luangalila
JF-Expert Member
- Jan 12, 2014
- 6,325
- 6,871
Hellow Guys, Habari yenu waungwana toka ktk jumuia yetu ya Afrika Mashariki, binafsi nawasilisha UZI leo siku ya Jpili, nimebahatika kutazama television kadhaa za Kenya nimeona hawa jamaa wanafanya investment kubwa sana ktk media houses zao tofauti kabisa na Tanzania, hata ukitazama vipindi vya Tv vya Kenya unaona umakini wa hali ya JUU mnoo kuanzia uandaaji wa habari mpaka makala wanazo tengeneza tofauti na Tanzania ni muda mrefu sanaa ktk Teleision zetu nyingi waandishi wetu wa habari wanashindwa kuandaa makala au habari za utafiti zilizo ktk kiwango kizuri na zenye content. Nikijaribu ku tolea mfano ktk vituo kadhaa vya kenya citizen tv leo Jpili wanaleta makala ya vijana wanaokwenda kujiunga na al shabaab hii kitu POA sanaa na sio mara yao ya kwanza kuleta makala kama izo hapa TZ makala za utafiti kama izi niliwahi kushuhudia kipindi kile cha sakata la watoto yatima pale MAKETE na HIV kule mkoa mpya wa Njombe alikuwepo dada mmoja toka channel Ten alikuwa anaitwa Bahati mndetele Nyembe alileta ile makala ilimpa sifa sanaa kuanzia hapo makala kama zile zimeadimika TZ achana na zile habari za uchunguzi za akina DC JM