KCMC na logo ya nyoka!

KCMC na logo ya nyoka!

Alama ya nyoka ina historia ndefu sana. Kihistoria hasa ilianzia pale Waisraeli walipoasi kule jangwani na Mungu akawaadhibu kwa pigo la kugongwa na nyoka. Musa alipokwenda kumwomba Mungu. Mungu alimwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba na kumwinua na kila atakayemwangalia akigongwa na nyoka atapona. Alama ya nyoka katika kipindi hiyo haikuwa na uhusiano na shetani bali Mungu alitaka Waisraeli wamwamini kwamba yeye ndiye mponyaji. Na ni kwa imani tu watu wengeweza kupona. Tunaambiwa kwamba kuna watu walitazama nyoka yule wa shaba baada ya kugongwa na nyoka na kweli walipona, hata hivyo wapo ambao hawakutazama na kwa hakika walikufa. Hii inatufundisha kwamba kupona kwetu ni kwa imani na anayeponya ni Mungu pekee. Ndiyo maana Yohana sura ya 3:14 Yesu anasema, "Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye." Logo hii ilianza kutumika katika mahospitali ya uingereza wakati ule wa tauni. Logo hii iliwapa watu imani kwamba aponyae ni Mungu kama vile alivyofanya kwa Waisraeli kule jangwani. Hivyo ndugu yangu usiwe na wasi wasi, nyoka aliyeko kwenye logo hana uhusiano na mashetani bali ni nembo ya uponyaji kutoka kwa Mungu.
Kwa kuwa shetani alimtumia nyoka kumrubuni eva ina maana kuanzia hapo nyoka akanasibishwa shetani ndugu rejea biblia
 
Back
Top Bottom