Kazi na mahusiano! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi na mahusiano!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Penny, Oct 31, 2008.

 1. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Za leo wandugu wapendwa,

  Noamba kuuliza mimi na ki professional cha u saloonisist na mme wangu ni mpenzi sanaaaa wa musiki mpaka kumpelekea kutaka kwenda kuanza kuwa DJ katika kumbi za mziki kama extra ways za kujiongezea kipato. Kwa kweli hili jambo siku liafikiana nalo na nikaongeanaye kwa kumuelekeza kuwa sijambo zuri especially kwa marriade couples. Ok kwa kweli alikubaliana nami ila kwa shingo upande sana. Sasa mimi nami kwa kuwa sina kipata bado cha kunipatia pesa, niliamua kufungua kijisaloon hapahapa home. Ila problem imekuja sasa, marafiki zake wanataka niwatengeneze nywele pia! nilipomwambia kwa kweli amekuwa mkali sana na niliamua kutowatengeneza tena ili kumtii mme wangu. Sasa wana JF nilipenda kupata michango katika haya mambo je yanastahili kufanyika au la.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,407
  Likes Received: 81,439
  Trophy Points: 280
  Kwenye ndoa makubaliano ni muhimu, wewe ulikataa mwenzako asiwe DJ na hivyo na yeye ana kila haki kama mumeo kukataa wewe kuwatengeneza nywele wanaume. Kinyume cha hapo ni mwanzo wa ugomvi.
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wote mmekosea, kwa angekua Dj ingekuaje? Kwani ukitengeneza nywele inakuaje? Naona kuna kutoaminiana hapo, hamuwezi kuchungana 24/7 maisha yatakua magumu sana.
   
 4. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante bubu, ila yeye kaona kuwa langu ndo zito sana ila yeye anaweza kufanya huo u DJ. Ndo maana nikaomba nipate kuchambuliwa katika haya mambo mawili.
   
 5. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sawa nashukuri, wote tunamakosa ila la kwangu ndo linaonekana kubwa kwa kuwa nitamshikana kimwili na yule mteja. Na yeye atakuwa anashika ma system na li earphone pekee!
   
 6. M

  Mama JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Penny, usiwe na bias kwenye mahusiano. Wewe ndio ulilikoroga sasa linywe;ulimkataza akaacha usilotaka, sasa yeye akikukataza kwa nini usiache analotaka?
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hehe! Ok naelewa labda kama kuna kushikana. Labda style zangu za nywele simple sana hazina hayo madoido.
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ungeigeuza hii story ikaanza yako kwanza...kisha yake..ungepata mawazo mazuri sana..sasa ulivyo anza ndio noma...

  Anyway unaweza kaa..nae tena mkaongea..kwa upole na kwa uwazi zaidi..kuaminia kutangulie mbele katika mazungumzo..kama ni U DJ si kuna muda wa kufanya kazi bwana...huwa wanakuwa wawili...so ongea nae yeye aje saa tano na nusu.Na imergence za ghafla hazitakuwa accepted labda atake ndoa ife.

  Vivyo hivyo na wewe kama una saloon ya unisex..weka mhudumu kuongeza kipato kwenye jamii...wewe tu kila kitu...hiyo kazi ya kushika wanaume...achia mdada na wewe unakuwa overall in charge wa shughuli nzima.Saa mbili saloon imefungwa uko nyumbani.
  Unafanya kazi za nyumbani na kumuandalia mumeo hifadhi...Hapa u serious unahitajika sana...kwa kweli vinginevyo ndoa itavunjika....

  Mshikaji wangu mmoja alimfungilia saloon mkewe ubungo...baada ya mida ya kufunga kuzidi kuongezeka....kisa kuwa wateja wengi...ilibidi kufunga saloo...see that

  Best wishes
   
 9. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante Mama, ila bias ndo nini! kimombo changu ni cha juu juu mama angu weee! sio eti nimekataa nimekubali kabisa na nimesikiliza. Ila yeye ndo bado anakijiba cha roho kuwa ana right ya kufanya huo uDJ. Kwa hiyo mimi niwe wivu sina ila roho inauma mama aah (as said by wazee wa ngwasuma) au!
   
 10. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kaka nashukuru, kwa kweli hii stori ni kweli ilianza na yeye huo uDJ then ikafatia mimi ndo nikaja kufungua kasaloon home. Mchango wako ni mzuri pia ila may be kufafanua am in England not tanzania.
   
 11. M

  Mama JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Penny, namaanisha maamuzi yako katika hili yameegemea upande mmoja, yaani yako yawe kwa namna yeyote ile hata kama mwenzi wako haridhii!

  Inabidi ukubali ukweli kuwa ulivyomkataza UDJ roho ilimwuma pia, lakini alikutii kwa vile anakupenda, sasa imekuja zamu yako hutaki kujitolea kuacha kufanya analokukataza mwenzio hata kama ni lile unalolipenda, yaani mkuki achomwe nguruwe, akichomwa binadamu unauma saana.

  Uache analokukataza mwenzio au umruhusu naye afanye alipendalo. Yangu ndio hayo tu. Nakutakia kila lenye heri na mafanikio.
   
 12. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Get you penny.

  I thinks this is general....unaweza kuona nini kina apply katika mazingira ya ya UK....
  Ni kuweka mipaka ya kazi ya kila mtu ili kupata muda wa kuongea mambo mengine ya kazi na maisha...at the same time check kama kazi zote zinaingiza kipato.Ambacho ni worth..katika familia yenu....if that is the case...katika hili...Uk najua life tight kama umeweza fungua hata saloon..that is great progress...

  Best wishes
   
 13. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  penny, jee mumeo huwa anapandisha ny**e akishikwa nywele?
  inawezekana hisia zake kwenye nywele zake ndo zinamfanya
  apinge vikali kwa saloon yako kuhudumia wanaume.

  jee pingamizi lako wewe kwa udj linasababishwa na nini hasa?
  kutomuamini mumeo kutokana na mwenendo wake au kitu
  kingine?

  naamini majibu yako katika haya masuala yanaweza saidia kupata
  ufumbuzo wa tatizo lako
   
 14. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli hana hisia za nyewele. Pingamizi langu la yeye kwenda kufanya uDJ nikutokana na tabia yake fulani fulani iliyonisababishia nishtuke! maana mkitoka kwenda out kwenye party hawezi kutulia na wewe sehemu moja utamkuta mara hapa mara pale, na anapendelea zaidi kuongea na wanawake sio wanaume. Ilibidi nimkalishe tabia na kumueleza hayo anayo fanya hayanipendezi ndo hapo nikaona ameanza kubadilika kidogo. So ilipokuja issue hii ya uDJ ndo nikamwambia kwanza hana fani nayo na pili itaniweka roho juu tuu so if he wants to be with me better aachane nayo. That is why when he also told me to stop making Men hair I agreed with a clean heart.
   
 15. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimerudi tena wandugu, kwa kweli ilibidi nimuache huyu bwana aendelee na UDJ wake maana imekuwa sasa ndo chanzo cha kutotoa pesa ya matumizi akidai kuwa hio kazi ndo ilikuwa ikimuuingizia kipato pia. Ila sasa cha ajabu mwenzangu last weekend alidiriki kwenda kuperform kwenye birthday party na kuniacha kitandani naumwa na kurudi saa kumi za usiku! Na kulikuwepo na mtu alieweza kumsaidia au angemkabidhi tuu hio deal. Hivi hapo kweli kuna kujaliana kweli! Naombeni msaada maana naona sasa kama naonewa vile.
   
 16. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ....hapo pa kurudi nilisahau lingine. Iliporudi usiku nilimsikia vizuri akiingia nikajifanya sijasikia lolote akaingia kulala. Sasa asubuhi nikamuuliza kiujanja tuu alirudi saa ngapi na aliniamsha kama kawaidia yetu tulivyozoea. Akajabu eti alisema tuu nimerudi ila hakunigusa. Ilihali yeye hakusema kitu chochote mpaka alipoingia kitandani na kuanza kukoroma. Sasa hapa nimemgundua anakauongo fulani hivi. Sasa nimwambie ukweli kuhusu hilo ili ajijue?
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...saaawa, mwanzo mzuri...

  ...u-Dj ni sawa na kazi nyingine,...kama alikwenda kazini, na u-Dj mara nyingi ni usiku, jitahidi kumsamehe tu na uelewe nature ya kazi yake...

  ...powa, mwambie tu ukweli uondoe duku duku lako, lakini kumbuka mara nyingine uongo hutumika kama intention ni kunusuru mapenzi...
   
 18. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapa kwenye italic umenikuna baba, kwingine tusubirie mawazo ya wengine. Nashukuru.
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Dec 28, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Poor Penny
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   

  Attached Files:

Loading...