Baada ya Kutuzimia kimya kimya, inasemekana kuanzia saa 6 na dakika 1 usiku wa leo mnatuwashia. Mimi nahitaji majibu ya maswali yangu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
Je,

1. Mlipozima mliagizwa au ni kiherehere chenu tu cha kutaka Sifa wana Ubungo Tower?

2. Hasara ambayo nchi hasa TRA imeipata na Makampuni mengine Makubwa nchini italipwa nanyi Ubungo Tower?

3. Kutuzimia Kwenu mnadhani mmefikia Lengo au wana Ubungo Tower mmeshadharaulika na Watanzania?

4. Makampuni yaliyo chini yenu nyie Ubungo Tower hii Hasara ya kuanzia 27 Oktoba hadi 6 November hii mtawasaidia Kuwalipa?

5. Baada ya Kuzima ila bado Watu wakahimia katika Himaya ya 'Vipi Enyi' Ubungo Tower mnajiona mmekomoa au mmekomolewa?

6. Wakati Watu wa Ubungo Tower mmekaa Kikao cha Kufikia Upuuzi wenu mliotufanyia Akili zenu zilikuwa ziko sawa sawa?

7. Na Oktoba mwaka 2025 mtakuja tena na huu Upuuzi au mtajishtukia na Kuachia kwakuwa ajaye ni Mstaarabu wa Mkuranga / Ruangwa?

Nayasubiri majibu yangu huku nami nikisubiria kuhakikisha kama kweli kuanzia Saa 6 na dakika 1 Usiku wa leo Ubungo Tower mtaturejeshea raha.
 
Wanatakari majibu
IMG_20201030_114927.jpg
 
Tumerudisha mtandao sasa tunaomba radhi kwa hitilafu zilizo jitokeza.!

na pia tutalipa fidia kwa watanzania wote ifikapo 2025

nb.wote mlio tumia VPN tutawapa adabu
asanteni wa tanzania.
 
Back
Top Bottom