Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,695
- 1,195
Interesting debate,
Nadhani tunahitaji new elections in one year!
Naafikiana na matatizo- kulingana na haya yaliotokea Kenya- Kibaki wala Raila wasigombee!
Wagombee watu wengine neutral!
Matatito na Ab-tizchz, we can make our arguments bila kuongelea Ukikuyu, Uluo, Ukamba n.k. Mnajua JF huwa hatujadiliani kwa misingi ya Kikabila!
Mzalendo, acha nikupe unielewe.Mie siongei na misingi ya kwamba nachukia kabila au nina ukabila.Ukweli ni kwamba waafrika tumezaliwa katika makabila na hata iweje hio nd'o hali halisi.
Kisha pia inabidi ufahamu psyche ya wakikuyu kule Kenya nd'o utaelewa matatizo ya hawa mabwana.Kwanza kabisa mkikuyu nadhani alikula kiapo toka enzi za Kenyatta eti hatoweza kutawaliwa na wajaluo...kisa na kisababu? Wajaluo wanamagovi!!Yaani hata wale waliosoma watakuambia hii kitu.Kama ulikua unatembelea kule Mashada wakati wa kampeni ungeona hio ishu kila siku.These has been their rallying point na pia turning other people against Luos.Yaani for more than 40yrs hii imekua sera yao.Hata hivyo wakenya wengine wakaanza kuona hii kitu haina maana na wakanza kumsikiza Raila.Wenyewe walikuwa wanasema eti Raila is unelectable.Basi ODM ilipolaunch Rally yake pale Nairobi walipigwa na butwaa kuona umati ulioshehena sehemu.Sasa hapo nd'o ikabidi waingie overdrive ya kucounter the guy maana waliona eeh!..huyu bwana atachukua hii kitu!!!
Pia wakikuyu wanawasiwasi ambao viongozi wao wamewatia akilini kuwa mjaluo akiongoza Kenya basi atawanyanyasa kishenzi kulingana na kua Kenyatta(yule rais wa kwanza)aliwaua wajaluo kishenzi na hamna lolote wangefanya.Viongozi wa maana wa kabila la wajaluo waliobwagwa ni kama Tom Mboya,Horace Ongili Owiti na Robert Ouko.Kisha sehemu ya Nyanza imenyimwa vigezo vyovyote vitakavyosaidia kukuza uchumi.Kwa hivyo mahesabu yote ya Kenya yanafanywa na ukabila ndani yake na ukitaka kuwajadili hawa mabwana lazima hio kitu utie akilini.
Tegemeo letu ni hiki kizazi kipya ambacho nadhani walienda shule na kuelimika kama wanavyojaribu kututambia.Hata hivyo bado wana-ukabila hata sijui vipi.Mfano huyo bwana tunayejadiliana naye hapo juu katuambia wazi ni mkikuyu.Nani kamuuliza?Si unaona ninachosema?Unatarajia kwa vile anacheza na mtandao basi upeo wake umezidi lakini wapi...ni wale wale.Hii mada ni kubwa na hivi karibuni nitabwaga kurasa kadhaa kukuonyesha ubepari wa hawa mabwana.Hata Mwalimu Nyerere angeshangaa nao.
Naomba kuwasilisha.