Kenya yachoma hifadhi yake ya Pembe za Ndovu na Faru zenye thamani zaidi ya Tshs Billn 450

BUSAMUDA

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
612
358
Rais wa Kenya tarehe 30/04/2016 ameidhinisha uchomaji wa Pembe za Ndovu Zenye thamani ya zaidi ya Tshs bill 300 na Pembe za Faru Zenye zaidi ya Tshs Bill 150.

Sherehe hizi zilihudhuriwa na rais wa Uganda Yoel Museveni na viongozi mbalimbali Africa.

Zinakadiliwa kutoka kwa zaidi ya tembo 8,000

Pembe za Faru zimetoka kwa zaidi ya Faru 343

Akiongea na CNN mhifadhi Richard Leakey anasema katika Dakika 15 duniani tembo 1 huuawa na majangiri.

John Scanlon anasema huu ni ujumbe Kenya inatuma duniani kuwa Kenya itapambana na biashara hii haramu ya wanyama pori."

Now it's Tanzania turn to burn its ivory stock.

Historic ivory burn covers the sky in smoke and ash
Millions of dollars of tusks, horn burn in Kenya - CNN.com
 
Siwezi kuzichoma aisee, why should I lose all those billions and end up looking for loans and grants of the same amount somewhere else... I'm sorry I can't
 
Usiochoma ina maana utauza au kubadilisha matumizi na matokeo yake wewe mwenyeww utaendelea kuchochea na kuhamasisha soko haramu la pembe za ndovu na kusifu kazi ya majangili,,kwahiyo ujangili utaendelea na tembo kuzid kuuawa
Big up to kenya aiseee,piga vita kutomomeza ujangiri
Kwa mujibu wa salim kikeke BBC swahil news, 65% ya tembo wameangamizwa ukanda huu,ujangil ukiendelea itafika kipindi vizazi vijavyo wataona kwenye picha tu kulikuwa na mnyama anaitwa tembo
 
Kwa Tanzania hii ni ndoto labda kizazi cha Mwaka 3000 kinaweza fikiria kuchoma fedha hiyo
 
Tatizo lingine la watu weusi kutaka kuwafurahisha wazungu,, una pembe za ndovu zenye thamani ya tsh billioni 450, taifa lako masikini kutwa kucha bajeti haitoshi na hizi pembe tayari ndovu wakutosha wameshakufa na hazina effect yoyote kwa binadamu hao wanaoziitaji yaani kwa kifupi ukiziuza kwa wachina haziwezi kuja kudhuru watu wako... Uza hizo pembe hizo hela fanyia biashara na faida itumie kuimarisha kulinda mbuga tembo wengine wasife...
 
Siyo watu weusi ila ni watawala weusi.
Nina amini kuna wengi wenye fikra chanya ila hawako katika ngazi za maamuzi
 
Tatizo lingine la watu weusi kutaka kuwafurahisha wazungu,, una pembe za ndovu zenye thamani ya tsh billioni 450, taifa lako masikini kutwa kucha bajeti haitoshi na hizi pembe tayari ndovu wakutosha wameshakufa na hazina effect yoyote kwa binadamu hao wanaoziitaji yaani kwa kifupi ukiziuza kwa wachina haziwezi kuja kudhuru watu wako... Uza hizo pembe hizo hela fanyia biashara na faida itumie kuimarisha kulinda mbuga tembo wengine wasife...
WARNING: usitumie ubongo wako kama pambo la ndani!
 
Wengi wamelaani kuwa kuzichoma sio suluhisho la kuhifadhi. Ni vyema zingeuzwa na mapato yake yatumike kuboresha uhifadhi wa wanyama hao.
 
Back
Top Bottom