Nilipeleka mgonjwa KCMC tukakutana na wanafunzi wenye umri sawa na wajukuu wake. Alianza mmoja akaongea naye kirefu sana na kumpimapima mara mbilimbili kijana akaandika notes kurasa zaidi ya tano! Mimi nilidhani hizo ni sehemu ya matibabu kumbe ni notes zake za kujisomea! Akaja kijana mwingine makamo yaleyale akarudia yaleyale ya mwenzie naye akajaza notes zake! Baadaye wakaja kikundi cha vijana kama 8 hivi na notebooks, yaani wote makoti meupe kama yangeyange, wanaanza kubishana kuhusu mgonjwa, mmoja akisoma kitu kwenye notes zake wanaanza kupeana upya zamu za kumtomasa tena mzee! Bahati yao mbaya walikuwa wanajadiliana kwa kiingereza kwahiyo niliwaelewa kila kitu kwamba wanabishania mambo ya kwenye kitabu, mara wanataja kuwa profesa fulani hapendi hivi anapenda vile, mgonjwa anadoda tu! Mapokezi tumekaa masaa matatu, na alipokuja daktari halisi ambaye nilimtambua kwa kitambulisho chake aliongea na mgonjwa kwa muda ambao haukuzidi dakika 10, akaandika notes kwenye headed paper ambazo hazikuzidi one page, na hakujadili chochote na wale wanafunzi! Yaliyofuata ambayo nayo ni kero tupu naona niache kwanza nitayasema baadaye. Lakini mtu asinidanganye kwamba kulikuwa na wanafunzi wanaofundishwa chochote pale, wale walimchezea mgonjwa, wakamtonesha, wakamwongezea maumivu, wakaondoka zao na notes zao!