Kauli zitakazomponza Magufuli na serikali yake

Kauli zitakazomponza Magufuli na serikali yake

Kwa muda mrefu Ccm iliweza kuwadanganya wananchi kwa Tanzania ni nchi changa na masikini. Mpaka miaka ya karibuni wapinzani walipoanza kuwafumbua macho kwamba nchi yenye madini aina zote, misitu, ardhi yenye rutuba, maziwa na bahari, gesi nk siyo masikini.

Magufuli akaidaka na kuitumia kwenye kampeni zake kwamba nchi hii si masikini. Hata baada ya kuukwaa urais ameendelea kuwambia wananchi juu ya utajiri wa nchi hii. Hadithi za kasungura kadogo hatuzisikii tena. Wananchi wanaambia ukweli na kupewa matumaini.

Tatizo litakuja pale ambapo wananchi wanaoimbiwa nchi yao ni tajiri wasipoona utajiri huo ktk haliza za maisha ya kawaida. Leo kelele zimeanza kwamba mitaani hakuna fedha na hali ni ngumu sana. Leo watu wanauliza tunabiwa serikali imeongeza makusanyo, mbona hatuoni nafuu kwenye huduma za jamii? Naamini hawamu hii itakuwa ngumu sana kwa wananchi wakati rais wetu anatuambia nchi yetu ni tajiri!
Hauoni unafuu kwenye HUDUMA za jamii, HUDUMA gan hizo? Unatumia macho ukiwa umevaa MIWANI IPI?
Unatazama kwa macho yapi kwenye ELIMU usiweze kuona wanafunzi wanasoma bila ada hadi kidato cha NNE, je huo siyo unafuu? MUHIMBILI wamenunua vitanda na mashuka ili wagonjwa wasilale chini, je huo kwako siyo unafuu?
Au ulidhani Magufuli atakuwa anagawa pesa mifukoni mwenu?
Acha uvivu, fanya kazi kwa bidii na ulipe kodi bila shuruti tuijenge nchi yetu!
 
Ni watanzania wajinga na wapumbavu peke yao watakaotegemea muhujiza wa aina hiyo! JPM aanze transformation leo kisha asali na maziwa vianze kutiririka kesho!
Tukubali kwamba mabadiliko haya yatachukua muda matokeo yake kuanza kuonekana mtaani na kwenye meza ya chakula ya kila kaya; tumpe muda na kumsaidia kwa kufanya kazi kwa bidii na kukataa maovu, tukome kushangilia watu waliojineemesha kwa raslimali zetu, tujifunze kukemea maovu, tujifunze kula tunachozalisha badala ya kujigeuza mchwa na mifisadi. Kupungua kwa mzunguko wa pesa mitaani ni matokeo ya kazi nzuri ya JPM ya kudhibiti fedha haramu za wizi, ufisadi na ujangili; subira yavuta heri; anayetaka miujiza aende kwa Geor davie na Anthony Lusekelo au TB Joshua akakusanye utajiri wa miujiza, hapa Tanganyika ni KAZI TU!
wewe msukule unapiga hiyo kazi au ndo kushangilia tu
 
Ukishaanza kutegemea maliasili zisizo mali akili tayari ushakuwa masikini.
 
AAh, kumbe utajiri ni pesa nyingi zikizagaa mitaani nilikuwa sijui asante kwa taarifa nzuri. Tuwashauri watengeneze nyingi zizagae mtaani mchezo utakuwa umekwisha raisi wetu atakuwa ametoa umaskini Tanzania ooh shauri zuri.
 
Tatizo la nchi hii ni kuacha watawala wafanye wanavyotaka hadi kila mmoja anajiona anaweza kuwa rais. Nchi nyingine kiti hicho ni cha moto. Rais lazima apigwe presha ajue anaongoza watu wanaofuatilia kila kinachofanywa na serikali yake.

Tukimuacha aongoze anavyotaka tutashuhidia mamia ya watu wakiutaka urais 2020 kama ilivyokuwa 2015
Kwa viwango vya JPM;ni wachache sana watautaka urais tena
wewe msukule unapiga hiyo kazi au ndo kushangilia tu

Overdog! Signature yako na Kutumia lugha hasi kama hiyo kunaakisi barabara udhaifu wa haiba, elimu, uzoefu na uwezo wako wa kufikiri na kuchambua mambo; sikulaumu wewe bali makuzi na mazingira uliyokulia na unamoishi sasa. Bs
 
CCM CCM hakuna Jipya Umaskini wa Tanzania ni wa Akili jamani MTU anadanganywa miaka 50 Kwa kupewa T-shirt Na kitambaa cha kichwa unategemea nini? Leo pamoja Na shida zote za watanzania Kundi dogo la watu 400 WABUNGE wanakopeshwa Mamilioni ya Fedha Na Magari ya kifahali watanzania wale wale waliopewa T-shirt Na vitambaa vya kichwa wamenyamaza kimya utadhani wehu.Magufuli baba waambie tu kuwa nchi no Tajiri watakushangilia tu
 
Huna lolote MTK hakuna cha ajabu Kwa JPM ni mtanzania Mwenye uchungu Na CCM amekuwa serikali awamu 2 nini cha ajabu
 
Kwa muda mrefu Ccm iliweza kuwadanganya wananchi kwa Tanzania ni nchi changa na masikini. Mpaka miaka ya karibuni wapinzani walipoanza kuwafumbua macho kwamba nchi yenye madini aina zote, misitu, ardhi yenye rutuba, maziwa na bahari, gesi nk siyo masikini.

Magufuli akaidaka na kuitumia kwenye kampeni zake kwamba nchi hii si masikini. Hata baada ya kuukwaa urais ameendelea kuwambia wananchi juu ya utajiri wa nchi hii. Hadithi za kasungura kadogo hatuzisikii tena. Wananchi wanaambia ukweli na kupewa matumaini.

Tatizo litakuja pale ambapo wananchi wanaoimbiwa nchi yao ni tajiri wasipoona utajiri huo ktk haliza za maisha ya kawaida. Leo kelele zimeanza kwamba mitaani hakuna fedha na hali ni ngumu sana. Leo watu wanauliza tunabiwa serikali imeongeza makusanyo, mbona hatuoni nafuu kwenye huduma za jamii? Naamini hawamu hii itakuwa ngumu sana kwa wananchi wakati rais wetu anatuambia nchi yetu ni tajiri!


Comrade, nadhani kwako masuala ya uchumi yamekupita kando. Kwa watu wanaojua uchumi hali ya sasa ilitarajiwa baada ya JPM kutangaza vita dhidi ya wakwepa kodi, wahujumu uchumi na mafisadi kwa ujumla wake. Ni kweli kuna kipindi fedha ilikuwa imezagaa mitaani na infalation kuwa juu kwa kuwa kulikuwepo na fedha chafu na ambazo hazitokani na uzalishaji. Uzalishaji ulikuwa chini. Sasa kuna udhibiti kwa hiyo fedha ya kuzagaa mitaani hakuna. Ukitaka fedha lazima ufanye kazi. Nafuu haiwezi kupatikana sasa itapatikana baada ya muda. Unakumbuka Enzi za Mkapa alidhibiti matumizi mpaka wakampachika jina la ukapa? Fedha kwa maana ya shilingi ilikuwa na thamani watu walikuwa wanapanda daladala kwa sh. 150/-. Sh. 1,000 ya wakati wa mkapa ulikuwa unaweza kununua nusu kilo ya sukari, nusu kilo ya unga, nusu kilo ya maharage.

Kwa hiyo faida ya udhibiti unaofanywa na MAGUFULI utauona baadaye kidogo na siyo kwa haraka kama unavyotaka wewe na watu wa aina yako. Uchumi haujengwi kwa blah blah na kulaumu na malalamiko yasiyo na mwisho. Nchi na uchumi wake inajengwa kwa kufanya kazi, na siyo kungojea dezo. Tunachopaswa kufanya sisi wananchi kwa maana ya Watanzania ni kumuunga mkono Rais kwa juhudi anazofanya. Kama JPM alidaka hoja ya wapinzani hilo ni jambo jema na wala huna haja ya kuanza kulalamika. Nchi haiwezi kujengwa kwa kulalamika kila dakika. Fanyeni kazi, na siyo kungojea au kuombea Rais afanye kosa halafu mje kwa nguvu kusema 'si mnaona, eti bwana!'.
 
Kama watu hawafanyi kazi wewe unafikiri watapata wapi pesa?.

Tatizo sisi watanzania tunalalamika sana lakini kujishughulisha hatutaki,yaani watu badala ya kufanya kazi wamekazania kujadili DNA ya Tiffa Dangote
Wewe unafanya kazi gani mkuu?
 
Kama watu hawafanyi kazi wewe unafikiri watapata wapi pesa?.

Tatizo sisi watanzania tunalalamika sana lakini kujishughulisha hatutaki,yaani watu badala ya kufanya kazi wamekazania kujadili DNA ya Tiffa Dangote
Nani kakwambia watu hawafanyi kazi? Acheni kauli za kilevi hizo... Leo nilikua napata nyama choma sehemu akaja kijana mmoja anauza makoti ya ngozi lundo mkononi mwake ... Kaja amechoka kabisa.... Tukamwambia asante hakuelewa akaanda kutulilia hali... Kwamba kazunguka wiki nzima hajauza na hapo alipo hajala.... Ilibidi tumnunulie ugali ajiunge nasi kula nyama... Kisha nikampa elfu 10 akaenda zake... Huyo ni mmoja wengine?

Watu wanavuja jasho sema kazi hazina tija... Acheni kauli za shibe na kilevi hizo....
 
Nchi hii ina hela za kumwaga.Wageni wanashangaa kuona watanzania wenyewe kama watu binafsi walivyozubaa.

Wewe kampuni hadi kutoka jirani tu hapa kenya wanakuja waanzisha bishara za kuzalisha vifaranga wanatajirika kibao mtanzania kazubaa tu anaangalia serikali imtafutie fursa.

Ziko kampuuni kama STEERS wanauza chips kuku wametajirika hadi basi.

Wako wafanyabiashara kama SAMAKI SAMAKI anajiuzia chakula chenye samaki ana maduka kila kona Dar salaam,MTANZANIA KAZUBAA TU ANASUBIRI SERIKALI IMTAFUTIE FURSA.

Raisi anaposema Tanzania kuna utajiri hatanii.Tatizo ni watu waliozubaa kama wewe.

Uganda ukienda walimu badala ya kulalamika huungana na kuanzisha shule zao.Wakiwa wao ndio wamiliki na walimu.Mashule mengi makubwa ya kutisha uganda yanamilikiwa na walimu.Tanzania watu wamezubaa tu unakuta mtu ana PHD anasubiri serikali imtafutie fursa hajui cha kufanya kama yule DK.RUTENGWE aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro
Sawa wakubwa ndo tunazisubiri hizo hela za kumwaga!!!
 
Kwa muda mrefu Ccm iliweza kuwadanganya wananchi kwa Tanzania ni nchi changa na masikini. Mpaka miaka ya karibuni wapinzani walipoanza kuwafumbua macho kwamba nchi yenye madini aina zote, misitu, ardhi yenye rutuba, maziwa na bahari, gesi nk siyo masikini.

Magufuli akaidaka na kuitumia kwenye kampeni zake kwamba nchi hii si masikini. Hata baada ya kuukwaa urais ameendelea kuwambia wananchi juu ya utajiri wa nchi hii. Hadithi za kasungura kadogo hatuzisikii tena. Wananchi wanaambia ukweli na kupewa matumaini.

Tatizo litakuja pale ambapo wananchi wanaoimbiwa nchi yao ni tajiri wasipoona utajiri huo ktk haliza za maisha ya kawaida. Leo kelele zimeanza kwamba mitaani hakuna fedha na hali ni ngumu sana. Leo watu wanauliza tunabiwa serikali imeongeza makusanyo, mbona hatuoni nafuu kwenye huduma za jamii? Naamini hawamu hii itakuwa ngumu sana kwa wananchi wakati rais wetu anatuambia nchi yetu ni tajiri!
Nimemsikia akisema nchi hii inauwezo wa kuwa donor country!! Hahahah south Africa yenyewe sio donor country itakuwa hii? Labda donor wa damu.
 
Naungana na Magufuli nchi hii si masikini ila mafisadi na mijizi ndio iliyotufikisha hapa ikiwemo iliyokimbilia upinzani baada ya kutoswa ccm. Pili tuchape kazi hatutaomndoa umasikini kwa kucheza pool table na kuzunguusha mikono.
 
Back
Top Bottom