Kenya: Ndege yapotea angani ikiwa na watu 10 huko Aberdares. Mabaki ya ndege hiyo yapatikana, abiria wote wafariki

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Ndege moja humu nchini iliyokuwa imebeba watu kumi Jumanne jioni imetoweka ikiwa angani kilomita 60 kutoka jijini Nairobi, Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Trans Nzola Samson Ole Kine alithibitisha, ilikuwa inatoka mjini Kitale ikielekea Nairobi.

IMG-20180606-WA0004.jpg

Ndege hiyo aina ya Cesna C208 yenye namba za usajili 5YCAC inamilikiwa na Kampuni ya Fly Sax nchini humu, na inakisiwa kutoweka kwenye mawimbi ya udhibiti wa safari za ndege, rada, katika eneo la msitu wa mlima Aberdares.

Shirika la Mamlaka ya Usimamizi wa Safari za Ndege nchini (KCAA) lilithibitisha habari hizo kupitia akaunti yake ya Twitter Jumanne usiku.

"Tunathibitisha ripoti ya ndege iliyokuwa ikitoka Kitale kuelekea Nairobi kutoweka angani. Ilionekana mara ya mwisho kwenye mawimbi ya rada saa nane na dakika mbili mchana maili 40 kutoka jijini Nairobi ikipaa juu kwa urefu wa futi 11,000", umesema ujumbe huo.

IMG-20180606-WA0005.jpg

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS), anayesimamia maeneo ya milima, Simon Gitau Jumanne usiku alisema Shughuli za kuitafuta ndege hiyo zimeanza katika milima ya Aberdares.

"Utafutaji kwa njia ya angani hauwezekani kwa sasa kutokana na hali ya hewa lakini utafanyika Jumatano asubuhi", alisema.

IMG_20180606_000637_222.jpg

UPDATES:
Utafutaji wa Ndege aina ya Cesna C208 yenye namba za usajili 5YCAC iliyopotea Juni 05, 2018 ukiendelea ambapo leo baada ya takribani saa 48 mabaki ya ndege hiyo yameonekana huko Njabini, katika eneo la msitu wa mlima Aberdares

em.jpg

Mabaki hayo yameonekana kwa kutumia utafutaji wa kutumia ndege, hivyo timu ya uokoaji ya watu waliopo ardhini pamoja na timu ya madaktari wanelekea katika eneo hilo

UPDATES:

Abiria wote 10 waliokuwemo kwenye ndege iliyopata ajali baada ya kupotea angani na kuanguka katika eneo la Njabini, Aberdares wamefariki dunia

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Fly Sax inayomiliki ndege hiyo.

1.jpg


2.jpg


3.jpg
 
Nawatakia heri kwa kweli!
Ionekane hiyo ndege na abiria wawe salama
 
The ill fated light cessna 208 plane has been located. All passengers confirmed dead. Two lady pilots among those who perished.
RIP Barbara and Jean as well as all the passengers.
May God comfort their families.
34581597_1149941735146956_6914449329931419648_n.jpg

34512479_1149941765146953_731116906815160320_n.jpg
 
Mapema mno kutabiri kuwa wamefariki
The ill fated light cessna 208 plane has been located. All passengers confirmed dead. Two lady pilots among those who perished.
RIP Barbara and Jean as well as all the passengers.
May God comfort their families.
 
Back
Top Bottom