Warioba na Tume yake walishamaliza kazi, sasa mbona Warioba anachonga kila siku wakati alishamaliza kazi?
Kazi yake binafsi?
Wakuu,
Jaji Warioba amesisitiza mara kwa mara kwamba "Wananchi Walio Wengi" walitaka Muundo wa Muungano uwe wa Serikali 3 na sio wa Serikali 2! Mara baada ya kupitishwa Katiba inayopendekezwa tulitarajia "wananchi walio wengi" waandamane na kupaaza sauti kwa kuwa maoni yao ya Serikali 3 yametupwa na Bunge Maalum la Katiba! Badala yake tumewaona UKAWA ndio waliokasirishwa sana na kutupwa maoni yanayokubali Muundo wa Serikali 3 na sio wananchi wa kawaida "walio wengi!"
Kinyume chake tumeona wananchi wakiendelea na shughuli zao kama kawaida huku UKAWA wakijaribu kuwashawishi waandamane bila mafanikio yoyote! Tulimshuhudia Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, akiswekwa ndani na wafuasi wachache wa CHADEMA kwa kuleta fujo na kuhatarisha amani! Hakuna wananchi waliojiunga na kikundi hicho cha CHADEMA kupinga "maoni yao kutupwa" na Bunge Maalum la Katiba!!
Hali hii inashawishi mtu aamini kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali 2 haujawa kero kama UKAWA wanavyotaka tuamini! Kama Muundo huu wa Serikali 2 ni kero basi kero hiyo ni kwa wana-UKAWA tu na sio kwa mtu mwingine yeyote!!
Tujadili!!
Haya ni mambo ya kujitekenya na kucheka mwenyewe siyo mbaya endelea kujitekenya halafu ucheke mwenyewe.
Mkuu wananchi wakiamua kama jambo linawakera hakuna kifaru kitakachoweza kuwazuia! Uwepo wa Polisi hauwezi kuwazuia wananchi waliokerwa!! Issue ni kwamba wananchi hawajakerwa!! Wananchi wakikerwa huwa hawazuiliki!! Jaribu ku-recall enzi za Vita vya Maji Maji jinsi wananchi walivyokerwa na kujitolea maisha yao!!
Wananchi waliokerwa unawafahamu mkuu? Huwa hawajali mbwa, maji, polisi au virungu! Tatizo ni pale wana-UKAWA wanapojaribu kujenga hoja zao kupitia migongo ya wananchi!Wananchi wa kawaida hawawezi kuthubutu kuingia mitaani wakati waljotunga katiba hiyo wamemwaga plisi, mbwa, maji ya kuwasha na madifenda na kuamuru WAPIGWE TU. Demokrasia kimsingi iko midomoni kivitendo ni MAKABURU TU. Hakuna tofauti na ilivyokuwa SOWETO kwa vitendo. Tofauti khbwa ni kwamba Soweto watesi walikuwa wazungu na hapa kwetu ni weusi tena ni kaka zetu, wakwe zetu, shemeji zetu, wajomba. Zetu, wanafunzi wetu n.k. Lakini MUNGU ni mkuu sana time will tell.
Kwa kuwa "Wananchi walio wengi" hawaelewi ndio maana Bunge Maalum la Katiba likaboresha maoni yao!