Baada ya Miaka 30 Huyu Hapa Ahukumiwa Kwenda Jela Mauaji ya Mwanamuziki 2Pac

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
442
Reaction score
1,085
Baada ya takriban miaka 30 ya sintofahamu kuhusu kifo cha rapa maarufu Tupac Shakur, kiongozi wa zamani wa kundi la “South Side Compton Crips”, Duane “Keffe D.” Davis, amepatikana na hatia ya mauaji yake.

Kifo cha Tupac mwaka 1996 katika shambulio la risasi lililofanywa na watu waliokuwa ndani ya gari kinasalia kuwa moja ya mafumbo makubwa katika utamaduni maarufu; kukiwa na nadharia nyingi zisizo na idadi lakini bila kukamatwa kwa mtu yeyote hadi mwaka 2023, wakati Davis alipofunguliwa mashtaka ya mauaji bila kutarajiwa.

Katika wiki za hivi karibuni, kesi hiyo inayoendelea Las Vegas imejikita katika kitabu cha kumbukumbu alichochapisha Davis mwaka 2019, ambamo aliandika kuwa yeye ndiye aliyetoa silaha iliyotumika kumuua Tupac.

Davis na wakili wake walidai kuwa hayo yalikuwa ni hadithi za kubuni na majigambo yaliyolenga kuuza vitabu, lakini baraza la wazee wa mahakama lilichukua saa chache tu kufikia uamuzi wa kumtia hatiani.

Kama anavyoandika mwandishi wa BBC News anayeshughulikia eneo la Amerika Kaskazini, Shaimaa Khalil, maelezo ya Davis mwenyewe ndiyo hatimaye yaliyopelekea kutiwa kwake hatiani.

Hata hivyo, huenda huu usiwe mwisho wa sakata hilo. Baada ya hoja za kuhitimisha kesi kusomwa, kiongozi huyo wa zamani wa genge la uhalifu aliambia mahakama kuwa atakata rufaa.

1788240881104.png
 
Hata kama amehukumiwa, jamaa amesema atakata rufaa. Hii ina maana kwamba hii kesi bado itazua headlines nyingine mbeleni na huenda tukasikia mapya, ingawa itakuwa ngumu sana kwake kuchomoka kutokana na yeye mwenyewe kujifunga kwa maneno yake.
 
Baada ya takriban miaka 30 ya sintofahamu kuhusu kifo cha rapa maarufu Tupac Shakur, kiongozi wa zamani wa kundi la “South Side Compton Crips”, Duane “Keffe D.” Davis, amepatikana na hatia ya mauaji yake.

Kifo cha Tupac mwaka 1996 katika shambulio la risasi lililofanywa na watu waliokuwa ndani ya gari kinasalia kuwa moja ya mafumbo makubwa katika utamaduni maarufu; kukiwa na nadharia nyingi zisizo na idadi lakini bila kukamatwa kwa mtu yeyote hadi mwaka 2023, wakati Davis alipofunguliwa mashtaka ya mauaji bila kutarajiwa.

Katika wiki za hivi karibuni, kesi hiyo inayoendelea Las Vegas imejikita katika kitabu cha kumbukumbu alichochapisha Davis mwaka 2019, ambamo aliandika kuwa yeye ndiye aliyetoa silaha iliyotumika kumuua Tupac.

Davis na wakili wake walidai kuwa hayo yalikuwa ni hadithi za kubuni na majigambo yaliyolenga kuuza vitabu, lakini baraza la wazee wa mahakama lilichukua saa chache tu kufikia uamuzi wa kumtia hatiani.

Kama anavyoandika mwandishi wa BBC News anayeshughulikia eneo la Amerika Kaskazini, Shaimaa Khalil, maelezo ya Davis mwenyewe ndiyo hatimaye yaliyopelekea kutiwa kwake hatiani.

Hata hivyo, huenda huu usiwe mwisho wa sakata hilo. Baada ya hoja za kuhitimisha kesi kusomwa, kiongozi huyo wa zamani wa genge la uhalifu aliambia mahakama kuwa atakata rufaa.

View attachment 3661001
Halafu,unakumbuka ulitoa taarifa kwamba John Mnyika kajiuzulu uongozi CHADEMA wewe@missHalima?
 
Mtu atunge hadithi kuwa alihusika kwenye tukio fulani baya hataachwa atakamatwa tu. Mfano mtu aibuke na kusema yeye ndiye aliyepanga jaribio la kumuua Lissu na amewapoteza wengi tu, watamshukia kama mwewe
 
Damu ya mtu haijawahi kumuacha mtu salama....
 
Baada ya miaka 30,hatimaye keefs d David akutwa na hatia katika mauaji ya Tupac Shakur!...

Hakupiga risasi au kuumiza lakini alipanga,na ikatekelezwa!...

Kila jambo huanza na mpango kazi kwanza kabla ya utekelezaji.
1000013144.jpg
 
Back
Top Bottom