Kenya Wako Kumwanya - Mashujaa Wetu wa Demokrasia?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Kuna majibu mengi mazuri yametolewa leo kwa maswali mengi ambayo yanaitatiza siasa za Afrika - upinzani na watawala. Lakini pia kuna maswali mengine yameachwa wazi ambayo majibu yake yataamua kama Tanzania inaweza "kufuata nyayo" za kidemokrasia ambazo zimeoneshwa na Kenya leo.. na zinatarajiwa kuoneshwa tena siku sitini baadaye:

Kenyata mwenyewe ametoa kauli tata on public

Mara oh sasa amekalia kiti,Mara ooh watu sita majaji hawawezi

kuzuia peoples will....anaruka ruka tu
 
Wewe jamaa walifika bei ukajiunga na kambi ya upotoshaji.
10-wajumbe-ndani-ya-ukumbi.jpg
 
Kuna majibu mengi mazuri yametolewa leo kwa maswali mengi ambayo yanaitatiza siasa za Afrika - upinzani na watawala. Lakini pia kuna maswali mengine yameachwa wazi ambayo majibu yake yataamua kama Tanzania inaweza "kufuata nyayo" za kidemokrasia ambazo zimeoneshwa na Kenya leo.. na zinatarajiwa kuoneshwa tena siku sitini baadaye:

Siyo kwa watawala hawa wasioambilika wa kizazi chetu! Pamoja na mambo mengi mengine ya kukumbuka kwa Mzee Kibaki ni kuruhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba ya nchi kwenye awamu yake ambayo matokeo yake ndiyo yanayoonekana sasa!
Hapa kwetu JK ana shauri la kujibu ahera huko baada ya wakati wake kuisha kwa kushindwa/kuwa na kigugumizi wakati wa mchakato wa mabadiliko ya katika ambayo kwayo sauti ya mwananchi ilikuwa inasikika sana! Kama asingaliionea haya leo hii utawala wa sheria ungeheshimika na kufuatwa!
 
Kenyatta Katoa Hotuba Iliyojaa Busara Kubwa, Ingekua Ni Huku Tanzania Ungesikia "Hao Majaji Tutarara Nao Mbere Kwa Mbere" !!

Umekisika alichowaambia vijana kwenye kampeni yake muda mfupi baada ya hukumu kutolewa? Kamuita jaji 'Chokoraa' na anasema sasa yeye ni rais!
 
Kenyata mwenyewe ametoa kauli tata on public

Mara oh sasa amekalia kiti,Mara ooh watu sita majaji hawawezi

kuzuia peoples will....anaruka ruka tu
Pamoja na hivyo ujue anaungwa mkono na raia wengi sana!
Anaamini pamoja na waliompa kura kuwa majaji wamewadisapoint angalau kwa muda.
Amekalia ten kiti kwa miezi miwili ijayo msikizeni yeye.
 
Kenyatta zile speeches anatoa kama Obama. Kwa ku inspire watu kwa speech tu, kakaa vizuri.

Mimi najiuliza,uchaguzi ukirudiwa halafu Raila akashindwa tena, itakuwaje?

Wana piga penalty /matuta . vinginevo ni kurusha shilingi
 
Kuna majibu mengi mazuri yametolewa leo kwa maswali mengi ambayo yanaitatiza siasa za Afrika - upinzani na watawala. Lakini pia kuna maswali mengine yameachwa wazi ambayo majibu yake yataamua kama Tanzania inaweza "kufuata nyayo" za kidemokrasia ambazo zimeoneshwa na Kenya leo.. na zinatarajiwa kuoneshwa tena siku sitini baadaye:

Nyuzi zako zilikuwa na positive response kutoka kwa wanajukwaa, toka ulipokubali kuwa mpotoshaji post zako zimechacha.
 
Shujaa wetu wa demokrasia ni mtanzania, John Pombe Magufuli. Sio dikteta uchwara wa Kenya
 
Wengi wanadhani matokeo ya hukumu ndilo jambo muhimu, hapana!

Kwa siasa za Afrika mkondo wa maelewano umetengenezwa ima kulazimisha hali fulani kama ilivyo hapa kwetu ambapo matokeo hayahojiwi, au kuingia katika machafuko kwavile mmoja ana nguvu kama ilivyo nchi nyingine na jirani zetu

Kilichotokea Kenya, kampeni zilifanyika kwa njia za kiustaarabu 'fair' kwa std zetu
Matokeo yakatangazwa hadharani na tume ya uchaguzi

Aliyeshindwa akampongeza aliyeshinda
Uhuru wa kupinga kilichoktokea ukatolewa kwa anayetaka kuandamana au mikutano

Aliyeshindwa akafuata mkondo wa sheria kutafuta anachodai hakikuwa sawa

Sheria ikaamua kuwa kuna dosari na uchaguzi urudiwe

Pande zikakubali matokeo ya mkondo wa sheria hata kama hawakubali matokeo ya sheria

Kumbe basi Waafrika tunaweza kufanya mambo bila kuwa katika TV za kuonyesha michirizi ya damu

Hiki ndicho kikubwa na muhimu kuliko hukumu yenyewe
 
Demokrasia ya kweli ni pale unapoheshimu maamuzi ya wengi...serikali ya kenya (inayoongozwa na Uhuru) pamoja tume ya uchaguzi walipindisha matokeo...
Kilichotokea kenya ni uthibitisho kuwa checks and balances kati ya judiciary na executive ziko effective...ila demokrasia bado

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenyatta zile speeches anatoa kama Obama. Kwa ku inspire watu kwa speech tu, kakaa vizuri.

Mimi najiuliza,uchaguzi ukirudiwa halafu Raila akashindwa tena, itakuwaje?

Hilo litakuwa suala jingine kabisa,
Muhimu ni kwamba Mahakama imesikiliza shauri lake na kutoa hukumu bila kufungwa na wanasiasa.
Huu ni ushindi tosha kwa Demokrasia ya Kenya.
 
Back
Top Bottom