Kelele za UKAWA na ukimya wa wananchi walio wengi

Kelele za UKAWA na ukimya wa wananchi walio wengi

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,978
Wakuu.

Jaji Warioba amesisitiza mara kwa mara kwamba "Wananchi Walio Wengi" walitaka Muundo wa Muungano uwe wa Serikali 3 na sio wa Serikali 2! Mara baada ya kupitishwa Katiba inayopendekezwa tulitarajia "wananchi walio wengi" waandamane na kupaaza sauti kwa kuwa maoni yao ya Serikali 3 yametupwa na Bunge Maalum la Katiba! Badala yake tumewaona UKAWA ndio waliokasirishwa sana na kutupwa maoni yanayokubali Muundo wa Serikali 3 na sio wananchi wa kawaida "walio wengi!"

Kinyume chake tumeona wananchi wakiendelea na shughuli zao kama kawaida huku UKAWA wakijaribu kuwashawishi waandamane bila mafanikio yoyote! Tulimshuhudia Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, akiswekwa ndani na wafuasi wachache wa CHADEMA kwa kuleta fujo na kuhatarisha amani! Hakuna wananchi waliojiunga na kikundi hicho cha CHADEMA kupinga "maoni yao kutupwa" na Bunge Maalum la Katiba.

Hali hii inashawishi mtu aamini kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali 2 haujawa kero kama UKAWA wanavyotaka tuamini! Kama Muundo huu wa Serikali 2 ni kero basi kero hiyo ni kwa wana-UKAWA tu na sio kwa mtu mwingine yeyote.

Tujadili.
 
Wakuu,

Jaji Warioba amesisitiza mara kwa mara kwamba "Wananchi Walio Wengi" walitaka Muundo wa Muungano uwe wa Serikali 3 na sio wa Serikali 2! Mara baada ya kupitishwa Katiba inayopendekezwa tulitarajia "wananchi walio wengi" waandamane na kupaaza sauti kwa kuwa maoni yao ya Serikali 3 yametupwa na Bunge Maalum la Katiba! Badala yake tumewaona UKAWA ndio waliokasirishwa sana na kutupwa maoni yanayokubali Muundo wa Serikali 3 na sio wananchi wa kawaida "walio wengi!"

Kinyume chake tumeona wananchi wakiendelea na shughuli zao kama kawaida huku UKAWA wakijaribu kuwashawishi waandamane bila mafanikio yoyote! Tulimshuhudia Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, akiswekwa ndani na wafuasi wachache wa CHADEMA kwa kuleta fujo na kuhatarisha amani! Hakuna wananchi waliojiunga na kikundi hicho cha CHADEMA kupinga "maoni yao kutupwa" na Bunge Maalum la Katiba!!

Hali hii inashawishi mtu aamini kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali 2 haujawa kero kama UKAWA wanavyotaka tuamini! Kama Muundo huu wa Serikali 2 ni kero basi kero hiyo ni kwa wana-UKAWA tu na sio kwa mtu mwingine yeyote!!

Tujadili!!

Jaribu kushirikisha ubongo wako na hali halisi…Mara ngapi nyie intarahamwe na polisi yenu mmewazuia wana UKAWA kuandamana..kila wakati pale bungeni mlikuwa mnalalamika…kama kweli rasimu ya Sitta/Chenge ilikuwa ni chaguo la wananchi..kwa nini siku Kikwete anakabidhiwa hiyo rasimu kulikuwa na uwingi wa polisi pale Dodoma???
 
Kwani wana ukawa sio watanzania? Au ni wakenya? Weka hoja yako vizuri
 
Mkuu wananchi wakiamua kama jambo linawakera hakuna kifaru kitakachoweza kuwazuia! Uwepo wa Polisi hauwezi kuwazuia wananchi waliokerwa!! Issue ni kwamba wananchi hawajakerwa!! Wananchi wakikerwa huwa hawazuiliki!! Jaribu ku-recall enzi za Vita vya Maji Maji jinsi wananchi walivyokerwa na kujitolea maisha yao!!
 
Watanzania bado wako gizani.........na huwa siwaelewi anyway ipo siku watajitambua lakini mengi zaid wamejaribu kuweka viongoz wanaowataka ila uchakachuzi wa kura nao unawakatisha tamaa hebu imagine yaliyotokea jimbo la segerea.....na huki shinyanga...mpaka mimi nilishaaamua hamna haja ya kwenda kupiga kura kwa sbb matokeo huwa yanapikwa
 
Kwani wana ukawa sio watanzania? Au ni wakenya? Weka hoja yako vizuri

Hoja inahusu wana-UKAWA (kikundi cha watanzania wachache) vs Wananchi wa Tanzania walio wengi!!
 
Ukawa ni sumu ya kuuwa ccm na vibaraka wake wote
 
Mbona mnatumia jeshi? Wanaukawa ni wengi kuliko wana ccm ccm wana kadi za uanachama wengi lkn wenye fikra sahihi mambo ukawa
 
Ukawa ni sumu ya kuuwa ccm na vibaraka wake wote

UKAWA hii hii ninayoifahamu (CHADEMA, NCCR na CUF) au nyingine mkuu? Don't you know kwamba urafiki kati ya CHADEMA, NCCR na CUF ni kama urafiki wa simba, pundamilia na fisi? Don't remember lugha za CCM B, C, nk? Subirini tu mwakani sio mbali!!
 
Mbona mnatumia jeshi? Wanaukawa ni wengi kuliko wana ccm ccm wana kadi za uanachama wengi lkn wenye fikra sahihi mambo ukawa

Umewahi kuona Serikali ya wapi isiyotumia jeshi? Kama UKAWA wanaleta vurugu waachwe tu, kwa lipi? Kuhusu fikra, hata Shetani huwa anafikiri kwamba ana fikra sahihi dhidi ya Mungu!!
 
Lakini tuache utani ukawa ikifa wanachama wa ccm wataongezeka vitambi
 
UKAWA hii hii ninayoifahamu (CHADEMA, NCCR na CUF) au nyingine mkuu? Don't you know kwamba urafiki kati ya CHADEMA, NCCR na CUF ni kama urafiki wa simba, pundamilia na fisi? Don't remember lugha za CCM B, C, nk? Subirini tu mwakani sio mbali!!
kesho tunasaini makubaliano maalumu kama una kuna tv angalia STARTV au ITV kuanzia saa nane mchana ukawa inawatesa sana wapuuzi wa ccm
 
Lakini tuache utani ukawa ikifa wanachama wa ccm wataongezeka vitambi
UKAWA haiwezi kufa kwa sababu UKAWA ndo njia sahihi ya kuindoa serikali ya ccm madarakani UKAWA ni mwiba mkali kwa serikali ya ccm huo ndo ukweli
 
Hivi kweli hawa wananchi ambao hata katiba hii ya sasa hawaijui ndiyo kweli tuseme wanataka serikali tatu!
 
kesho tunasaini makubaliano maalumu kama una kuna tv angalia STARTV au ITV kuanzia saa nane mchana ukawa inawatesa sana wapuuzi wa ccm

Kila lakheri mkuu, msisahau kuwa kuna CCM B humo humo! Msije mkalalamika kuwa hamkuambiwa!
 
UKAWA haiwezi kufa kwa sababu UKAWA ndo njia sahihi ya kuindoa serikali ya ccm madarakani UKAWA ni mwiba mkali kwa serikali ya ccm huo ndo ukweli

Mkuu mtabaki kuwa wapinzani tu maana njia mnazotumia kutaka kuingia madarakani wananchi wameshazishtukia!
 
Lakini tuache utani ukawa ikifa wanachama wa ccm wataongezeka vitambi

UKAWA ni kama popo ambaye ana sifa za kuwa ndege na sifa za kuwa mnyama! Hatujui kuwa UKAWA ni chama, NGO, SACCOS au kitu gani! Hatujui sifa za kujiunga na UKAWA ni zipi, uongozi ukoje, malengo yake ni yapi, nk!
 
Back
Top Bottom