Kazi au mume......ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi au mume......ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nailyne, Sep 14, 2011.

 1. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nina best yangu ameolewa mwaka sasa, recently amepata kazi nje ya tz (UN) kwa mkataba wa miaka 2,yupo kwenye maandalizi kuondoka nchini amepewa miezi 2 ya kujiandaaa. Ameongea na mumewe kuhusiana na suala hili mumewe ameridhia.

  Best yangu anatamani sana angeondoka na mumewe, na mpango wake ulikuwa wakati yeye yupo huko kikazi mumewe angekuwa anasoma degree ya pili. Mume amegoma amesema yeye hawezi kuacha kazi, na kama ni kusoma yeye atasoma hapa hapa tz. Hii issue inamsumbua sana best yangu na anasema kama vipi anaweza akaachia hiyo opportunity.

  Mimi nimemshauri asiache hiyoo nafasi aliyopata, na aendelee kumshawishi mumewe waende wote kwani sioni sababu ya huyo mume kutokwenda na mkewe. Siamini kama kazi ni kisingizio coz ni mwajiriwa serikalini,na mishahara ya serikali inajulikana kwa hiyo sio kusema akiacha hiyo kazi atakuwa amepoteza big opportunity.

  Naombeni tips zaidi juu mtazamo wenu kwenye hili labda naweza kupata idea za kumpa best yangu akaweza kumshawishi mumewe akubali waondoke wote, coz naamini itaimarisha ndoa yao.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wengine tukishauri tunaweza kuharibu.........yeye ndiye anayemfahamu mumewe vizuri zaidi anaweza kumwelewesha kwa utuvu na kama atatumia nguvu yake kama mwanamke, (naamini nimeeleweka) anaweza kufanikiwa.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  kwa utamaduni wetu wa kiafrica, mume kumkubalia itaonekana kama kale kamfumo unaoitwa mfumo jike wa kihindi.
  Kwa kuwa tunaendeleza utamaduni wetu wa mfumo dume hilo lijama halitakubali kwenda kusherehekea madola ya UN.
  Ushauri: wote wamtangulize Mungu mbele hakuna kitu kitakachoshindikana. wakimtanguliza Mungu mbele na kwa baraka zake mama ataondoka kwa amani ya moyoni, na mume atabaki bongo kwa amani ya moyoni, au wote wakaondoka kwenda UN au wote wakabaki bongo.
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kazi ndio mpango mzima!
   
 5. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa si kuta kusema hilo tangu mwanzo hata mimi nimeona ni suala la mfumo dume zaidi na je ataonekanaje kwa jamii, lakini mkuu mwisho wa siku huyo anayeenda huko ni mkewe na hayo ni maisha yao nadhani angefikiria effect watakayopata kwa wao kuwa mbalimbali kwa miaka 2 esp katika kipindi cha mwanzo wa ndoa yao.
   
 6. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haujaharibu mkuu ni ushauri wa maana pia asante sana
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  marriage vs career,siku zote ni mtihani mkubwa sana,achilia mbali mmoja kupata kazi majuu lakini hata mkiwa hapa bongo.Chukulia mfano kina mama ambao taaluma zao zinawalazimu kurudi nyumbani late kama bankers na manesi,akifika nyumbani amechoka,foleni (labda wanaishi Boko/mbagala),yaani hata nguvu ya kupika hana achilia mbali huduma ya kitandani.Mimi naona it is a matter of choice maana huwezi kula keki na wakati huo huo ukawa nayo mkononi,watulie watafakari na mwisho wa take chance,maisha wakati mwingine ni gamble.
   
 8. C

  Chief Ken Lo Member

  #8
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona hakuna ishu hapo koz hus amebariki safari!
  kwenye red kuwa serikalini sio kigezo cha kuvuruga mipango na harakati za m2 kimaisha, huwezi jua ana michongo gani inayomuingizia mawe hapo town zaidi ya hiyo salary! jamaa atakuwa ameweka vitu kwenye mizani kaona atapoteza fursa kibao akiwa nje ya nchi kwa hiyo miaka 2!!mshauri asiache hiyo nafasi, baraka za mwenzake zinatosha kabisa kumpa amani ya moyo
   
 9. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,477
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nadhani mke atumie subira zaidi. Yaani aendelee kumsihi mumewe wakati huo akijiandaa na safari. Lakini akikataa kabisa mke aondoke akaanze kazi labda upweke utamfanya mme afikirie upya msimamo wake. Lakini simshauri mke aachie hiyo chance.
   
 10. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani huyo mumewe ni macho juu sana kiasi anahofia kumwacha abaki TZ atakuta ameshasepa? manake hadi mwanamke anafikiria aachie post aliyopata ili abaki na Husband.. au labda ni uchanga wa ndoa ... mie hata sielewi!
   
 11. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Lakini kazi ya UN ni mkataba wa miaka miwili, so mume akiacha kibarua chake aondoke na mkewe then mkataba ukija kuisha itakuwaje?? Wanarudi kwenye msoto wa kutafuta kazi tena hapa bongo...?
   
 12. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Amwache mume tu hapa yeye aende, kazi ni kazi hata kama ni ya serikalini, hawezi mlazimisha mumewe aache kazi ili aende nae kwenye kazi yake, huwezi jua mbeleni itawasaidia ukizingatia kazi yake ni ya mkataba
   
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ushauri wangu Huyu Mdada Asiache kwenda huko UN..BUT pia ajaribu kujua kwa nini Mshkaji anagoma kwenda..Sitaki kuamini kama ni Mfumo dume ndo unasababisha Jamaa Achomoe..Wangapi wamewafata wakezao Bwana..Aendelee kumpa nafasi ya Kufikiria zaidi!!
   
 14. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sidhani kama anahofu ya kumuacha atakuta ameshasepa coz mtu akiwa macho juu juu hatasubiri usafiri ndio afanya mambo yake, atafanya na wewe ukiwepo, swala sio tu mume kubaki bt pia chances ambazo mume anaweza kupata kwa kukubali kusafiri na mkewe, cha kwanza ni suala la shule ambapo mke yupo tayari kumsapoti mumewe asome masters wakiwa huko kwa hiyo salary yake.
   
 15. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi zao ni mkataba sawa lakini ukishatia mguu chances za kuongezewa mkataba ni uhakika unless umefanya kazi hapo zaidi ya ten yrs..
   
 16. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umenena, its gamble n sometimes u hv take a risk, nimefurahi sana umeliona hilo la marriage v ajira esp to women inawacost sana,inahitaji hekima sana kwa mume kuelewa hili na mwanamke kuweza kubalance hayo maisha.
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nailyne, hilo bold ndio tatizo, wanaume wetu wa kiafrika hawapendi hiyo kitu,umsomeshe halafu badae uringe? au akikukosea tu uanze kumsimanga, hiyo ni ngumu sana na amini nakwambia ndio hiyo mumewe hataki
   
 18. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gaga thanks, nahisi umenifungua macho sana basi kama ni hivyo ipo kazi,nadhani umenisaidia kufikiria angle nyingine ya ushawishi,hilo la shule nadhani haitawork.
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Miaka miwili hata si mingi yaani wala asijiumize kichwa..............anaweza weka mechanisms ya kukutana kila baada ya muda flani wala haina shida! Kwanza its good bana to have a break!
   
 20. SaraM

  SaraM Senior Member

  #20
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaambie aende akakae mwenyewe kiasi, akirudi kama wamekutana jana yake mahaba motomoto
   
Loading...