Kuna kazi ambazo huwezi mpa mtu hata kama unampenda sana kama hana taaluma hiyo.
Hatuwezi kumpa Pasco wa JF ukuu wa kitengo cha upasuaji MOI kwa kufurahishwa na michango yake JF. Wala Mbwana Samatta kuwa Katibu Tawala Simiyu kwa vile ni mcheza mpira mahiri.
Nimesikia orodha ya ma DAS imetoka na wengi ni vijana watumikaji kisiasa bila utaalamu.
Kwa wanao fahamu, kazi ya DAS (Katibu Tawala Wilaya) sio ya kisiasa wala ya blabla na watendaji wa kazi hiyo walikuwa wanaandaliwa rasmi toka zamani katika chuo chetu cha Mzumbe.
Ni kazi ya kiutawala inayosimamia sheria na taratibu za utumishi ndani ya wilaya. Huyu ndio mtaalamu wa kumuongoza mtawala wa siasa (DC) asiende harijojo.
Sasa orodha iliyotoka ETI hata watu wenye weledi mdogo kama Mtela Mwampamba wamepewa u DAS sio tuu ni kichekesho bali ni matusi kwa hiyo wilaya aliyopelekwa.
DAS,RAS au Katibu mkuu wa wizara akiwa bogus ni maafa katika sehemu hiyo.
Sio wivu kama watu wenye akili nyepesi watakavyo fikiri bali tujiulize Taifa hili tunalipeleka wapi? Hakika kwa mwendo huu ndani ya miaka 3 tutakuwa watu wa migogoro itayo hitaji msaada wa nje.
Inawezekana umeleta mada kwa sababu za kiitikadi lakini nakuunga mkono kwa hoja yako kwamba baadhi ya walioteuliwa kuwa ma-DAS ni disaster...Nadhani wako wanaomchezea JPM kuhusiana na teuzi mbalimbali...DAS ni post ambayo siyo ya kisiasa kabisa, na mtu anayeteuliwa kuwa DAS ni lazima narudia ni lazima awe mtumishi aliyebobea katika utawala, utumishi na uongozi ...ni hatari kubwa tena sana kumteua mtu kuwa DAS kwa kuwa tu aligombea ubunge au alihusika kwenye kampeni...HII NI HATARI...nawafahamu baadhi walioteuliwa nimeachwa mdomo wazi...Tunaomba JPM asaidiwe siyo kumhujumu...Kwa nini umteue mtu ambaye hajui chochote kuhusu uongozi, utawala na utumishi???? Wale wanaopendekeza majina kwa teuzi mbalimbali watangulize taifa hili mbele...