sungura23

Member
Apr 1, 2013
52
72
Habari Wana JF! Poleni kwa shughuli za kila siku za ujenzi wa taifa letu pendwa. Leo npo jukwaa hili nipate mawazo/maoni/ushauri wenu.

Kwa sasa ninafanya kazi za sales kwenye kampuni moja ndogo hapa jijini Dar es Salaam. Ajira hii naitumikia kuanzia asubuhi saa 1 na hadi kufikia mchana saa 6 ninakuwa nimekamilisha majukumu yangu.

Natafuta namna ya kutumia muda wangu kuanzia saa 6 mchana hadi muda wa jioni kujishughulisha ili kujiongezea kipato. Yaani natafuta kazi ya kufanya kwa masaa ama kazi ya kuingia shift ya mchana.

Nina diploma ya TEHAMA (Information Communication Technology) na kiuzoefu nimewahi kufanya kazi kama "Technician", "Salesperson", "Customer Support Officer" na pia nimefanya kazi kama "Receptionist" kwenye mapokezi ya hoteli kwa miaka miwili.

Naweza:
-Kufundisha computer pamoja na applications zake
-Kufundisha lugha ya Kiingereza
-Customer Service/Customer Support
-Computer Service/Maintanance
-Data collection/Data entry
-Marketing/Sales
-Hotel Reservation/Booking
-Marketing and Sales

Mawazo/Ushauri/Mwongozo kutoka kwenu utapokelewa, naamini hakuna aliyefanikiwa bila ushirikiano na watu. Popote penye fursa nipo tayari tuzungumze.

0769-904755
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom