Kejeli nilizoambiwa siku naachana naye

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Wakuu mmebarikiwa Sana na Mungu wa Mbinguni hakuna laana.

Leo naendelea na muha taeleza siku naondoka rasmi na kuachana Naye.

Nakumbuka nyakati hizo Yule mwanamke alizidi kunipanda kichwani alianza tabia za kurudi usiku Sana nyumbani yaani Mimi nilikuwa nafanya kazi maeneo ya ubalozi WA kenya nawahi kufika kibaha kuliko yeye aliyekuwa Tu hapo mbezi ya kimara alikuwa anafika nyumbani Saa nne au Saa tatu na ni mwalimu nadhan mnaelewa mwisho vipindi mashuleni.

Skuwa najari Sana maana hata sikuwa na wivu Naye wala sikuwa hata namuuliza lolote alikuwa anakuta mi nimeshapika na nimelala kabisa na mtoto wangu aliyekuwa standard 2.

Kuna wengine watashangaa kuhusu mtoto kwani nilisema alifariki aliyefariki ni mdogo wake na huyu sasa, Huy ni wa kike.
Akifika anagonga mlango nafungua anaingia anakula nilichopika na siulizi Ila narudi zangu kulala.

Nilikuwa nimeomba kazi nyingine niliunganishiwa na bro wangu aliyekuwa na mke mchawi kama mtakumbuka kisa chake. Sasa zilikuwa zimebaki kama siku tano mi kukabizi ofisi huko dar kisha nisafiri kuja kanda ya ziwa kwenye kazi mpya.

Siku moja akirudi usiku kwenye Saa tatu hivi alikuta natoa vyombo vichafu nampa binti yangu anavitoa nje huko nilitaka avikute nje huko maana vingine vilikuwa na wiki viko ndani ni vichafu ilifikia hatua ukitaka kupika inabidi nioshe viwili vitatu nipate cha kupikia ili mtoto wangu ale.

Wakati binti yangu anatoka na baadhi ya vyombo akakutana na mama yake mlangoni akamwambia virudishe ndani nikamsikia nikamwambia mtoto peleka nje mama MTU anasema virudi ndani nilitoka Kwa hasira nikavichukua nikavitupa huko nje.

Aisee yalianza maneno mazito na matusi juu mbele ya mtoto wangu takribani masaa mawili mtu anafoka mpaka majirani wanasikia.
Alisema 👉 wewe ni mjinga Tu, fala wewe, unajidai unajua kutomba wapo wanaojua kutomba kuliko wewe, kama ni kusepa we sepa Tu, Achana na Mimi mtoto WA shetani wewe, Baba yako ni shetani, waambie hata na ndugu zako mi siogopi lolote nenda kawaambie na wazazi wako huko, huna akili hata kidogo, shoga wewe.

Baada ya kunishambulia Sana mi nikiwa kimya Tu na mtoto anashangaa Tu, akachukua simu yake akampigia mama yake akadai mi nataka kumpiga na maneno mengine mengi Tu sjui alijistukia kuona mi nipo kimya akajua pengine usiku Sana taliamsha dude. Akamwambia mama yake eti 👉 uskiskia nmekufa ni huyu Baba........ndo kaniua.

Mmmh niliduwaa Sana nakumbuka nilipaki vitu vyangu rasmi usiku ule ule nikabakiza nguo kama tatu za kuendea kazini ili nikakabizi ofisi ya watu.

Zikipita siku mbili nikamuita nikamwambia sichukui chochote kile kwenye mji huu Ila nahitaji ondoka na mtoto akajibu 👉 ukimtaka mtoto huyu labda unikate shingo ndo umchukue, nikamwambia sawa Kila la kheri.

Asubuhi nilibeba bengi langu nikaondoka zangu mpaka leo hii ni miaka sasa miwili na nusu sikuwahi onana Naye na nilishaoa sasa.
Nitawambia siku nyingine nini kilijiri baada ya kuondoka.

Karibuni wakuu Kwa povu, matusi, kejeri, maoni, ujuaji, kebehi, dharau, pole, salamu NK.
 
Hatua ulizochukua makini sana pia nakupongeza,huyo mwanamke kwanza mshamba baada ya kumuacha kwa vyovyote kesha kuwa mzigo kwa mchepuko atakuwa alitamba labda miezi 6 baada ya wewe kuondoka sasa hivi kwa vyovyote ni gombania goli nakushauri mfatilie mtoto akigoma achana nae zaa wengine.
 
Back
Top Bottom