SoC03 Kazi za mitaji chini ya milioni 1, na mtu yeyote anaweza kufanya

Stories of Change - 2023 Competition

gaspern gaspal

New Member
May 12, 2023
2
1
Kazi ni nini?
(Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu).
Kazi ni utumiaji wa nguvu,juhudi, maarifa katika jambo au jitihada, bidii, utendaji.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka na wimbi kubwa la tatizo la kukosa nafasi za kufanya kazi. Lakini tatizo hili Kumekuwa likilalamikiwa sana na vijana hasa waliomaliza masomo ya vyuo. Sasa Mimi mwenzenu nimewaandalia baadhi ya kazi ambazo mtu yeyote anaweza kufanya hata kama hujawahi kuifanya au hana taaluma hiyo. Kikubwa unacho takiwa kuwa nacho ubunifu, kuwekeza na kujitoa afu kutoa muda wako katika kazi hiyo. Kwani wanasema hata dola ya rumi haikujengwa siku moja. Kwaio unachatakiwa ni kijipa muda huku ukiwa unafanya kazi kwa bidii.

1.KUTENGENEZA BUSTANI
Huduma hii ya kutengeneza BUSTANI ni moja ya huduma iliyo ibuka katika miaka ya hivi karibuni baada ya kukua kwa biashara ya Nyumba kama vile Nyumba za kulala wageni, Migahawa, Nyumba za kupumzikia na zinginezo. Huduma hii inahusisha kupanda mimea tofauti tofauti yenye rangi tofauti tofauti ambayo kwa pamoja ikiewekwa katika mpangilio maalumu huleta mvuto fulani. Mimea hiyo Inaweza pia ikawa inatoa harufu fulani nzuri ambayo itakua inawavutia watu walio karibu nayo.

Kijana mwenzangu unaweza ukafanya huduma hii kwa kuanzia na mtaji wowote ulionao kwani kwa sehemu kubwa ya hii huduma kufanikisha, gharama huwa zinakua za mteja. Wewe kijana unatakiwa uwe mtaji kidogo sana. Pia ukiwa na simu janja itakusaidia zaidi katika kutafuta mitandao sehemu zingine wenzio wametengenezaje na kutumia kama rejea yako.

Na malipo ya kutengeneza BUSTANI moja huwa tegemea na eneo ulilopo na uzoefu wako katika utengenezaji wa BUSTANI. Mara nyingi huwa 10%-25% ya gharama ya BUSTANI inayotengenezwa.
Hapa baadhi ya picha za BUSTANI

Screenshot_20230626-155242.jpg

Picha ya 1. BUSTANI
Chanzo,

2. BIASHARA ZA MTANDAONI NA MITANDAO YA KIJAMII
Katika nyakati za leo, ulimwengu upo kiganjani kuna watu wengi wanaotumia mitandao katika shughuli zao. Moja ya shughuli hizo ni kuuza na kununua bidhaa mitandaoni. Sasa kama kijana una biashara au huduma yeyote ile unaweza ukawafikia wateja wengi na wa sehemu kubwa na tofauti tofauti.

Kwa mfano wewe ni fundi wa talazo unaweza ukawa una kurasa wako kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, Twitter na zingnezo kujitanagaza. Na ukawafikia wateja wengi zaidi. Kuliko ukiwa unakaa tu mtaani kwenu ukisubiri majirani, marafiki na ndugu zako wakupe kazi. Biashara za mtandaoni zitakusaidia ukutane na wateja wapya kila siku. Unaweza ukajitangaza na kuwafikia wateja wengi kwa ketengenenza tangazo la biashara na kulilipia kupitia mfumo maalum ambao unaruhusu kutengeneza tangazo, kama META kwa Facebook na Instagram, na google ads kwa you tube na app za google.

Hivyo hivyo kijana mwenzangu kama wewe ni fundi bomba, mfugaji, mkulima, kujenga, siku, muuzaji wa siku, pikipiki yaani unafanya kazi yeyote unaweza ukatengeneza tangazo la biashara na ukapata wateja wengi na ukapata kipato cha kukuzi mahitaji yako ya kila siku.

Unachatakiwa kuwa nacho simujanja au kompyuta na hela kidogo tu hata TZS 50,000 inatosha kuanzisha biashara yako mtandaoni na kwenye mitandao ya kijamii.

Screenshot_20230623-220551.jpg

Picha ya 2. Tangazo la kijana fundi TV

3.KUTENGENEZA MWANASESERE
MWANASESERE ni vitu wanavyochezea watoto wadogo. Vitu hivyo vinaweza kuwa mfano wa kitu fulani kama wanyama, maumbo fulani kama vile nyumba, gari nakadhalika. Vinaweza kuwa vinatoa sauti au visitoe pia vinaweza vikawa vya kuendesha au la.

Sasa kijana mwenzangu kama wewe unaweza kubuni unaweza ukawa unatengeneza na kuviuza ukapata kipato chako cha kujikimu na maisha yako kila siku. Ikizingatiwa malighafi mengi ya kutengeneza MWANASESERE huwa na vitu vilivyokwisha tumika na vimetupwa. Na hivyo ukawa huna haja ya kuwa mtaji mkubwa sana wa kuanza nao.

Kwa mfano moja ya malighafi ni makopo ya mafuta yalioisha, makopo ya maji, kanda mbili, nguo zilizo chakaa, mipira, waya za umeme nakadhalika.

Hala chini nimekuwekea baadhi ya picha za mwanasesere


Video ya 1. watoto wakendesha mwanasesere

4. KUTENGENEZA SABUNI NA MAFUTA
Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa sabuni na mafuta katika jamii zetu za sasa. Na kufanya kuwe na soko kubwa la sabuni na mafuta.Kwa upande wa sabuni hasa za maji zimekuwa zikihitajika katika usafi wa choo ambao unafanywa kila siku na kila nyumba na hivyo kufanya kuwe na uhitaji mkubwa wa sabuni.

Kutengeneza sabuni ya maji hakuitaji mtaji mkubwa sana kwani huweza kutengeneza katika mazingira ya kawaida kabisa.

Sasa vijana wenzangu tuitumie hii fursa na tuweze kupata kipato ambacho kitaweza kututoa katika wimbi hili la umasikini na utegemezi kwa wazazi.

Screenshot_20230626-150521.jpg

Picha ya 3. Sabuni za maji tayari kwenda sokoni.
Chanzo,

5. KUPAMBA WASANII
Msanii ni mtu kwenye uwezo wa kuchora, kuchonga, kutia nakshi au mwenye ufundi wa kutunga na kutoa mawazo yake kama vile kwa ushairi,hadithi, tamthilia nakadhalika(kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili).

Na kazi ya msanii inaitwa sanaa. Katika miaka hii kazi za wasanii zimekuwa nyingi na wasanii wamekuwa wakiwekeza sana katika sanaa zao. Hivyo basi na kufanya kazi moja ya msanii unaweza ikahusisha watu wengi ili kuikamilisha. Watu hao water wamekuwa wakiaajiliwa na msanii.

Kwa msanii anaajiri mtu wa kumpamba mavazi yake na wahusika wote wa kazi yake. Mapambo hayo yanakua ni pengine mitindo wa nywele zao, michoro ya kwenye miili yao, namna ya kuongea kwaio katika kazi yake, kutembea, kula na vitu vingene vingi ambavyo vitafanyika Katika kazi ya msanii.

Na hivyo kama kijana ambaye unauwezo kumpamba wasanii unaweza ukanza kufanya hiyo kazi, na kujipatia kipato. Unaweza ukaanza kuwapamba wasanii wadogo wadogo ambao hawana majina, kadiri unavyofanya hiyo kazi ndivyo utakavyo kuwa na watu wengi ambao watahitaji huduma yako. Pia unaweza ukatumia mitandao kujitanagaza na watu wakajua huduma yako.


6. KUWA MWALIMU WA MAZOEZI YA VIUNGO
Mazoezi ya viungo ni aina ya mazoezi yanayofanywa kwaajili ya kuimarisha viungo vya mwili kama vile vya mwenye mikono, miguu, mgongo nakadhalika. Na katika maisha yetu ya sasa kutokana na kubadilika kwa mitindo ya maisha Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wenye uhitaji wa huduma hii ya mazoezi ya viungo vya mwili.

Sasa kijana mwenzangu unaweza ukujifunza aina za mazoezi na ukawa mwalimu mzuri ili uje ufungue eneo lako la kusimamia na kufundisha watu wengine. Kwa sababu siku hizi wapo watu wengi wanahitaji kufanya mazoezi hayo. Hii ni kwa sababu wengi wanashinda kazini(ofisini) na wanaenda na kurudi kazini kwa magari hivyo na kuwafanya wahitaji muda wa kufanya mazoezi.

Katika kuanzisha huduma hii kijana hauhitaji mamilioni ya hela. Hata TZS 150,000 tu inatosha.

Na wewe ukapata kipato chako na ukajikimu na gharama za maisha. Mara nyingi ukubwa wa kipato utapata unategemea eneo ulilopo, na idadi NA aina vipindi unavyofundisha.

Screenshot_20230626-151119.jpg

Picha ya 4. Mwalimu wa mazoezi ya viungo na mwanafunzi wake.

Chanzo,

7. KUTENGENEZA FANICHA
FANICHA ni vyombo vya nyumbani vinavyotengenezwa kwa kutumia mbao kama vile viti, meza, kabati, na vinginevyo vingi. Katika maisha ya mwanadamu FANICHA zimekuwa na uhitaji mkubwa muda wote. Na kufanya kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa mafundi wa kutengeneza FANICHA. Soko lipo katika kutengeneza FANICHA mpya au kurekebisha ilio haribika.

Sasa kijana mwenzangu unaweza ukajifunza ufundi wa kutengeneza FANICHA na ukawa unajipatia kipato cha kujikimu maisha ya kila siku. Kwani kijifunza ufundi hakuhitaji gharama kubwa sana. Unaweza ukajifunza useremala katika sehemu tofauti tofauti kama ni katika vyuo vya VETA au kwa kufanya kazi na mafundi wa mda mrefu. Gharama ya kusoma VETA au kwa fundi haizidi TZS 200,000/-. Pia ufundi seremala hauna mahesabu magumu sana, kiasi kwamba kwa mtu yeyote anaweza kujifunza.

Na pia ili vifaa vya msingi havina gharama sana kwa mfano kipima urefu bei ake kuanzia TZS 25,000/-,Msumeno TZS5,000/-, Nyundo TZS 3,000/- vitu vingne huwa ni gharama za mteja kama kulanda mbao, kuchana mbao na zinginezo. Na hivyo basi kuanza kazi hii unaweza kuaianza Kwa mtaji wowote ule ulionao. Ila upataji wa wateja unategemea na eneo unalofanyia kazi, muda ulio nao toka uanze kufanya hii kazi na jitihada zako kazini.

IMG_20230625_095316_757.jpg

Picha ya 5. Dawati la fundi seremala akijiandaa kuanza kazi
IMG_20230625_095358_901.jpg

Picha ya 6. Fundi seremala akiendelea na kazi.

8. HUDUMA YA KUPAMBA NYUMBA

Huduma hii ya upambaji wa nyumba imekuwa fursa kubwa ya kibiashara katika miaka yote hasa katika miaka ya hivi karibuni, baada ya kukua Kwa biashara ya nyumba hasa nyumba za kulala wageni, za kupangisha, za kumpumzikia na hata za kuishi.

Huduma hii huhusisha kupaka rangi, kuchora michoro ya kuvutia nje au ndani ya nyumba, kupanda mimea na kupangilia taa za umeme kwa namna ya kuvutia. Kutokana kuwepo na uhitaji huo kuna fanya kuwepo na fursa ya kibiashara. Kwa vijana wenzangu tunaweza tukajiajiri katika upambaji wa nyumba na tukajipatia kipato cha kujikimu na maisha. Pia kazi hii inaweza ukafanya na mtu yeyote na wala haitaji elimu. Kazi hii inaitaji tu ubunifu wako fundi.

Malipo yake ni 10%-20% ya gharama ya upambaji wa nyumba. Na mara nyingi gharama ya upambaji nyumba hugharimu hadi TZS 5,000,000/- kwa Nyumba.
Kijana mwenzangu unaweza ukajifunza kazi hii aidha kwa mafundi au ukajifunza mwenyewe mtandaoni.

IMG_20230619_091803_260.jpg

picha ya 7. Mafundi urembo wa nyumba wakiwa kazini.

9.KUTENGENEZA BAISKELI NA PIKIPIKI
Baiskeli na pikipiki ni moja wa vyombo vya usafiri vyembe watumiaji wengi hapa nchini. Kutokana kuwa na watumiaji wengi kunafanya kuwepo na uhitaji mkubwa katika jamii zetu.

Sasa kama kijana unaweza ukatumia uhitaji huu kuwa fursa ya kujiajiri na ukapata kipato. Ingawaje kuna vijana wengi wapo katika kazi hii ya kutengeneza pikipiki na baiskeli lakini bado kuna uhitaji mkubwa wa mafundi.
Gharama za kuanzia ni ndogo, wala haizidi TZS 200,000/- . Na pia unaweza ukafumgua ofisi yako popote kwani haitaji lazima uwe na jengo.

IMG_20230625_084937_300.jpg

Picha ya 8. Mafundi baiskeli wakiwa kazini.

img_20230625_092604_006-jpg.2669361

Picha ya 9. Vifaa vya fundi baiskeli.

IMG_20230625_094638_386.jpg

Picha ya 10. Vijana mafundi pikipiki wakiwa kazini.

Kwa ujumla vijana wenzangu fursa bado zipo za kutupatia kipato cha kujikimu na maisha yetu. Na tukaacha kuwa mzigo kwa familia, jamii na hata taifa kwa ujumla. Kitu tunachotakiwa kufanya ni kuacha kukaa tu bila kazi. Tuamke tuanze safari ya matumaini hata kwa maitaji midogo midogo hii hii tulionayo. Tuanze tukiwa na matumaini makubwa ya kuwa siku moja tutafanya na sisi biashara za mitaji mikubwa.
Wanasema" utakuwa vile unawaza utakuwa"

Asante.
 

Attachments

  • IMG_20230625_092604_006.jpg
    IMG_20230625_092604_006.jpg
    649 KB · Views: 84
  • VID_20230625_094634.mp4
    1.2 MB
  • Screenshot_20230626-155242.jpg
    Screenshot_20230626-155242.jpg
    116.5 KB · Views: 22
Back
Top Bottom