Kenya Wako Kumwanya - Mashujaa Wetu wa Demokrasia?

Kosa la kwanza ni kuutelekeza mchakato wa katiba. Mengine ya mahakama na tume huru ni matokeo ya hilo kosa.
 
Hilo litakuwa suala jingine kabisa,
Muhimu ni kwamba Mahakama imesikiliza shauri lake na kutoa hukumu bila kufungwa na wanasiasa.
Huu ni ushindi tosha kwa Demokrasia ya Kenya.
Hata baba yako ni mtu mwingine kabisa lakini mtu akikutambulisha wewe kama mtoto wa baba yako, atakuwa hajakosea.

Habari niliyosema hapa ni kwamba, hii tabia ya Uhuru kuwa mpole sana na kuruhusu demokrasia inachangiwa na vurugu zilizotokea 2007 na kuepelekea kesi ya The Hague. Uhuru akitakakufanya uhuni wowote wa kuambia askari wapige waandamanaji sasa hivi, anakuwa anajishtukia kwa kuwa lile zimwila The Hague bado linamuelemea.

Huku kwetu hatuna hiyo element.Ndiyo maana watu wa upinzani wanapigwa kama mbwa koko, mahakama haziheshimiwi etc.

That element cannot be discounted.
 
Kenya inaonekana taasisi zake zipo huru na kuna uwazi kuliko Tanzania,Hivi kati ya Kenya na Tanzania ni ipi ipo corrupt zaidi? maana corruption ni kutumia madaraka vibaya
Hili ni somo zuri sana kwa wale wasioamini katika mifumo ya kiutawala
Uwepo wa vyombo huru tu unatosha kuleta maelewano.

Uchaguzi ukirudiwa Kenyatta akashinda tena si yeye tu bali Kenya yote itakuwa imeshinda

Kwetu sisi tume ya uchaguzi ikitamka tu hata bila kuhesabu kura,fulani kashinda hakuna wa kuhoji
Ndiyo yale ya Jecha kuwa tume na kuvuruga uchaguzi tena akiaambiwa apewe tuzo

Hapa kwetu Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anateuliwa na mwenyekiti wa CCM
Msajili wa vyama vya siasa anateuliwa na mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais
Majaji wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais si kama Kenya wanapoomba kazi

Orodha inaendelea. Kimantiki hata katika uadilifu wa kiwango cha malaika, anayeonyesha shaka juu ya hilo hapaswi kulaumiwa. Mfumo hauonyeshi ''impartiality' hata kwa hbahati mbaya
 
Hata baba yakoni mtu mwingine kabisa lakini mtu akikutambulisha wewe kama mtoto wa baba yako, atakuwa hajakosea.

Habari niliyosema hapa ni kwamba, hii tabia ya Uhuru kuwa mpole sana na kuruhusu demokrasia inachangiwa na vurugu zilizotokea 2007 na kuepelekea kesi ya The Hague. Uhuru akitakakufanya uhuni wowote wa kuambia askari wapige waandamanaji sasa hivi, anakuwa anajishtukia kwa kuwa lile zimwila The Hague bado linamuelemea.

Huku kwetu hatuna hiyo element.Ndiyo maana watu wa upinzani wanapigwa kama mbwa koko, mahakama haziheshimiwi etc.

That element cannot be discounted.

I totally agree with you,
Leo nimezungumza na watu na kuwaambia Uhuru Kenyatta asingepelekwa ICC leo Kenya ingewaka moto.
Imethibitika kwamba watawala wa Afrika bila kutishiwa na viranja wa nje wanaweza kuigeuza hii nchi kuwa The Gulag.
 
Huku kwetu demokrasia tutaipimia longido kwenye marudio ya uchaguzi kama kawaida yetu ukipiga kura usionekane kwenye kituo na vilevile tutakamata watu tuwaweke ndani kwa ajili ya upelelezi ili kumpa nafasi mkurugenzi wetu kutangaza mtu wetu na polisi na magari ya washawasha yatarandaranda kila kona kutekeleza domokrasia ya mzee wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna majibu mengi mazuri yametolewa leo kwa maswali mengi ambayo yanaitatiza siasa za Afrika - upinzani na watawala. Lakini pia kuna maswali mengine yameachwa wazi ambayo majibu yake yataamua kama Tanzania inaweza "kufuata nyayo" za kidemokrasia ambazo zimeoneshwa na Kenya leo.. na zinatarajiwa kuoneshwa tena siku sitini baadaye:

Kenyatta kalazimika kukubali sababu ya makandokando ICC,sababu anajua akifanya kinyume kesi bado mbichi name sio hiyari kwani ndio kinara wa kuvuruga uchaguzi 2007
 
Leo Kenya wameithibitishia Afrika na dunia nzima kwamba ni nchi gani ina wasomi wenye tija Afrika.
Leo nimewaogopa sana Wakenya na nitawaheshimu mpaka siku ninayoingia kaburini. (Sitanii kwa hili)
Nchi hii ndiyo pekee Afrika ambayo Katiba ya nchi inalindwa na Mahakama ,sidhani kama kuna nchi nyingine kama hii.
Daima historia itawakumbuka sana hawa Majaji wa Kenya.

Kitendo cha kuheshimu Mahakama kinaleta picha nzuri kwamba wananchi wako kwenye mikono salama.
Hapa kwetu Tanzania sisi tunaishi maisha ya hofu kama wakimbizi tusio na haki yoyote.
Hakuna anayeheshimu maamuzi ya Mahakama,Hakuna Utawala wa Sheria na Hakuna haki.

Ushahidi ni kule kinachoendelea kule Kimara,
Mahakama imeweka Zuio (Injunction) lakini wewe unabomoa tu,
Unategemea kama hauheshimu vidogo kama hivi makubwa utaheshimu kweli?
Hivi haki zetu za msingi zikivunjwa tunaweza kuheshimiwa na Mahakama zetu kweli?

Majaji wetu wengi ni wa aina ya
Mzee Lubuva, Mzee Mutungi na Mzee Augustino Ramadhani,
Ambao wanaheshimu ilani za Chama cha Mapinduzi kuliko Katiba ambayo wameapa kuilinda. Ukiwauliza kwanini mnyafanya hivyo wanakuambia "Every Country has its own legal traditions, and ours is this, this is our Jurisprudence" (What a lackadaisical statement from a learned intellectual)

Wanafalsafa wakubwa duniani kama,
Plato alivyozungumzia uwepo wa Muhimili wa Mahakama
A.V Dicey alivyozungumzia Utawala wa Sheria (Rule of Law)
Montesquieu alivyozungumzia Mgawanyo wa Madaraka (Separation of powers)
Waliishi na kuona hatari ya kurundika nguvu zote za dola kwenye chombo kimoja au mtu.
Sisi tunapuuza maarifa na kushangilia upumbavu usio na tija. (Tunaimba Zidumu Fikra)

Hebu angalia tu,
Kesi ya Kikatiba ya Marehemu Mtikila (Mgombea Binafsi) ilihukumiwa na makada wa CCM, (Augustino Ramadhani)
Huku Professor Kabudi (Mwana-CCM) kama Rafiki wa Mahakama (Amicus Curriae) alienda pale kufanya UZANDIKI tu.
Walifanya figisu figisu hadi Jaji Mkuu Mstaafu Mzee Samatha aliwaponda sana kwa ule ujinga wao. (Tafuta Kitabu chake cha RULE OF LAW VS RULERS OF LAW utaelewa ninachokisema)

Watanzania tuachane na hizi SIASA za CHADEMA na CCM,
Albert Einstein once said "You can't solve the problem at the same level it was created"
We deserve better than being under the thumb of these thugs.
We deserve a better life than this.

Al-Watan , Ndahani , Mzizi wa Mbuyu , JokaKuu
 
Wengi wanadhani matokeo ya hukumu ndilo jambo muhimu, hapana!

Kwa siasa za Afrika mkondo wa maelewano umetengenezwa ima kulazimisha hali fulani kama ilivyo hapa kwetu ambapo matokeo hayahojiwi, au kuingia katika machafuko kwavile mmoja ana nguvu kama ilivyo nchi nyingine na jirani zetu

Kilichotokea Kenya, kampeni zilifanyika kwa njia za kiustaarabu 'fair' kwa std zetu
Matokeo yakatangazwa hadharani na tume ya uchaguzi

Aliyeshindwa akampongeza aliyeshinda
Uhuru wa kupinga kilichoktokea ukatolewa kwa anayetaka kuandamana au mikutano

Aliyeshindwa akafuata mkondo wa sheria kutafuta anachodai hakikuwa sawa

Sheria ikaamua kuwa kuna dosari na uchaguzi urudiwe

Pande zikakubali matokeo ya mkondo wa sheria hata kama hawakubali matokeo ya sheria

Kumbe basi Waafrika tunaweza kufanya mambo bila kuwa katika TV za kuonyesha michirizi ya damu

Hiki ndicho kikubwa na muhimu kuliko hukumu yenyewe
Ulichoongea ni sahihi kabisa ila hukumu pia imeandika historia katika siasa za Afrika. Kwamba dosari kwenye chaguzi zetu zilikuwa zikidharauliwa na kukanushwa na watawala (washindi wa chaguzi) ikiwamo wizi. Ambacho si cha muhimu ni nani alyeshinda au kushindwa katika hukumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenyatta Katoa Hotuba Iliyojaa Busara Kubwa, Ingekua Ni Huku Tanzania Ungesikia "Hao Majaji Tutarara Nao Mbere Kwa Mbere" !!
Hakuna hekima yoyote pale.Anasema eti watu sita tu wametengua maoni ya watu milioni kadhaa,hiyo ni kuikosea adabu korti
 
ni matumaini kila atakaeonekana alisababisha ni mwendo wa kupotea na mungiki wanarudi rasmi kazini!
 
Leo Kenya wameithibitishia Afrika na dunia nzima kwamba ni nchi gani ina wasomi wenye tija Afrika.
Leo nimewaogopa sana Wakenya na nitawaheshimu mpaka siku ninayoingia kaburini. (Sitanii kwa hili)
Nchi hii ndiyo pekee Afrika ambayo Katiba ya nchi inalindwa na Mahakama ,sidhani kama kuna nchi nyingine kama hii.
Daima historia itawakumbuka sana hawa Majaji wa Kenya.

Kitendo cha kuheshimu Mahakama kinaleta picha nzuri kwamba wananchi wako kwenye mikono salama.
Hapa kwetu Tanzania sisi tunaishi maisha ya hofu kama wakimbizi tusio na haki yoyote.
Hakuna anayeheshimu maamuzi ya Mahakama,Hakuna Utawala wa Sheria na Hakuna haki.

Ushahidi ni kule kinachoendelea kule Kimara,
Mahakama imeweka Zuio (Injunction) lakini wewe unabomoa tu,
Unategemea kama hauheshimu vidogo kama hivi makubwa utaheshimu kweli?
Hivi haki zetu za msingi zikivunjwa tunaweza kuheshimiwa na Mahakama zetu kweli?

Majaji wetu wengi ni wa aina ya
Mzee Lubuva, Mzee Mutungi na Mzee Augustino Ramadhani,
Ambao wanaheshimu ilani za Chama cha Mapinduzi kuliko Katiba ambayo wameapa kuilinda. Ukiwauliza kwanini mnyafanya hivyo wanakuambia "Every Country has its own legal traditions, and ours is this, this is our Jurisprudence" (What a lackadaisical statement from a learned intellectual)

Wanafalsafa wakubwa duniani kama,
Plato alivyozungumzia uwepo wa Muhimili wa Mahakama
A.V Dicey alivyozungumzia Utawala wa Sheria (Rule of Law)
Montesquieu alivyozungumzia Mgawanyo wa Madaraka (Separation of powers)
Waliishi na kuona hatari ya kurundika nguvu zote za dola kwenye chombo kimoja au mtu.
Sisi tunapuuza maarifa na kushangilia upumbavu usio na tija. (Tunaimba Zidumu Fikra)

Hebu angalia tu,
Kesi ya Kikatiba ya Marehemu Mtikila (Mgombea Binafsi) ilihukumiwa na makada wa CCM, (Augustino Ramadhani)
Huku Professor Kabudi (Mwana-CCM) kama Rafiki wa Mahakama (Amicus Curriae) alienda pale kufanya UZANDIKI tu.
Walifanya figisu figisu hadi Jaji Mkuu Mstaafu Mzee Samatha aliwaponda sana kwa ule ujinga wao.

Watanzania tuachane na hizi SIASA za CHADEMA na CCM,
Albert Einstein once said "You can't solve the problem at the same level it was created"
We deserve better than being under the thumb of these thugs.
We deserve a better life than this.
Umemaliza mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa la kwanza ni kuutelekeza mchakato wa katiba. Mengine ya mahakama na tume huru ni matokeo ya hilo kosa.

Tatizo kwetu ni kuwa mchakato wa Katiba ulikuwa ni dubwasha lililotengenezwa na watawala na kubambikizwa kwa taifa na watu wakalidandia. Mchakato wenyewe ulianza vibaya ndio matokeo yake yalikuwa mabaya.
 
Kenyatta zile speeches anatoa kama Obama. Kwa ku inspire watu kwa speech tu, kakaa vizuri.

Mimi najiuliza,uchaguzi ukirudiwa halafu Raila akashindwa tena, itakuwaje?

Tatizo siyo kushindwa tena; hoja ni kuwa kweli ashindwe tena. Sidhani kama kuna kikomo cha kupinga ushindi wa Urais Kenya. Ni kwa maslahi ya Uhuru na Wakenya wenyewe kuhakikisha kuwa jaribio la pili la kumchagua Rais lina matatizo madogo zaidi kuliko ilivyo sasa ili kwamba hata mtu akishinda tena au akishindwa tena awe tayari kumpigia simu mwenzie na kumpongeza kwa ushindi wake. Kusiwe na wingu la hisia kuwa kuna 'kamchezo".
 
Atasema lolote, muhimu katika yote ni je anakubaliana na hukumu? Kama anakubali uchaguzi urudiwe atakuwa ameheshimu mkondo wa sheria hata kama hana heshima na matokeo ya mkondo huo.
Of course ni lalamike aseme maneno ya kukandia kidogo maana hili waliamini limepita na hasa baada ya kukosekana vurugu kubwa mitaani wakajua mahakama itathibitisha tu. Tatizo ni ushahidi; ili kumthibitisha Uhuru kama Rais ingebidi mahakama itupilie mbali uzito wote wa ushahidi uliokuwa mbele yao na uelezee kwanini imeupuuzia.
 
Kuna majibu mengi mazuri yametolewa leo kwa maswali mengi ambayo yanaitatiza siasa za Afrika - upinzani na watawala. Lakini pia kuna maswali mengine yameachwa wazi ambayo majibu yake yataamua kama Tanzania inaweza "kufuata nyayo" za kidemokrasia ambazo zimeoneshwa na Kenya leo.. na zinatarajiwa kuoneshwa tena siku sitini baadaye:

Wewe pia ni mmoja wapo uliiweka rehani demokrasia baada ya kujulikana bei yako demokrasia ni msimamo na tunda la haki , sio ubabe wala fitna na husda . Wala sio udikteta uchwara uliopo sasa! Ni aibu na muona aibu wote mnaosifu demokrasia ya kenya ambayo muhura uliopita tuu walikuwa wanaomba tuwasaidie kwenye siasa zao, sasa tumerudi nyuma tunajifunza siasa na demokrasia za siasa zao, ccm na kundi lenu aibu aibu saaaaana!!.

mzee mzima haishiwi maneno
 
Back
Top Bottom