Kauli za rais Kikwete akiwa Igunga si kutisha na kuingilia Uhuru wa Mahakama?

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
494
Awali ya yote niwapongezi wazalendo walalahoi wa nchi kwa uvumilivu mwingi dhidi ya uongozi usionatija wa Serikali yetu.
Katika Vyombo vingi vya habari leo hii kuna Picha kutoka Ikulu ikimuonyesha Rais akisalimiana na wenyeji wa Igunga katika ziara za Kiongozi wa nchi kuhimiza manedeleo na shughuli za CCM.

Kauli na maneno ya Kiongozi wa nchi na mtawala kutoa maneno ya kushambulia muhimili mwingie wa Mhamakama na wakati huo huo kesi shauri likiwa mahakamani ni upofu na ufinyu wa busara.

Katika ili na wasiwasi kama Rais JK alipata wala nafasi fupi kusoma hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Igunga au ushauri wa kisheria kutoka kwa watu wake? Kama kiongozi wa nch anaweza kutoa maneno ya upuuzi mbele ya wananchi juu ya mwenendo wa kesi ya uchaguzi Igunga ,je kwa nini pia wananchi wasiamini kama kuna wakati anawatisha watendaji wa mahakama kutekeleza mahitaji yake kama ambavyo kuna fununu katika kesi ya uchaguzi wa Arusha.?

Katika ili Raisi JK ameonyesha udhaifu wa wazi na ukosefu wa Busara na utawala bora.Moja ya nukuu ni hii

Alisema ujenzi wa Daraja ni ahadi ya serikali ya chama cha CCM na ipo katika ilani ya CCM sasa anashangaa imekuwa ni kigezo cha kuvuliwa ubunge kwa Kafumu, itabidi sasa tuwe tunafanya kampeni za Kibubu kwani ukiongea tu inakuwa kosa na hapo mbeleni itabidi tutafute namna ya kuepukana na hilikwa kauli hii naona anapingana moja kwa moja na sheria za nchi hii. Pia alisema Dr. kafumu amekata Rufaa wanachosubiri ni uamuzi wa mahakama kama watashinda au la lakini wakishindwa wataingia kwenye uchaguzi na watashinda kwa kishindo kuliko uchaguzi uliopita.
 
Gazeti la mwananchi la leo limeandika habari kuhusu JK kufungua ujenzi wa daraja la Mbutu na Mradi mkubwa wa maji kwa wakazi wa Igunga. Akihutubia wakazi wa Igunga kwanza alionyesha mshangao wake kwa Mahakama kumvua Ubunge aliyekuwa mbunge wa hapo Dk Kafumu vile vile Raisi alienda mbali zaidi na kudai kwamba Ujenzi wa hilo daraja ni moja kati ya mambo yaliyopo kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2010. Maswali ya kujiuliza hapa je JK anaingilia uhuru wa mahakama?? na je baada ya JK kuongea hayo haki itatendeka wakati wa kusikiliza Rufaa? vile vile JK alienda Igunga ktk ziara ya kiserikali au Kichama? Kwann ujenzi wa hilo daraja ambalo limekuwa kero toka enzi na enzi uanzwe kujegwa sasa? Je hii si rushwa ya wazi kwa wanaigungunga?
Source: Mwananchi Jumanne, January 8, 2013 uk wa 4
 
nawaonea huruma ambao mnahangaika na JK, ametoka msibani juzi kwa msanii mwenzie tumuache apumzike!
 
kwenye kesi ya lema haki ilitendeka?unajua tofauti na uhusiano kati ya chama tawala na serikali ki utendaji na kimuundo?ukijibu maswali haya itakuwa ni rahisi kukuelewesha.
 
Katuni+Igunga.jpg
 
Moja ya kauli tata za kufungua mwaka za Mh... kuna msemo unasema matakwa ya mkubwa ni amri!

Gazeti la mwananchi la leo limeandika habari kuhusu JK kufungua ujenzi wa daraja la Mbutu na Mradi mkubwa wa maji kwa wakazi wa Igunga. Akihutubia wakazi wa Igunga kwanza alionyesha mshangao wake kwa Mahakama kumvua Ubunge aliyekuwa mbunge wa hapo Dk Kafumu vile vile Raisi alienda mbali zaidi na kudai kwamba Ujenzi wa hilo daraja ni moja kati ya mambo yaliyopo kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2010. Maswali ya kujiuliza hapa je JK anaingilia uhuru wa mahakama?? na je baada ya JK kuongea hayo haki itatendeka wakati wa kusikiliza Rufaa? vile vile JK alienda Igunga ktk ziara ya kiserikali au Kichama? Kwann ujenzi wa hilo daraja ambalo limekuwa kero toka enzi na enzi uanzwe kujegwa sasa? Je hii si rushwa ya wazi kwa wanaigungunga?
Source: Mwananchi Jumanne, January 8, 2013 uk wa 4
 
Ngoja nirejee utekelezaji wa ahadi zake zote tangia 2005 ambazo zipo kwenye ilani then ndiyo nitaanza kumteteea kwa nguvu zote.
 
Kwa maslahi ya chama!!!na ziara iko kichama zaidi sion!!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

unataka kutuambia ajeenda km rais bali km mwanachama wa ccm...hakuna kitu kama hicho,, yeye ni umbumbumbu wa sheria tu, sheria za uchaguzi zinasema kipindi cha kampeni kusiwepo na mambo yanayoashiria rushwa....wao waligawa mahindi na waziri wake akatumia kofia yake vibaye na kuatisha wananchi kama msipomchagua mbunge wa ccm asingejenga hilo daraja wakati serekali inatakiwa itekeleza majukumu yake bila kuangalia sehemu fulani ni chama gani kinatawala........
 
Awali ya yote niwapongezi wazalendo walalahoi wa nchi kwa uvumilivu mwingi dhidi ya uongozi usionatija wa Serikali yetu.
Katika Vyombo vingi vya habari leo hii kuna Picha kutoka Ikulu ikimuonyesha Rais akisalimiana na wenyeji wa Igunga katika ziara za Kiongozi wa nchi kuhimiza manedeleo na shughuli za CCM.

Kauli na maneno ya Kiongozi wa nchi na mtawala kutoa maneno ya kushambulia muhimili mwingie wa Mhamakama na wakati huo huo kesi shauri likiwa mahakamani ni upofu na ufinyu wa busara.

Katika ili na wasiwasi kama Rais JK alipata wala nafasi fupi kusoma hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Igunga au ushauri wa kisheria kutoka kwa watu wake? Kama kiongozi wa nch anaweza kutoa maneno ya upuuzi mbele ya wananchi juu ya mwenendo wa kesi ya uchaguzi Igunga ,je kwa nini pia wananchi wasiamini kama kuna wakati anawatisha watendaji wa mahakama kutekeleza mahitaji yake kama ambavyo kuna fununu katika kesi ya uchaguzi wa Arusha.?

Katika ili Raisi JK ameonyesha udhaifu wa wazi na ukosefu wa Busara na utawala bora.Moja ya nukuu ni hii

Alisema ujenzi wa Daraja ni ahadi ya serikali ya chama cha CCM na ipo katika ilani ya CCM sasa anashangaa imekuwa ni kigezo cha kuvuliwa ubunge kwa Kafumu, itabidi sasa tuwe tunafanya kampeni za Kibubu kwani ukiongea tu inakuwa kosa na hapo mbeleni itabidi tutafute namna ya kuepukana na hilikwa kauli hii naona anapingana moja kwa moja na sheria za nchi hii. Pia alisema Dr. kafumu amekata Rufaa wanachosubiri ni uamuzi wa mahakama kama watashinda au la lakini wakishindwa wataingia kwenye uchaguzi na watashinda kwa kishindo kuliko uchaguzi uliopita.

Mkuu umepotoka, tena sana tu maana wewe kama mwana CHADEMA unangalia upande wako tu na wa chama chako.
Sidhani kama unawakilisha maoni ya wana Igunga na Mbutu waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza, kumwelewa na kumpa moyo rais kwa hayo aliyoyatamka.

Tujiulize kwani mhimili wa sheria una tawaliwa na miugu hadi wasifanye makosa?

Kosa kubwa ililofanywa katika hukumu dhidi ya Kafumu ni KULAUMU ILANI YA CCM.
Inaelekea huyo hakimu/jai aliyetoa hukumu ni kada wa CHADEMA.

Kuwalaumu viongozi walioko madarakani kwa kuwapa moyo wananchi katika machungu waliyonayo huo ni upuuzi.
Ssa leo nenda pale Igunga au Mbutu na kwaambie wale wananchi kwamba ile ahadi ya JK ilikuwa bomu na kapepee bedera yako kama hujatukanwa.

Ni ujinga kulaumu tu katika mambo ya matatizo ya msingi ya wananchi ati kwa vile tu ahadi zimetolewa n CCM.

Kwa taarifa yako hata huyo kada wa CHADEMA aliyefungua kesi dhidi ya Kafumu kwa ajili ya daraja hilo hilo hata kwenye sherehe hakuwapo kwa aibu.
Aibu hiyo ndiyo inayowaonyesha CHADEMA walivyo wanafiki.

Na kwa taarifa yako wananchi wa Igunga wameomba, tena mbele ya Rais barabara hiyo iwekewe lami toka mjini, kilometa karibu sita, na ombi hilo limekubaliwa.
Kubwa zaidi ni Mgufuli tena aliyesema anaipandisha barabara hiyo toka kiwango cha halmashauri kuwa kiwango cha kimkoa kama anavyoruhusiwa na sheria.

Na hilo CHADEMA nendeni kwa hakimu/jai yule yule ili mrudishe maendeleo ya wana Igunga nyuma.
 
Mimi binafsi nakushangaa wewe kwa kujiuliza swali la kitoto kama hilo.huyo bwana hajielewi kwa lolote lile.kama aliweza kusamehe wezi wa epa kana kwamba yeye amekuwa mahakama hili linakushangaza vipi?msamehe bureeeeee.
 
hii kauli ya jk itamzamisha Kafumu
hali haikuwa nzuri maana hata mapokeo ya hizo kauli zake hayakuwa mazuri kwani watu wengi walikumbwa na mshangao huku wakiguna tu, isipokuwa watu waliokuwa katika msafala wake ndo walikuwa wakimpigia makofi.
 
Maumivu ya kichwa huanza polepole. Pole Dr. Kafumu kwa kulazimishwa mambo na wanaCCM hadi PhD yako inaota ukungu. Waungwana tulikusikia ukisema hutaki kukata rufaa wamekulazimisha umekata.
Dr. Kafumu unatakiwa kujua kuwa waliokuvua ubunge ni wajuaji wa mambo yao na vilevile na wao walijua kuwa wewe kuacha cheo kizito kama cha ukamishina tena wa wizara nyeti ya nishati na madini eti kisa kuwasaidia wanaigunga wenzio inapwaya kidogo. Ungeweza kuwasaidia ukiwa kamishina zaidi kuliko ukiwa mbunge.
Redio mbao kuwa uliahidiwa uwaziri hatuwezi kuzipuuza na redio mbao kuwa huyu ndugu alijua mwenendo wa kesi yako na ndiyo maana hakukuteua kuwa waziri wakati anafanya marekebisho ya mwisho ya baraza lake la mawaziri nazo ni hisia sahihi japo hakuna data za kukazia.
Nashauri Dr. Kafumu ukutane na Hawa Ngumbi akushauri jinsi ya kuondoa kesi mahakamani, maana utakaposhindwa CCM haitakulipia hizo gharama utalipa mwenyewe.
 
Mimi nadhani angejifunza sasa Kwamba Baada ya Rwekabarila kufanya yale aliyokuwa amemuagiza na wananchi Kumlilia Mungu atende Haki, Waheshimiwa Majaji kwa kiwango Kikubwa wameamua kutenda haki na kuwalinda wananchi na dhuluma za watawala

Raisi ametukosea wananchi heshima ,nadhani amevimba kichwa kwa sababu mambo mengi anayaamua,kuyatenda na kuyatekeleza akidhani yeye yuu juu ya sheria anajipoteza,Maadamu ametamka kwamba mahakama haikutenda haki kama vile yeye ni Jaji wa mahakama ya rufaa katika hiyo rufani ya Kafumu wananchi tutaiangali kwa jicho la karibu zaidi
Nimkumbushe tuu Raisi Kikwete Kwamba nchi sio mali yake na ni tofauti kama anavyoendesha chama chake cha CCM ,kule amejimilikisha chama,leo anaweza akaamuka akasema hakuna mwanaume anaweza kugombea nafasi ya usipika wa bunge na ikawa
Akasema wajumbe wa NEC hawatachaguliwa na mkutano mkuu na ikawa
Akasema wajumbe wa nec 2/3 watatokana na familia ya Kikwete na ikawa
Akasema wakuu wa mikoa na wilaya watakuwa ni rafiki zake na wa mwanawe Ridhiwani na ikawa
Lakini asituchezee kuanza kuagiza mahakama Kuu kutenda atakavyo kamwe hatutamvumilia
 
hali haikuwa nzuri maana hata mapokeo ya hizo kauli zake hayakuwa mazuri kwani watu wengi walikumbwa na mshangao huku wakiguna tu, isipokuwa watu waliokuwa katika msafala wake ndo walikuwa wakimpigia makofi.
Muongo mkubwa, mbona wananchi walifurahi sana pamoja na wale sungusungu walioonyesha gwaride la mguumbele!
 
kaza buti jk tekeleza ahadi za CCM ..waache waendelee kupiga m4c..daraja tayari limejengwa sijui watakuja sema hapo kuwa ccm haijafanya kitu
2015 ni kama hivi CCM NIMEFANYA VS CHADEMA NTAFANYA ...... MWANANGU NTAKULETEA PIPI VS MWANANGU CHUKUA PIPI TAYARI NIMEKULETEA.. HA HA KICHEKO
 
Muongo mkubwa, mbona wananchi walifurahi sana pamoja na wale sungusungu walioonyesha gwaride la mguu

HADI TV ZIMEONYESHA MTU NYOMI MTU WANASHANGILIA KWENDA MBELEE...TEH TEH HADI 2015 CHADEMA MTAONGEA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWENU..
 
Mkuu umepotoka, tena sana tu maana wewe kama mwana CHADEMA unangalia upande wako tu na wa chama chako.Sidhani kama unawakilisha maoni ya wana Igunga na Mbutu waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza, kumwelewa na kumpa moyo rais kwa hayo aliyoyatamka.Tujiulize kwani mhimili wa sheria una tawaliwa na miugu hadi wasifanye makosa?Kosa kubwa ililofanywa katika hukumu dhidi ya Kafumu ni KULAUMU ILANI YA CCM.Inaelekea huyo hakimu/jai aliyetoa hukumu ni kada wa CHADEMA.Kuwalaumu viongozi walioko madarakani kwa kuwapa moyo wananchi katika machungu waliyonayo huo ni upuuzi.Ssa leo nenda pale Igunga au Mbutu na kwaambie wale wananchi kwamba ile ahadi ya JK ilikuwa bomu na kapepee bedera yako kama hujatukanwa.Ni ujinga kulaumu tu katika mambo ya matatizo ya msingi ya wananchi ati kwa vile tu ahadi zimetolewa n CCM.Kwa taarifa yako hata huyo kada wa CHADEMA aliyefungua kesi dhidi ya Kafumu kwa ajili ya daraja hilo hilo hata kwenye sherehe hakuwapo kwa aibu.Aibu hiyo ndiyo inayowaonyesha CHADEMA walivyo wanafiki.Na kwa taarifa yako wananchi wa Igunga wameomba, tena mbele ya Rais barabara hiyo iwekewe lami toka mjini, kilometa karibu sita, na ombi hilo limekubaliwa.Kubwa zaidi ni Mgufuli tena aliyesema anaipandisha barabara hiyo toka kiwango cha halmashauri kuwa kiwango cha kimkoa kama anavyoruhusiwa na sheria.Na hilo CHADEMA nendeni kwa hakimu/jai yule yule ili mrudishe maendeleo ya wana Igunga nyuma.
Ndugu usiwe na fikra finyu juu ya matumizi ya Sheria unaposema ni Ujenzi wa Daraja la Mbutu ni Ilani ya CCM ilikuwaje Magufuli kusema nanukuu "MSIPOICHAGUA CCM DARAJA LA MBUTU HATUTAJENGA" yeye akiwa waziri anamamlaka kisheria kuyazungumza hayo, kama kauli hizi angezizungumaza mgombea Kafumu zisingekuwa na utata, Na unaposema hukumu dhidi ya Kafumu ni kulaumu Ilani ya CCM na Jaji ni kada wa CDM hapo nimekuweka katika kundi la Vilaza kwa kuandika bila kutafakari.
 
Back
Top Bottom