Mkuu Hofstede,
Kwa kweli hali ya Tabora ni mbaya sana. Ila watu hilo hawalioni. Acha wakomeshwe na labda hii itawapa uwezo wa kuanza kufikiri. Wakipata kibano cha nguvu na aje mtu awaambie kuwa kuna njia nyingine nyingi zinaweza kutumika ili wasisote namna hiyo, basi wenyewe itabidi waanze kufikiri mara mbilimbili.
Tabora kweli kunywa soda ni alama ya utajiri. Sanasana utawaona kwa baba/mama ntilie wakipata vichai kwa maandazi/vitumbua. Atakayefika kwa Mzee Kalilo pale First and Last Hotel (sijui kama bado ipo) basi huyo ni mkali. Wanaofika Tabora hotel ni Wahindi na wageni wanaotembelea mji. Wanyamwezi pale ni wakuhesabu wanaoweza kufika pale na kula.
Ninasubiri Dr. Slaa ahamie Tabora na awe anatembelea kata kwa kata ili awaweke sawa. Hii aifanye mara moja kwa mwaka na hadi kufika mwaka 2015 basi matawi kibao ya Chadema yawe yamefunguliwa huko Tabora.
Sasa kuwa na mbunge na Waziri kama alivyo Mzee wa Pekecha pekecha, si ni kashehse?