Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,124
Nakumbuka kufeli kwa wanafunzi wa Sheria mwaka huu na mwaka jana na sababu zilizotolewa na shule ya sheria Dar es salaam. Naangalia inachukua muda gani vyuo vya Tanzania kuprinti cheti cha mwanafunzi aliyehitimu; naangalia inachukuliwa hatua gani kwa wasomi wazembe na wasio na maadili, naangalia ni kazi gani wasome wenye PHd waliopo vyuoni wanafanya yakuimarisha mawazo na fikra zao.
Haya yote ukiyachambua unabaini wapo madaktari na maprofesa ambao tofauti na kufundisha hana kazi nyingine amewahi kufanya. Wapo maprofesa ambao tafiti zao hazijawahi kutumika popote.
Ukifika ofisini kwa profesa pale UDSM na ukaenda ofisi ya mwalimu wa Bao Bao utabaini kwanini hawa watu wameshindwa kujikwamua. Kama profesa awezi kugharamia kutengeneza kiti na meza vya kukalia yeye anasubiri serikali imnunulie unandani ataipenda nchi yake.
Mbaya zaidi wapo maprofesa wengi ambao wamezuia watu wenye akili wasiwe maprofesa kwa sababu ya roho mbaya.
Kwa maprofesa hawa wenye kuamini kukariri na siyo kufanya kazi field tusipoamua kuwachuja tukabaki na wale ambao elimu zao zitabadilisha maisha ya wengine lazima tufeli.
Ifike mahali tuwe na wasomi ambao mwanafunzi akifeli roho inauma na anajiona kabisa hakufanya kazi yake. Tuwe na maprofesa kama wa vyuo vya wenzetu ulimwengu wa kwanza ambao wanapambana mwanafunzi asifeli na wala asiumizwe na maisha ya vyuo. Tuwe na maprofesa wenye roho nzuri kama waalimu wa private schools ambapo wanajivunia ufaulu.