JAMII-ASM
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,305
- 524
Haitakuwa mara ya kwanza kwa Kenya kuchoma moto pembe za ndovu. Hii ni katika sifa au ''legacy'' za kupigiwa mfano alizoacha Mzee Arap Moi,kwani yeye ndio muasisi wa uchomaji pembe za ndovu Afrika.
Rais Kenyatta kaamua kuivunja rekodi ya Mzee Moi. Kenyatta kaamua kuchoma pembe za ndovu zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 120 ,sawa na shilingi za kitanzania bilioni mia mbili. Pembe hizi zina uzito wa tani 120 na inasadikiwa zilitokana na mauaji ya tembo elfu nne.(4,000) .Huu ni mzigo mkubwa kuliko yote duniani kupigwa moto.
Tukio hili ,litakalo fanyika mwezi Aprili ,litahudhuriwa na watu maarufu duniani , akiwemo Leonardo Di Caprio (wa muvi ya Titanic), Nicole Kidman,mchezaji maarufu wa basketball mchina Yao Ming.
Matajiri wakubwa duniani Paul Allen (muasisi wa Microsoft),mtoto wa Warren Buffet aitwae Howard Buffet (huyu aliwahi kuwafadhili helikopta TANAPA lakini bahati mbaya helikopta ilipata ajali na kuua rubani),George Soros,mwanamuziki shoga Elton John..na tajiri Michael Bloomberg.
Inaaminika Tanzania tuna mzigo mkubwa sana..kuliko huu.Lakini tumegoma katakata kuuteketeza. Huko unakotunzwa una usalama kiasi gani ... labda wadau mnipashe.
Leonardo DiCaprio and Nicole Kidman to Attend Torching of Largest Ever Ivory Stockpile to Help Put an End to Poaching
Video ya Kenyata akichoma tani 15