani ya Shilingi na viwango vya juu vya riba vimesababisha nchi hiyo kuwa katika hali ngumu ya Kifedha.

Prof. Ndung’u amesema kiwango cha Ubadilishaji Thamani ya Fedha na kiwango cha riba vimeongeza Deni la Taifa kwa kati ya 4.3% hadi 5.2% ambayo ni sawa na Tsh. 2,404,387,971,450 ikiwa ni kwa robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/24.

Serikali ya Rais Ruto imekuwa ikiitupia lawama za mzigo wa Madeni Serikali ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na kueleza ilikuwa na kasi kubwa ya uchukuaji Mikopo yenye masharti ya muda mfupi bila kuwa na usimamizi mzuri wa miradi.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) hadi kufikia Juni 2023, Deni la Taifa lilikuwa Tsh. Trilioni 174.15 huku Benki ya Dunia pekee ikiidai Kenya zaidi ya Tsh. Trilioni 24.96 huku China ikidai zaidi ya Tsh. Trilioni 20.10.
 
Back
Top Bottom