Kenya: Rais John Magufuli azua minong'ono

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1472649402344.jpg


Serikali ya Kenya imepuuza kutokuwapo kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati wa mkutano wa kimataifa uliomazika hivi karibuni nchini hapa.

Hilo limetokana na kuenea kwa minong'ono na wasiwasi miongoni mwa wakenya juu ya dhamira yake ya utangamano wa kikanda.

Wakenya wengi walitarajia Rais Magufuli kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa Mashariki na uwapo wa Japan kupitia mpango wake wa ushirikiano na maendeleo ya Africa (Ticad) angehudhuria mkutano huo.

Lakini Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Amina Mohamed, alipuuza madai hayo akisema Rais Magufuli alituma mwakilishi, Waziri Mkuu Kassim majaliwa.

"Si yeye pekee ambaye hakuhudhuria mkutano, kusema kweli aliwakilishwa vyema na hakuna haja ya kuhofia. Tanzania na Kenya zina uhusiano mzuri, tuache kujikita kuwa wabaya "alisema Waziri Amina Mohamed katika mahojiano kwa njia ya simu.

Tangu aingie madarakani Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli ametembelea Uganda na Rwanda pekee.

Tofauti na mtangulizi wake Jakaya Kikwete ambaye alijulikana kwa kusafiri nje, Rais Magufuli amejikita katika masuala ya nyumbani, akimbambana na ufisadi katika utumishi wa umma.


Chanzo: Mtanzania
 
Eti serikali ya Kenya imepuuza! Serikali ya Kenya na mkutano huu wapi na wapi!, mkutano ungeweza kufanyika nchi yeyote ndani ya jumuiya so serikali ya kenya haihusiani kabisa usiisingizie.
 
Wote ngeli tumejifunza tu kwa hiyo hakuna wakumcheka mwenzake sio wakenya au wtz magufuli kutokwenda isihushwe na lugha ukizingatia waliokwenda kwenye huo mkutano kwa ajili ya kuonyesha umahiri wa kuongea english kwani kulikuwa na wanozungumza kireno kiarabu kifaransa n.k
 
Duh, Magu huyu bodyguard wake inaonekana kazi anaiweza haswa. Cheki alivyokunja ndita. Hivi yule mwanamama aliyekuwa katika convoy ya magufuli wakati anaanza uongozi yupo wapi.?

KPwZL6N.jpg
 
Back
Top Bottom