Kazi zimekua ngumu sana

Habari wakuu?
Ni kijana wa kiume mwenyewe umri usiozidi miaka 27

Nimemaliza degree katika maswala ya kodi mwaka 2014

Nilipata vikazi lakini vya mkataba(contract job) ambazo ndio nilikua nafanya up to this time ambapo mkataba umeisha na hakuna dalili za kuongezewa

Aisee nahitaji mtu yoyote mwenyewe connection hapa Dar es salaam angalau hata nipate pa kujishikiza

Siangalii malipo wakuu swala ninalotaka ni kupata sehemu yakwenda tu asubuhi mana Najua ukiwa na sehemu takutana na watu na tapata hata connection zingine

Sichagui kazi ila ni mfanya kazi mzuri a ia bidii ya kutosha

Naomba kuwasilisha wakuu huku nikihitaji msaada zaidi hata wa mawazo

Mkuu jaribu kuomba kazi ya kufundisha pale chuo cha kodi Pale mwenge
 
Nimemaliza ifm bachelor of taxation

Kazi za Kodi nilizowahi kuzifanya ni kama
Kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu elimu ya kodi
Kutengeneza tax returns
Kufanya assessment na zinginezo

Nimeishi mikoa kama Dodoma,singida,Mbeya,Tabora na Dar es salaam ambapo ndio mwenyeji zaidi

Mahitaji ni kwanza kumudu at least garama za maisha na kufikia malengo ya kimaendeleo lakini pia kujiendeleza zaidi katika nyanja ya maswala ya kodi

Na ningeshukuru ungeniruhusu nije PM ili turlewane zaidi Mkuu!
Hii degree ni shida sana, Kuna ndugu yangu alitafuta kazi sana akaishia uteller bank, lakini maisha yanaenda ivo ivo.
 
Back
Top Bottom