Kenya, Uganda na Rwanda waweka makubaliano ya ulinzi

Kenya, Uganda na Rwanda waweka makubaliano ya ulinzi

Ni kweli ila kenya isingejiingiza huko maana mahusiano yetu na wao ni zaidi ya rwanda na uganda. Hata kwanza ukiuliza hata wakenya wanakerwa sana na uamzi wa rais wao kuvunja mahusiano wao na Tz
 
ulichokisema na mimi nilitaka kumwambia hivyo hivyo huyu jamaa, kagame hataki upinzani ndio maana media za rwanda zimebaki kumsifia tuu. Kaenda uingereza katupiwa mawe.

lakini nafikiri mwisho utafika nyoka atapondwa kichwa tu
 
Hebu tuacheni kwanza tupo busy na Zitto sasa hivi
 
Tujiulize je kuna faida yoyote tutakayoipata?? Waendelee tu sisi hatuwahitaji
 
hapo umesema mkuu. Usishangae tz tukaombwa kusaidia mambo yakiharibika

siyo mara ya kwanza! Uganda baada ya amini kuharibu hali ya hewa huko uganda ni tanzania ilipigiwa magoti kuikomboa uganda, rwanda walipoanza kuchinjana kama mbuzi ni tanzania tulimtuma mwalimu nyerere kwenda kuwapatanisha, kenya walipoanza kuchinjana baada ya matokeo ya uchaguzi 2007 tanzania yetu kama kwaida ilikuwa kimbilio tukamtuma mzee wetu mkapa kuwapatanisha, lakini sasa inabidi tujifikirie upya ! Tumezungukwa na mashetani
 
ni kweli, kwani raia wa rwanda hana chaguo lingine zaidi ya kuonesha kuwa wanampenda hata kama hawampendi, kwani anatawala nchi kwa mkono wa chuma. Kama walioko nje wanafuatwa kuuawa sembuse raia iliyeko ndani? Si nchezo aise!! Jeshi la taifa limeshikiliwa na minority (14% population), wewe unafikiria majority watafurukuta kuonesha msimamo wao?

ukweli ndi huo mkuu.. Kagame anapendwa kwa uchapakazi wake na sio hayo unayoongea. Ungefanikiwa kwenda rwanda nadhani ungeshuhudiya mwenyewe
 
voice of america pia wameelezea hili. Waziri wa ulinzi wa rwanda kaulizwa kwa nini tanzania na burundi hamjazishirikisha,kajikanyagakanyaga tu!nadhani bongon tuwe nao macho hawa!

wanafiki mara nyingi wakishikwa pabaya ni sawa sawa na mende aliyebanwa na mlango, asineweza kujitetea kwani nia yao ovu kwa tanzania ni dhahiri hata mtoto mdogo anaifahamu
 
mkuu usijipe moyo tu,,,, hawa jamaa wana mikakati mikubwa zaidi ya unavozani

mikakati yao ya kuua na kupora mali asili ya drc tumefanikiwa kuizuia, ipi mingine? Usisahau wahutu nao wanapigana usiku kutwa kuikomboa nchi yao
 
Ni kweli ila kenya isingejiingiza huko maana mahusiano yetu na wao ni zaidi ya rwanda na uganda. Hata kwanza ukiuliza hata wakenya wanakerwa sana na uamzi wa rais wao kuvunja mahusiano wao na Tz
lakini jk full kujipendekeza, alikwenda kwenye sherehe za uhuru wa kenya wakati kenyata hakuja kwenye sherehe za uhuru wa Tanzania,
 
wanamgambo wanne tu wa alshabab walilisumbua jeshi dhaifu la kenya kwa muda wa zaidi ya siku nne, waasi wa lra bado ni tishio kubwa kwa utawala wa museveni sasa ni zaaid ya miaka 20, rwanda hali ni tete kiusalama, haijulikana kesho itakuwaje kutoka kwa wahutu wanaonyanyaswa na kuteswa na serikali ya kitusi ya kagame . Wote watu (maraisi) ni wanted wa icc watarajiwa . Tanzania hatuwahitaji

hatuwahitaji ila tunawamezea mate
 
Waendelee tu kujitenga sisi nchi yetu tunasonga mbele atuwaitaji wezi wa madini
 
Back
Top Bottom