Kazi ya kwanza ya Wizara mpya ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iwe ni kuruhusu Watanzania kupokea malipo kupitia Paypal

Hivi hakuna kiongozi Serikalini anayepitia hizi kilio cha wananchi kwa manufaa mapana ya Taifa? Naamini biashara ya online ikisimamiwa vyema ni fursa ya ajira kwa wananchi na chanzo cha mapato kwa serikali
Ni kweli kabisa mkuu sema serikali haijaamua kuchukulia serious hili swala. Humu jukwaani naamini tuna watendaji wakuu wengi sana wa wizara tofauti tofauti za serikali
 
Yaani hii serikali, we acha tu! Sasa si kutiana hasara huko!! Manake kwa kufanya transfer ya mafungu I bet umeingia gharama maradufu kuliko kama ingekuwa ni single transfer!!

Kazi tunayo safari hii!!
Mkuu Chige ,yaani nataka kutuma 150K US$ huko nyymbani,naambiwa hazitafika,nitachapwa na fimbo ya "money laundering".
Nimetuma 150K US$ kwa mafungu 30,ndio salama yangu.
Punguza sefuri mjomba ni US$ 150 siyo 150K ni utz huo
 
Naomba kuelimishwa: Kutuma hela kwa Paypal au Kupokea hela kwa Paypal. Kipi kinashusha thamani ya Shilingi ya Tanzania, na kipi kinaongeza thamani Shilingi ya Tanzania, ukilinganisha na dola ya Marekani?
 
Naomba kuelimishwa: Kutuma hela kwa Paypal au Kupokea hela kwa Paypal. Kipi kinashusha thamani ya Shilingi ya Tanzania, na kipi kinaongeza thamani Shilingi ya Tanzania, ukilinganisha na dola ya Marekani?
Najitahidi kukuelewa ingawaje swali lako halijakaa vizuri kwavile hakuna uhusiano wa moja kwa moja katika kushusha au kupandisha thamani ya shiling over USD!!

Hata nitajitahidi kukuelewa kwa kusema kwamba, kama PayPal TZ ingekuwa ina-receive pesa (being paid through PayPal) halafu Watanzania wakachangamkia online business kwa kuuza bidhaa mbalimbali kupitia mitandao kama eBay, Amazon, AliExpress and the like, it means wangekuwa wanalipwa in terms of USD!

Sasa kama hizi transaction zinakuwa kubwa, it means zitaingiza ndani more USD! Sasa kwavile uchumi wetu unatumia TZS, ina maana hao Sellers wa Kibongo wangelazimika ku-convert hizo USD to TZS na hivyo kutengeneza demand for TZS ambayo in turn ingepandisha au ku-stablize bei ya TZS over USD!!

Lakini kwavile our PayPal inatumika tu ku-SEND money, and assume Watanzania wangekuw wanafanya sana manunuzi mtandaoni, ina maana hapo wangekuwa wanafanya import business!! Sasa kwavile wengi wana local currency accounts, ina maana kufanya hayo manunuzi watatakiwa kufanya conversion from TZS to USD na hivyo kutengeneza Demand for USD!!

Simple Economic Principle inasema high demand of products and/or service inasababisha kupanda bei kwa bishaa husika! Na kwavile hapo kungekuwa na demand for USD, ina maana bei yake ingekuja kuwa juu, na hivyo kushusha thamani ya TZS over USD!!

Ndo maana katika hali ya kawaida, nchi ambayo inauza sana nje currency yake inakuwa strong na thamani kubwa na inayonunua sana nje inakuwa kinyume chake!!
 
Ila haya makato ya voda na tigo cjui nyie nguchiro wa Lumumba mnayaonaje????
 
Unatakiwa kwanza kuoga ukimaliza cku zako ok
 
Asante sana Chige, perfect Explanation! Watanzania tupende elimukama hizi ili tufanye maamuzi ya busara. Hatuwezi kujitenga na mfumo wa kidunia tukitaka kusonga mbele kiuchumi.
 
Naomba kuelimishwa: Kutuma hela kwa Paypal au Kupokea hela kwa Paypal. Kipi kinashusha thamani ya Shilingi ya Tanzania, na kipi kinaongeza thamani Shilingi ya Tanzania, ukilinganisha na dola ya Marekani?
kwa serikali kutoruhusu watu kupokea pesa toka paypal kunashusha thamani ya pesa sababu sisi tunakuwa watumia pesa tu za kigeni sio wapokeaji

ina maana utafute mfano dola toka vyanzo vingine ulipie bidhaa au huduma wakati wewe huingizi dola toka nje!!!

Kupokea pesa kutafanya hela yetu iongezeke thamani
 
Labda hao watawala watakuelewa maana we Ni mwanalumumba mwenzao. Badala ya kupiga hatua, nchi inarudi nyuma sabb ya sera za KIJIMA kama hii ya kuzuia PayPal. Incredible!!!
 
Swali langu ni je ni nani anatakiwa kuanzisha hiyo paypal ? ni serikali au makampuni binafsi? kuna kuna kampuni iliwahi leta maombi na ikakataliwa? kama ilikataliwa serikali ilitoa sababu gani za kukataa.
 
Sasa kama wameweza fanya hivyo kwa MPESA unafikiri watashindwa ku impose makodi makubwa huko Paypal?

Unless hela ziwe zinaishilia kwenye account ya paypal na kutolewa bank ila pia watatengeneza Tozo tu huko benki hata hio paypal iwe haina tija kwa mwenye account. Hii nchi yetu imekuwa ngumu kweli kweli.
 
Swali langu ni je ni nani anatakiwa kuanzisha hiyo paypal ? ni serikali au makampuni binafsi? kuna kuna kampuni iliwahi leta maombi na ikakataliwa? kama ilikataliwa serikali ilitoa sababu gani za kukataa.
Ni kazi ya serikali kuweka kanuni na sheria zake sawa.
 
Kama kweli hivyo ndivyo, kwa nini basi unadhani watoa maamuzi walitoa maamuzi hayo?
 
Umelijibu swali la kipi kinashusha thamani ya shilingi. Na kipi kinaongeza. Unakisia ni kwa sababu zipi za uamuzi wa kuzuia kupokea hela za paypal TZ? Na nani chanzo: Tanzania au Paypal?
 
Kwa mtazamo huo. Hata kama PayPal na payment processors wengine hawaoni potential kubwa kwa Tanzania, ni vema Serikali yetu kuwavuta waje kufungua huduma kwetu kwa kuzingatia maslahi mapana ya uchumi wa nchi na ajira kwa vijana.
Mwelekeo na hali ilivyo kwa sasa duniani uchumi kwa sehemu kubwa unahamia DIGITAL
 
Ni kweli DIGITAL business sasa hivi ndio inaongoza kwa kutoa mabilionea wanawapita hata wanaofanya biashara ya mafuta na madini

mafuta na madini hayafui dafu kwa utajiri kwa digital business
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…