Kero chuo kikuu cha tiba KCMC-tumaini university | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero chuo kikuu cha tiba KCMC-tumaini university

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kcmc-students, Sep 9, 2010.

 1. k

  kcmc-students Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kero katika chuo kikuu cha tumaini kcmc


  TASWIRA

  Kilimanjaro christian medical college- ni chuo kikuu cha Tiba na huduma afya ya jamii,ikiwa ni moja ya vyuo vilivyopo chini ya vyuo vikuu vya tumaini hapa nchini.

  Katika sera ya serikali ya Tanganyika iwapo mwaka wa 1960’s.ilitwa mkutano ujumuishayo mashirika ya dini hasa yale ya kikristo katika uchangiaji katika kuboresha na kuanzisha hospitali za rufaa na utoaji mafunzo katika sekta ya afya.
  Chini ya uongozi wa makanisa ya kilutheri na anglikani kupitia shirika lao la good Samaritan foundation GSF na washirika wake wa nje ipatapo mwezi march 1971 walianzisha KCMC ambayo ilichukuliwa na serikali muda mfupi baadae,na kurejeshwa baadae katika huduma chini ya mfuko wa GSF mwaka 1992.ikiwa ni katika sera ya sere kali ya kuwezesha mashirika binafsi kutoa elimu ya juu na huduma za jamii.na ilipofikia mwaka 1993 bodi kuu ya ELCT edificial uamuzi wa kuanzisha chuo kikuu cha TUMAINI ,ikijumuisha chuo kikuu cha KCM-COLLEGE kitoacho mafunzo ya tiba. Katika vitengo zifuatazo:-
  Shahada ya udaktari
  Shahada ya uuguzi
  Shahada ya viungo bandia.

  Utangulizi;
  Pamoja na sera nzuri ya wizara ikiwa chini ya serikali yetu tukufu ya Tanzania,katika kukimbiza gurudumu la uboreshwaji katika kutoa huduma za afya katika nchi yetu hasa katika kuongeza idadi ya watoa huduma katika vituo vya afya hapa nchini.

  MAPUNGUFU KATIKA CHUO KIKUU CHA TIBA KCM-COLLEGE;-

  Pamoja na sera ya kupanua utoaji wa elimu katika chuo hichi cha tiba ikiwa ni pamoja na kuongeza kozi na idadi ya wanafunzi maradufu katika mazingira yaleyale bila ya maboresho yeyote,ikiwemo na uhaba wa madarasa na yasiyokidhi idadi,uhaba ya wakufunzi, vifaa vichache na vichakavu vya kujifunzia,kotukuwa na maktaba ya chuo.ulipwaji duni wa wakufunzi,na upandishwaji wa ada ya chuo bila kuzingatia mkataba ,usiri uliopo kati ya chuo na wizara ya elimu na mafunzo(MEVT).

  -Malalamiko kutoka kwa wanafunzi;-

  TAALUMA:­-
  Utoaji wa huduma za kitaaluma umekuwa ukizorota siku hadi siku,ikiwa ni katakana na kotukuwa na wakufunzi wa kutosha na kujitegemea kakita kila idara,hivyo tukiwa tegemezi chini ya waajiriwa wa muda mfupi na mrefu ambao wanahudumia wagonjwa hosptalini.

  Hivyo tukiwa hatuna uhakika wa walimu kuja darasani kwa utaratibu ulioakinishwa katika mfumo wa ratiba ambazo zimekuwa nikawaida kubadilika kila mara bila kamala madhara yanayoweza kujitokeza.

  Hivyo walimu wamekuwa ni watu wa kutafutwa na wanafunzi ikiwemo viongozi wa kujitolea wa madarasa iliwaje wafundishe,ambao wakati mwengine imekuwa ni vigumu kupatikana na engine wakiwa wakikataa katakana na kutotaarifiwa na uongozi husika wa idara.

  Wakufunzi wengi hasa wale katika masomo ya basic science yatolewayo mwaka wa kwanza na wa pili yamekuwa yakfundishwa na wanafunzi wa masters wa hapo chuoni wakiwemo hasa wale wa mwaka wa kwanza kama tutor,ambao mara nyingi wamekuwa wakikiri hawavifahamu vizuri na kwa undani vitu wavifundishavyo hivyo wakitumia slides chache za powerpoint ambazo unakuta ziliandaliwa zamani mno na nyingine wakidownload kwenye internet kama wikipedia ambazo zimekuwa na mapungufu makubwa.

  Wakufunzi hawa wamekuwa wakitumiwa mara nyingi na chuo kwa kigezo cha kuwa ni part yao ya field ila wakati huohuo wakiwa kwenye ratiba za wodini pia,na mara nyingi wamekuwa wakilalamika hawapewi kitu chochote kama bakhsishi au kifuta jasho kutoka chuoni kama sehemu ya tution fees.

  Pia kumekuwa na udanganyifu ambao umekua ukijirudia mara nyingi katika uanishaji ya wakuu wa idara chini ya chuo ikiwa baadhi ya idara kotukuwa na mhusika peyote,

  IDARA YA PATHOLOGY:
  Kumekuwa na ugumu wa muda mrefu wa kotuku na walimu katika idara hii huku wanafunzi wamekuwa wakilazimika kujisomea wenyewe bila mwongozo.

  Na mara wanafunzi wanapoahitaji ufumbuzi kutoka katika utata huu wamekuwa wakipewa ahadi zisizokuwa na mafanikio wala kutekelezeka, baada ya wanafunzi wa mwaka wa pili mwaka jana kuitisha mgomo,basi chuo kililazimika kumleta mwalimu ambaye anafundisha chuo kikuu cha SUA,ambaye likuta ni vigumu kumuelewa hasa katika ufundishaji wake na akiwapa mifano ya mifugo kama ngombe,mbuzi na n.k.

  Pamoja kotuku na vigezo,hupewa muda wa wiki mbili kufundisha vipindi vya mwaka mzima vinavyohitaji sii chini ya masaa 84 ambapo vinafundishwa kwa kwa masaa 16 tu yani vipndi nane tuu.
  Ipo wakati ambapo tulipata habari ya kuwa hospitali ya kcmc na chuo cha kcm college kupata wakufunzi watatu wa pathology kutoka nchi nje ambao wamefunzu masomo hayo na kushindwa Kuelewanaa gharama ikisadikika kuwa kutoka katika hao wapo wachache ambao walikuwa very cheap.
  Ila katakana na dhamiraa ya ulaji ya wachache,tutaendelea kuteseka.

  IDARA YA ANATOMY AND PHYSIOLOGY:
  Idara hii imekuwa ikisusua ikiwa haina waliimu wakutosha na kotuku na mkuu wa kitengo hivyo chuo kutumia madaktari wa hospitali kineme wanafunzi wa shahada za uzamili yani masters ambao wengi wao wakiwa na ugumu wa kukumbuka kwa usahihi vitu alivyopitia miaka sita ama saba iliyopita wakati akiwa chuoni.

  Pili vifaa vya vielekezii vimekuwa ni haba na vibovu na visivyojitosheleza hivyo vimekuwa kikwazo kwa wanafunzi kujifunzia.
  Udogo wa chumba cha anatomia kijulikanacho kama kadava kimekuwa kisichokidhi idadi ya wanafunzi 120 kwa wakati mmoja kikiwa na miili michache na mfumo duni wa kusafisha hewa yani ventillation kitu ambacho kimepelekea wakati mwingine wanafunzi kuangukaa katakana na ukali wa dawa ya kuifadhia miili iulikanayo kama fomalin,
  Pia nguo za kufanyia majaribio zimekuwa ni chafu wakati mwingine zikiwa hazijafuliwa katakana na mfumo duni wa utoaji pesa ili zifuliwe
  ,kuwa idara ya hospitali kama sehemu ya wafanyakazi kujikumbushia lakini kutokana chuo kotukuwa na chake imekilazimu kutumia sehemu hiyo hiyo bila ya kuweka walimu waelekezii wa kumsadia mwanafunzi wakimwachia mtunzaji wa miiili hapo kuwaelekeza wanafunzi ,mtu ambaye ni mzee wa muda mrefu na asiyekidhi kiwango ikiwa wakati mwengine kuwapotosha wanafunzi.

  Jee kwa kuhoji tu utaratibu huu wenye mfumo duni na usiojali afya ya mtu na udanganyifu kwa kutotumia ada ya mwanafunzi husika katika kumwezesha na kumboreshea mazingira ya kupata taaluma yake inadhihirisha kuwa ubadhirifu wa wazi wazi wa pesa walipazo watoto wa kulima wenye nia njema na taifa lao bila ya kujaliwa na watu wachache wenye maslahi binafsi.

  VIFAA SAIDIZI KATIKA TIBA
  Kumekuwa na utata na uozo katika upatikanaji na ulipaji katika vifaa husika, wanafunzi wamekuwa wakitozwa 300,000/= hadi 800,000/= kutokana na prospectus mpya kwa kila mwaka ikiwa ni gharama ya vifaa kama stothoscope na BP machine na patella hammer au kigongeo ambavyo mwanafunzi hupewa mara moja hasa aikiwa mwaka wa tatu
  Vifaa hivi ni pungufu ya gharama iliyotajwa hapo juu,na pia viletwavyo vimekuwa havina ubora wa kutosha na pia mara nyingi wanafunzi wamekuwa wakivigomea na kuvirudisha.
  na je kwa mwaka wa kwanza na wa pili hizo fedha husika zinaelekea wapi ikiwa mwanafunzi masomo yake hayahitaji vifaa hivyo,tusemeje kwa hapo???

  Wanafunzi tumekuwaa mara nyingi ni kwanini Tumekuwaa tunadaiwa fedha hizi za special faculty requirement kama sehemu ya ada bila ya kuwa na vigezo,hivyo basi fika itakuwa ni maslahi ya watu wachache na wala si dhamira ya tumaini university.
  Hivyo basi ingekuwa ni bora kwa kila mwanafunzi awe na uhuru wa kujiunulia vifaa vyake mwenyewe bora na vyenye viwango.kitu ambacho kitaweka imani ya mwanafunzi juu ya chuo.


  MAFUNZO NJE YA CHUO
  Kumekuwa na uonevu bila ya kujali haki za kimsingii za kiutu pale mafunzo husika yanapomlazimu mwanafunzi kutembea umbali mrefu kwaa kwa miguu na kuwashidilia wanafunzi 120 na ziada kwenye coaster moja na hiace moja,iliwagawanywe katika vijiji husika vya hapa mkoani. Je hii ni sawa????
  Pili baadhi ya wanafunzi wakiwa huko vijijinii hukosa mtu mwelekezi wa kuwaongoza na kuishia kuhadaa bila mpangilio huku bodi ya mikopo ikitoa fedha 400,000 kwa mwaka kwa ajili ya kumgharimia mwanafunzi mmoja tena ni kwa mwezi moja.
  Jee pesa hizi kwa watu 100 zipatazo 40,000,000.ndio bajeti na allowance ya madereva wawili wa coaster ya chuo na hiace ya mtu binafsikwa trip 30 kwa mwaka.ambazo mtu huweza kutumia 1200 kwa kwenda na kurudi akitumia usafiri binafsi??
  Je hizi pesa zinaenda wapi na kama si matumizi ya watu binafsii????

  MAKTABA
  Mpaka sasa chuo haina maktaba ya kumwezesha mwanafunzi kujisomea hivyo wanafunzi wakilazimika kujipenyeza mapaka kwenye maktaba ya hospitali ambayo ni ndogo na yenye vitabu vichache na vya zamani kidogo na kutokuwepo na huduma ya internet inayoekeweka ikiwa na komputa nane tuu ambazo tano tu ndo zinazofanya kazi kwa shida.

  Maktaba hii pamoja udogo wake pia imekuwa na wahudumu wachache tena wenye sifa na pia muda inayofunguliwa ni finyu hasa ukizingatia ugumu wa masomo yao.
  Na muda mwingine chuo kimeshindwa kuchangia chochote katika maktaba hiyo ili kuongeza ufanisi.
  Hali inayopelekea wafanyakazi kulalamika kufanyishwa kazi kwa muda mrefu bila kujaliwa maslahi yao na hivyo wakati mwingine hospitali imekuwa ikitishia kusitisha huduma hiyo kwa wanafunzi.
  Hii ni hatari kubwa kwetu…….????

  ONGEZEKO LA ADA

  Mapema mwaka huu kumekuwa na factual kuongezwa ada ya chuo kineme kitu ambacho baadae baadhi ya wanafunzi wanaopitishiwa hela zao na wafadhili kwenye akaunti ya chuo kukatwa bila ya wao kupewa taarifa,na baada ya kuja juu wachache walirudishiwa pesa zao na iliilazimu serikali ya wanafunzi kuonana na utawala husika ambao baadae mkuu wa chuo alitoa notisi ya kila mwanafunzi kutumia prospectus mpya ambayo imbibe ada mpya ambayo itaanza mwaka huu wa masomo wa 2010/2011 kwa wanafunzi wanaoendelea huku wakiacha ile ya Manzoni ikitupwa kapuni kabala ya muda kuisha .
  kwa wale wenye wafadhili kama mashirika binafsi na vitengo mbalimbali kama jeshi na n.k.watalazimika kulipa ada hiyo na kitu ambacho hueda kikawagharimu wengine kushindwaa kuilipa kutoka na bajeti ambazo zilishapitishwa mwanzoni
  vile vile wanafunzi wa mwaka wa kwanza walilazimishwa kuanza kutumia ada hiyo kitu ambacho kiliwalazimu wanafunzi wawili wa mwaka wa kwanza kushindwa kuendelea na masomo yao na kurejea nyumbani .

  Habari zinazoaminika akinukuliwa raisi wa seikali ya wanafunzi ambaye ni mjumbe kwenye bodi kuu ya maamuzi ya tumaini university ama kijulikana kama senate.
  Katika moja ya vikao vya mwaka huu walipitisha azimio la kuwataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza tuu ndo walipe ada mpya na wale wanaoendelea walipe ile ya zamani yani mkataba wa prospectus ambao walijiunga nao mara walipodahiliwa chuoni.
  Na kumekuwa na vitisho vya watu kutolewa wakati wa kufanya mtihani endapo mtu hajaclear ada yake.

  Je hii ni sawa kubatilisha maamuzi ya vikao vya senate ,ama ni janja janja ya watu wachache ambao hawana nia njema na Tumaini chuo kikuu.
  Na ongezeko hili ni kwa maboreshoo yapi yasiyoonekana ,au ndo utapeli wa kisasa wenye azma za kusadikika

  Bodi ya vyuo vikuu vya Tanzania ilishatoa mwongozo mapema ya kwamba vyuo vyote vilivyokuwa na nia ya Upandishaji wa gharama za uendeshaji vyuoni.usubiri mfumo utakaotolewa na bodi ya TCU ambao uptake ni mwongozo wa vyuo vyote hapa nchini,
  Na pia vyuo vilikumbushwa tena mapema mwaka jana baada ya chuo cha tumaini dar es salaam (TURDACO) kutangazwa kupandishwa ada kwa upande wao .tulishuhudia onyo kali kwenye vyombo vya habari ya kuwa wasiongeze ada mpaka watakapotoa mwongozo.

  Sasa je ina maana management ya Tumaini hawakuliona hili agizo,mpaka sasa ni miezi sita tuu imepita wanapandisha tena kwa KCM-COLLEGE.

  Bodi ya mikopo

  Vile vile bodi ya mikopo nayo ilishatoa waraka wa wazi kwa mwaka wa jana wa masomo 2009/2010.
  ikinukuliwa kwamba loan bodi haitawajibika kwa chuo chochote kuongeza ada ya wanafunzi,kitu ambacho vyuo vingine vikuu imeunga mkono agizo hilo na huku chuo cha Tumaini ikikiuka agizo hilo kwa ukaidi ambao tunadhani ni wale wachache wasiokuwa na uzalendo juu ya taifa lao na kuwakwamisha ndoto na ari ya watoto wa hali ya duni ambayo wako tayari kilitumikia taifa lao kwa moyo.

  Vile vile tunashindwa kujua ni mlango upi wa ukarimu ulioweza kuwasaidia wanafunzi wa grant wa chuo kikuu cha tiba na teknolojia kuwapa nyongeza ya pungufuu ya ada walipiwayo na wizaraa (MEVT)
  Huku tukishuhudia kwa chuo cha kcm college kutupiwa mbali maombi yake.
  tunaombaa bodi itusaidiee kamala ombi letu kwa mara ya pili
  Wizaraaa ya elimu na mafunzo
  Kumekuwa na usiri mkubwaa kati ya chuo na wizaraa husika juu ya mkataba unaojazwa baina ya mfaidikaji wa grant na chuo husika bila ya kuwa na unyumbulisho toka wizaraa husika.hali hii ni kama kukiuka maadili ya utekelezaji wa azma ya serikali kwa uadilifu kutoakana na kutowajibika ipasavyo baina ya pande zote mbili husika kimkataba.
  Pia wizaraa husika imekuwa ikitulipia tuition fees na kuacha kutulipia examination fees je hapa ni sawa kwela,mwanafunzi asome na asifanye mtihani je mfadhili haoni ya kuwa inaacha rasilimali watu ielimishwe bila ya kutahiniwa na kuathiri ubora na ufanisi wa watumishii wa umma kupitia kcm-colllege

  Na katakana na ongezeko hili la ada wizard imeikatalia kcm college ongezeko la ada huku ikitoa mwanya kwa wanafunzi hao kuomba msaada wa nyongeza bodi ya mkopo kama walivyofanikiwa chuo kikuu cha cha tiba na teknolojia cha IMTU,bila ya wizaraa kutoa msaada au mwongozo kwa bodi ili kusikiliza maombi ya chuo chetu,hali iliyopelekewa chuo chetu kutupiwa kapuni.
  Je hii ni sawa na haki kwa usawa.
  Na baada ya serikali ya wanafunzi kuomba mwongozo kutoka wizaranii kwa nia njema,wizaraa ilijibu kinyume ya maombi rejea ya serikali hiyo ambayo ni chombo cha haki tekelezi ya wanyonge.kwa kuomba hao waliopeleka maombi hayo wapewe onyo kali na kurejea chuoni huko awali ambako hawakupata haki yao ya kissing kufahamishwa na kupatiwa unyumbulisho kutoka kwa mfadhili wao anawalipiaje.

  Hivyo basi tunaombaa serikali yetu kupitia wizaraa iangalie swala hili nyeti kwa mara ya pili kwa jicho la huruma na umakini zaidi.

  UTAWALA
  Utawalawa kcm college umekuwa na mparaganyiko kiwi huku ukiacha utaratibu wa proffessional na kuingiza undugu na kufahamiana zaidi na hivyo wakati mwingine kuleta maamuzi mabovuu na yasiyokuwa na tija.

  Maamuzi makubwa mara nyingi yamekuwa yakitoka kwa mkuu wa chuo na vice chancellor ambaye mara nyingi amekuwa karibu na hichi chuo ukiachilia mbali vyuo vinine vya tumaini ambavyo anahitajika pia.
  Na hao wawili ndio wanajiitaa na wakilazimisha kuwa signatories wa chuo bila ya wao hata bursar ambaye wamemwajiri asiye na kukidhi vigezo na kuwa na lugha chafu,amekuwa akishindwa kufanya kazi hiyo na kulazimu vitu visimame kwa muda mpaka warejee.

  Hawa watu wamekuwa wapunjaji wa malipo kwa wakufunzi wachache waliopo,na kuhimizaa wanafunzi wa masters kufundisha ikijua haitawalipa kitu hivyo wakijua wataitumia vipi tution fees ya mwanafunzi kwa matumizi yao binafsi.

  Watu hawa pia waliweza kuchukua mfuko wa serikali ya wanafunzi na kuwaamulia pindi wakati wa hitaji endapo watawasaidia ama kutowapa chochote,huku ikikwamisha uendeshaji katika shuhuli zao husika.  Barua ya wazi toka

  Sauti ya Ukweli Kcm-College
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Noted with concern
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kasheshe.

  TCU wana changamoto kubwa kuthibiti mambo vyuoni, na hasa kuoanisha upanuzi wa vyuo kwa upande moja, na upatikanaji wa lecturers/professors na nyenzo za kufundishia kwa upande mwingine.

  Kwa ada kubwa zinazotozwa na vyuo binafsi sio sahihi vyuo hivyo vitoe wataalamu walioivishwa nusunusu.
   
 4. Sonnet

  Sonnet Senior Member

  #4
  Aug 13, 2014
  Joined: Oct 22, 2013
  Messages: 149
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Hamna chuo kikamilifu.... Hata harvard inamapungufu yake.
   
 5. geniusbaraka

  geniusbaraka JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2014
  Joined: Aug 1, 2014
  Messages: 528
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mia mia nimekupata bro
   
 6. P

  PAROKO-MAPUTO Member

  #6
  Aug 13, 2014
  Joined: Mar 28, 2014
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha majungu mkuuu jenga chako/?/
   
 7. idoyo

  idoyo JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2014
  Joined: Jan 13, 2013
  Messages: 3,040
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  usihalalishe dhambi kwa dhambi. ati vile padri kazini basi ukizini sio vibaya.
   
 8. Ngongongare

  Ngongongare Member

  #8
  Aug 13, 2014
  Joined: Jan 16, 2014
  Messages: 35
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Poleni sana
   
Loading...