Soma CPA kasome defensive factors ambazo zinaweza kukulinda usiwe liable.Utaelewa....Pamoja na uzibaji wa njia Sijui walijibishana nini kama muwajuavyo madereva bajaji na boda, keno akamlamba kibao kijana akaon sio kweli kaenda kweny bajaj yake katafuta silaha kaichukua, kwamba hapa naenda kujeruhi, kamchoma nayo" unasema kaua bila kukusudia? Basi Sheria ni pana aisee
Boda boda na bajaji wengi wana bisibisi tena zile ndefu kabisa.Mkuu mambo ya kisu au bisibisi ni yiming hata uwe vandame mtu akikutime anakuua
Ok ok mkuuSoma CPA kasome defensive factors ambazo zinaweza kukulinda usiwe liable.Utaelewa.
Huku kudharauliwa na kuchukiwa mmekutaka wenyewe.Shida sio hekima shida ni chuki, I'm telling you I know what I'm telling you raia punguzeni chuki na Jeshi lenu,
"Jeshi la kupiga wananchi wa Tanzania" ....JKWTZ! 😲 💬 🤔Jeshi la kupiga raia, ni jeshi lisilo na nidhamu
Jeshi makini haliwezi kuact kama thugs
Kama kakutukana ndio una haki ya kumpiga?Kuna sababu, hawezi mtu akakuzaba makofi pasinakua na sababu yawezakua wewe ni mtovu wa nidhamu umemtusi km afanyavyo huyu member humu Don Vill hivi huyu aanze kuporomosha matusi mbele ya Askari na kumvimbia unadhani nini kitafuata? Mtu anatukana viungo vya mama yake anavitaja bila kua na staha unahisi nini kitafuata?,
Askari mwenye shule havimbi hovyo. Nasikitika kanari alishindwa kucontrol hasira.Punguza chuki za kijinga, form 4 failure ndio mlivyokaririshwa kua kila Askari ni form 4 failure? Acha kua mjinga chagua kua mwerevu,
Tatizo ni kwamba kuna watu baadhi wakiwa na nyadhifa flani serikalini wanafikiri ndio wana title deed ya hii nchi kwamba they can do you whatever they want, na wala huwawezi Fanya chochote, sasa ona sasa, Mungu atujalie hekima na busara katika kufanya maamuzi.Duuh inasikitisha sana kama ni kweli ila hawa jamaa muda mwingi wanakosea mengi kwa kujiona hawagusiki........sasa kama nikweli mtu mwenye mafunzo mpaka cheo hiki anakufa kibwege namna hii? Kwasababu ya parking? Afande gani mwenye mafunzo na inaonyesha alikuwa senior jeshini anakosa busara na hekima kiasi hiki.
Afike apa kambini atoe maelezo vizuri tumsikie ili tuone tunajadili vipi kifamiliaUjinga plus kigogo ni nani mbele ya Jeshi yaan kigogo umtume bodaboda akaue mwanajeshi alafu unavimba kua akiguswa utaua wewe nani useme akiguswa utaua mamlaka hayo unayatoa wapi?
Mbona watu wengine ni washamba sana? Wanafanya kazi bure? Si ni kazi waliyoichagua na wanalipwa? Hujui kuna mgawanyo wa kazi? Unajua watu wanaokulisha wewe? Unajua watu wanaokutibu? Unajua watu wanaosafisha takataka? Una maana kwa vile mtu analinda ndiyo apige raia bila kufuata sheria?Magari yamepita asubuhi Mzee wewe umelala yamepita malori kibao yamebeba wanajeshi yanatoka Lugalo, endelea kulala wao hawalali wanakulinda wewe na mipaka ya Nchi yako
Duuh Kanali ni mtu mkubwa sana jeshini kwann alifanya kitu Cha kijinga namna hii? SI Bora angepiga simu kikosini awaite vijana wake kuliko alichokifanya au alikuwa amelewa?Inasemekana ( kwa aliyenipa Taarifa Kamili kuwa ) Dereva Bajaji jana Usiku katika Baa Moja maarufu iliyo kwa ndani ( Mafichoni kidogo ) mkabala na Petro Station ya PUMA Kawe alipishana Kauli na Mwanajeshi ( tena Mkubwa wa Cheo cha Kanali ) kuhusu Kuzibiana njia ya kupita.
Ambapo Afande Kanali alikuwa Kapaki Gari lake lililokuwa limezuia njia kwa mbele na Dogo ( Dereva Bajaji ) kuhoji kwanini Afande aliziba njia hali iliyomkwaza Afande ( wa Cheo cha Kanali Muro kama sijalikosea Jina lake ) ambapo Afande Kanali akatoka ndani ya Gari lake na Kumzaba Makofi Dereva Bajaji huyo.
Kisha nae ( Dereva Bajaji ) kwa Hasira akaamua kwenda kuchukua Bisibisi Bajajini Kwake na kuja Kumchoma nayo Afande Kanali upande wa Moyo hali iliyomfanya akimbizwe Lugalo Hospital kwa Matibabu na Umauti kumkuta huko huko Wodini.
Wanajeshi wenye utadhani wana kwashiakoo. Wanategemea kuchangia raia kwa makundi. Unadhani mwanajeshi mmoja anaweza kuleta ngebe mbele ya raia? Tena raia mmoja tu...We endelea ukipigwa useme wanajeshi wakorofi over
Na pengine hata huyo bajaji ukute alikuwa hajui kama Marehemu ni mwanajeshi, ila Cha kujifunza huku barabaran sio sehemu Nzuri kuvimbiana Bora uwe mpole tu hasa ukiwa kapukuYaani inashangaza sana,unampiga mtu makofi,ili?
Sasa amekuchoma na bisibisi umekufa,wakati labda ungemuelimisha tu,kua dogo ngoja nipite,au unatumia saikolojia tu,mnayamaliza.Hii yakuamini askari anaweza akamdhibiti yeyote,inaleta changamoto.Hapo ukute kanali aliwaza tu kua kwasababu yeye ni mwanajeshi,akimpiga makofi,dogo ataomba msamaha,kumbe dogo kavurugwa,mwishowe ni kufa eti kwa kukitwa na bisibisi... aisee.