MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 710
Licha ya ukweli kwamba kuna kada mbili za wahudumu kwenye hospitali ya KCMC, ambayo ni wauguzi (Nurses and Trainee Nurses) ambao hutofautishwa kwa rangi za sare zao (Nyeupe kwa Nurses na Hudhurungi kwa Trainee Nurses), na Wahudumu (Service Ladies) ambao hutambulishwa kwa sare zao za kijani, ni kada hii ya Wahudumu ambao wengi wao ni wanawake ambao japokuwa umri umekwenda, bado wana nguvu za kufanya kazi. Haitakuwa busara kuacha kuzungumzia suala la kiwango cha elimu cha kada hii ya Wahudumu, kwani ndicho kiini cha mgogoro ambao unatishia kuiweka hospitali hii maarufu ya rufaa katika mlolongo wa kesi pindi ambapo wananchi, wateja wa hospitali hii, watakapoamka na kuanza kudai haki zao. Si nia ya waraka huu kuzungumzia suala la kiwango cha tiba kwenye hospitali hii, kwani nacho kina utata ambao utazungumziwa katika wakati mwingine.
Tukirejea kwenye suala la kada ya Wahudumu, ambao wanaelekea kuwaambukiza kada la Wauguzi baadhi ya tabia zao, kada hili la Wahudumu limeelekezewa tuhuma mbali mbali, zikiwemo:
1. Kutokuwa na kauli safi au ya upole kwa wagonjwa na/au wasaidizi wao
2. Kuchelewa au kukataa kuwahudumia wagonjwa na/au wasaidizi wa wagonjwa pindi ambapo Wauguzi wanapokuwa mbali ilhali wao wako wodini wakifanya usafi
3. Kutumia lugha ya dharau na kali wakiwagombeza wagonjwa na wasimamizi wao, wakilalamikia hali ya wodi na/au vyoo kuwa chafu, huku wakijua kwamba hospitali hii hutembelewa na zaidi ya wageni 2000 kwa siku wanaofika kuwaona wagonjwa wao na idadi hii hufikia zaidi ya 5000 kwa siku wakati wa mwisho wa wiki
4. Katazo la wagonjwa na/au wasimamizi wao kutochaji simu zao wakati wa mchana, bila kuzingatia kwamba mawasiliano ni suala la lazima na wala si anasa
Uongozi wa KCMC unaombwa kujibu haraka tuhuma hizi kama ifuatavyo:
1. Tabia ya Wahudumu kukosa kauli safi na/au ya upole kwa wagonjwa na wasimamizi wao inaweza kutafsiriwa kwa namna mbali mbali. Mosi ni kwamba pengine hospitali hii si mahala pazuri kama inavyosifiwa kwani Wahudumu na Wauguzi ni kada ambazo wagonjwa na/au wasimamizi wao huwa ya kwanza kukutana nayo kabla hata ya kuwaona madaktari. Pili, kutokana na hili, upo uwezekano kwa wagonjwa kuingiwa na hofu kwmba pengine hawatapona, na kupata msongo wa mawazo ambao huchangia kutopona kwao kwa muda mrefu. Hali ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa upasuaji kwani mara nyingi hakuna maandalizi yoyote yale ya kisaikolojia kabla na baada ya upasuaji, kazi ambayo huachiwa wauguzi, ndugu na wasimamizi.
2. Wahudumu au wauguzi wanapochelewa au wanapokataa kutoa msaada kwa wagonjwa, tena kwa mambo ambayo ni madogo na ambayo yako ndani ya uwezo wao, kwa kauli za "Subiri nakuja huoni niko bize?", "Hiyo si kazi yangu, mwambie nesi," na hii ya mwisho "Kwani hujamwona daktari wako?" ni kauli ambazo zinawachefua wagonjwa kiasi ambapo wanajenga chuki na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Wauguzi na/au Wahudumu, jambo ambalo linachangia wagonjwa kuathirika zaidi haswa pale ambapo wanahitaji zaidi msaada kutoka kwa kada mojawapo kati ya hizi.
3. Suala hili ni tata, kwani kuwadharau wagonjwa na kuwaita wachafu haswa baada ya wageni kuondoka, au wakati wa usiku ambapo watu wengi huwa wamelala ni jambo la uonevu mkubwa. Uongozi unashauriwa kuajiri watu maalum watakaokuwa wanafanya usafi wa vyoo, na/au kuwalipisha wageni gharama ndogo wakati wanapotaka huduma hiyo ili kupata fedha za kuhahikisha kwamba vyoo hivyo vinakuwa visafi pamoja na kuwalipa wanaosimamia usafi. Lakini hili la Wahudumu kuwavaa wagonjwa kila asubuhi kwa shutuma za kuwa wachafu halipaswi kupuuziwa hata kidogo.
4. Haiyumkini kudhihirika kwamba suala la mawasiliano hivi sasa si la anasa tena baada ya serikali kubaini kwamba idadi ya watumiaji wa simu waliosajiliwa kwa mujibu wa sheria sasa imefikia milioni 28. Hii si idadi ndogo hata kidogo.
Kitendo cha kuwazuia wagonjwa na wasimamizi wao kuchaji simu zao wakati wa mchana ni kero kwani inaweza kutokea dharura wakati wa mchana, ambapo mgonjwa anaweza kuzidiwa na simu yake kutokuwa na chaji, kwa hiyo kwa kuwa wakati huo ndugu wanakuwa hawapo, wasimamizi wachache waliopo hushindwa kutoa msaada wa kuwasiliana na ndugu wa mgonjwa. Inawezekana kabisa kwamba namba ya simu ya ndugu wa mgonjwa kuwa imehifadhiwa kwenye simu yenyewe badala ya simcard, jambo ambalo huleta utata zaidi. Katika hali kama hii, hospitali yaweza kupelekwa mahakamani na kudaiwa fidia kwa madai kadhaa, yakiwemo kuwajibika kwa mwajiri kutokana na makosa ya kiutendaji ya mwajiriwa (Vicarious Liability), uzembe wa makusudi (Criminal Negligence) na kuua kwa makosa (Wrongful Death).
Tukiweka wastani wa kati ya Shs. 200 na 300 milioni, hospitali yaweza kujikuta ikidaiwa fidia ya Shs. 600 milioni kwa kosa hili moja la katazo la kuchaji simu wakati wa mchana.
Haiyumkini vifaa vya kuchajia simu huubadilisha mfumo wa umeme wa Mkondo Geugeu kwenda Mkondo Mmoja (alternating to direct current), hakuna ambaye anaweza kudai kwamba gharama za umeme zinaweza kupanda kwa matumizi ya kuchaji simu, kama hicho ni kigezo cha zuio hilo. Kama mojawapo ya sababu za katazo hilo ni usalama, msimamizi wa mgonjwa anaweza kushauriwa kumsaidia mgonjwa kuchaji simu yake wakati ambapo hakuna wageni, asubuhi na mchana baada ya kifungua kinywa na chakula cha mchana.
Wagonjwa na wasimamizi wa wagonjwa waliohojiwa na mwandishi wa makala haya wameelezea kwa hisia kali kwamba huenda hospitali hii haina sifa zinazotangazwa huko nje, na huenda wagonjwa watakaozidi kuelezea manyanyaso wanayoyapata wakiwa wodini watachangia kupungua kwa idadi ya wagonjwa watakaokuwa wakienda kutibiwa hospitalini hapo, na kusababisha hospitali hiyo kuchukiwa na watu wengi, haswa ndugu wa wagonjwa.
Wagonjwa hao wamewasifia madaktari wanaowajali na kuhakikisha wanapona. Lakini wamesema wapo madaktari wavivu ambao wanaona uamuzi wa kuondoa baadhi ya viungo vya wagonjwa kama vile miguu au mikono, kabla ya kuhakikisha kwa kina kwamba viungo hivyo havitibiki, ni uvivu wa kufikiria au kutafuta njia nyepesi zaidi.
Wadau katika sekta ya afya waliohojiwa wamesema kumekuwa na ongezeko la wimbi la wagonjwa wa kisukari ambao wengi wao wamepoteza viungo vyao na kupata athari mbaya zaidi, hatimaye wakipoteza maisha yao pia.
"Binafsi sidhani kama kumkata mgonjwa wa kisukari mguu wake ni kumsaidia kwani hata baada ya hapo ugonjwa uko pale pale," alisema mdau mmoja.
"Kuna tofauti kubwa ya mtazamo wa tiba ya ugonjwa wa kisukari kati ya madokta wanaofanya kazi kwenye hospitali binafsi na za umma. Wale wa za umma wanaona kukata miguu ni kama vile kupata vikombe vya ushindi lakini wale wa za binafsi wanaona ushindi kwao ni pale ambapo wanamruhusu mgonjwa arudi nyumbani akiwa na miguu yake yote miwili," aliongeza.
Aidha, wagonjwa hao wa KCMC wamewasifia Wauguzi kwa kazi yao nzuri huku wakiwatahadharisha kutoiga tabia za Wahudumu. Wakitoa onyo kali kwa Wahudumu wamesema waache tabia zao mbaya za kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima zao.
"Hata mbwa wako anayekulinda ukimtesa sana, iko siku atakuuma na kukimbia. Mhudumu hana haki ya kuingia wodini na kutuamrisha tuzime taa huku kukiwa na mwanga hafifu bila kwanza kutusalimia kisha kuuliza kwa adabu sababu ya taa kuwashwa. Sisi ni watu na sio mbuzi. Tumechoka kufokewa," alisema mgonjwa mmoja wodini humo.
Kwa ujumla wao wagonjwa wameutaka uongozi wa hospitali hiyo kuzifanyia kazi mara moja tuhuma hizo pamoja na kutoa ufafanuzi kwenye vyombo vya habari.
Mwandishi wa habari hizi ambaye amekuwa akifuatilia tuhuma hizi kwa muda mrefu akitumia mbinu mbali mbali za kiuchunguzi alihakikishiwa na wagonjwa hao kutoutafuta uongozi wa hospitali kwani wao wana akili timamu na wanajua walisemalo.