Kauli ya Rais kusali siku tatu imetafsiliwa kinyume,Makanisa yanafurika na kuongeza maambukizi. Serikali ichukue hatua

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Wasalaam wana jamvi...Tuepushwe na janga hili.

Huko Korea Kusini,nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi mapema tu baada ya China,kuna mji wa Daegu,huu ni mji wa nne kwa ukubwa huko Korea Kusini,unapatikana Kusini mwa Korea Kusini.Hapa ndio alipatikana mgonjwa wa 31 kati ya wagonjwa wa mwanzo kugundulika na Corona.Mama huyu muumini wa (Huduma za Kiroho) wa kanisa la Shincheonji aligundulika baada ya kuwa amehudhuria kanisani zaidi ya mara 5 katika mlolongo wa majuma mawili.

Mji wa Daegu ikawa ndio "epicentre" ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona Korea Kusini.75% ya wagonjwa wote Korea kusini walitokea mji wa Daegu na 73% toka katika kanisa hili.

Hata baada ya Mama huyu,ambaye vyombo vya habari vimempa jina la "SuperSpreader Woman" kugundulika na dalili za Corona,bado aligoma kuchukuliwa vipimo,akazidi kwenda kanisani na kuambukiza wengine.Na waumini wengine walipotakiwa kwenda kupima,walikaidi kwa kuamini kuwa "Maombi na damu ya Yesu vitawaokoa".

Walizidi kwenda kanisani na kuambukizana.Baada ya mgonjwa huyu wa 31(Superspreader Woman),serikali iliamua kufunga makanisa,sehemu za starehe,massage centres na mahali pote pa mkusanyiko.Hii ikawa ni pamoja na kuufunga mji wa Daegu kwa kuzuia watu kuingia na kutoka.Mji huu kama ilivyo Wuhani China na Meli ya Diamond kule Japan,ukafungwa na watu wakabaki ndani bila kutoka nje.

Serikali ikatoa tamko kali kwa wote watakaokusanyika kwa ibada au mambo mengine,haikuzuia watu kusali ila ilisisitiza watu wasali wakiwa katika familia zao ndani ya nyumba.

Kiongozi wa Kanisa hili la maambukizi alipoona hali mbaya na watu wanakufa,akatoka kuomba radhi raia,akitoa mchango wa $10 milioni kama sehemu ya kusaidia kukabiliana na gonjwa hili.Serikali ikazikataa na ikaamua kumfungulia mashitaka kwa uzembe na kusababisha hatari ya uhai wa watu.

Tumeanza siku tatu za kusali na kuliombea Taifa,hali hii imepokewa kwa namna tofauti na mtazamo tofauti.Wale wenye huduma za kiroho wameanza kusema wanamuunga mkono Rais kuliombea Taifa,na wanatangaziana ratiba za mikesha na mfungo katika mkusanyiko wa makanisa yao.Huko Twitter na Instagram,Manabii na Mitume wameanza kutuma video wakiwa wamesongamana wakiomba na kusema wanamuunga mkono Rais.

Sasa Manabii na Mitume,wameanza kukusanya watu makanisani kwa kufuata kauli ya kuomba siku 3 aliyotoa Rais,na uinjilishaji huu mamboleo,wengi wanatuma kwenye mitandao na kum-tag msemaji wa Ikulu ili aone juhudi zao kuwa wanamuunga Rais.

Hili ni janga jingine.Huu ni mtihani mwingine ambapo kauli ya Rais inaweza kuchukuliwa kwa namna ya kuongeza misongamano.

Kama wenzetu walichukua hatua kali baada ya mgonjwa wa 31 tu,sisi mpaka sasa wagonjwa ni 140+ kwanini tusichukue hatua muhimu?

Hawa Manabii na Mitume wao hawaangalii sana taratibu za afya na kanuni zake,wao wanatazama mambo kwa imani na miujiza.Katika hili hatuitaji miujiza na maombi tu,tunapaswa kufuata kanuni zote za afya na kuheshimu ushauri wa wataalamu na si Wanasiasa.

Wengine wanadhani kufunga makanisa ni kuzuaia uhuru wa kuanudu...BIG NO!Na wengine wanaona kufunga makanisa na kuondoka uwezekano wa makusanyiko ya watoa sadaka na malimbuko!Ukisisitiza mkusanyiko wa ibada katikati ya janga hili,ni uuwaji!Pepo mchafu wa aina hii awatoke manabii na mitume wanaotazama sadaka na sio uhai wa waumini wao.Nyakati hizi ndio tunaweza kujua rangi halisi ya Mitume na Manabii wetu.

USHAURI:

(a)Kama ambavyo wenzetu waliifunga miji yenye maambukizi makubwa kusiwe na kuingia wala kutoka,sasa ni rasmi Mji kama Dsm unapaswa kuwa na "half lockdown".Kuruhusu magali ya chakula na mizigo tu.Mgonjwa alipatikana Lindi,ametokea Dsm na aligundulika ndani ya Basi.

(b) Mamlaka kuu itoe tamko kuzipumzisha sehemu za ibada,starehe na mikusanyiko katika miji mikubwa na hasa mji wa Dar es Salaam,sababu tuna case study kuwa nchi moja athirika,75% ya wagonjwa walitokea kanisani.Kufunga sehemu za ibada sio kuzuia uhuru wa kuabudu bali ni kuongeza nafasi ya watu kuwa na uhuru wa kuabudu katikati ya majanga yanayoweza kuwaangamiza watu sababu ya mikusanyiko.Pale Roma,Vatican,sasa hata Pope na Maaskofu pamoja na Mapadre hawatumii kikombe kimoja cha divai,maana mapadre wengi Italia wamekufa kwa Utamaduni wa kanisa wa kutumia Chalice moja na Chibolio moja kwenye misa,kumbe wakagundua Corona inaambukiza hata kwenye kikombe cha divai ambacho kiimani ndani yake ipo damu na mwili wa Yesu Kristo...Hii Corona inasambaa hata katika vyombo vilivyobeba mambo matakatifu(kiimani).

(c)Serikali kwa kutumia vyombo vyake Vikuu vya Habari kama Tv na Radio,viunde vipindi maalumu vya kimasomo kwa Watoto wa Chekechea mpaka Sekondari ya Upili na kuvirusha kila siku ili kufanya muendelezo wa kielimu kwa watoto wanapokuwa nyumbani.Huku kwenye nchi zilizoendelea,watoto wanaendelea kupata mafunzo kwa njia ya "Online" ili kufanya wasijisahau.Kwetu huko nyumbani teknolojia hii ni ngumu kutekelezeka vijijini.Radio na Tv vinaweza kuwa mbadala...Hii ndio kazi ya Wizara ya Elimu na Taasisi zake.

(d)Eneo la Chakula,ni muda wa serikali kuitoa hifadhi ya Chakula hasa mahindi,ambayo kwa Takwimu tulizokuwa tunapewa kuwa tuna chakula cha ziada cha kutosha,kutolewa kwa mahindi kutafanya unafuu katika baadhi ya vyakula hasa katika wakati huu ambao hali ni mbaya.Ili bei za vyakula zisiwe juu sababu ya kisingizio cha Corona

(e)Hii ni kama Vita,ni wakati sasa wa Amiri Jeshi mkuu kuwa hadharani,kuongea na Taifa mara kwa mara na moja kwa moja.Kutumia Twits au njia nyingine ambayo si ya moja kwa moja ya wananchi kuona na kusikia sauti ya hisia za Amiri Jeshi mkuu,inaongeza kutokutilia mkazo kwa raia.Rais awe na kauli zisizoegemea sana mambo ya kiroho,bali kitaalamu na kiafya.Tunamuhitaji Mungu sana wakati huu,lakini kwa kutupa akili na utashi,Mungu alikwisha toa nafasi ya kuepukana na majanga kwa kuwasikiliza wataalamu aliowapa talanta mbalimbali katika sekta ya afya.

(f)Serikali itazame na kuwalinda wafanyakazi wa sekta rasmi,na hasa sekta binafsi katika mashule na makampuni,serikali itazame wafanyabiashara wenye anuani kamili walio na mikopo katika mabank,kusitishiwa madai ya mikopo kwa muda ambao biashara zao zimelala.

(g)Mwisho ni kwa Watanzania wote.Tujue kuwa ugonjwa huu upo,unauwa...Tusiwe na tamaa ya pesa na kupuyanga kwa kisingizio cha umasikini na kutafuta chakula.Hakuna umasikini mkubwa kama maradhi, Maradhi huleta dhiki na taabu.Tutoke na kuzunguka pale inapobidi...Tuwalinde wengine na tujilinde wenyewe.

Tulio ughaibuni na mahali gonjwa hili lilipoanzia kabla ya kufika Afrika,tumejilaumu sana kutokuchukua tahadhari ambazo tunadhani nyie mnayo nafasi ya kuzichukua sasa.Binafsi nimepoteza "co-workers" wanne na rafiki mpendwa mmoja,ambaye sikuweza hata kusema "Farewell thee",sababu amezikwa kama nguruwe aliyekufa kibudu.

Tujilinde na Tuwalinde wengine,COVID-19 inaweza kupiga kambi Afrika na kutuuwa kama kuku wa mdondi.
 
Naunga mkono hoja yako mkuu!!

Inaonekana kama serikali inaogopa kusitisha mikusanyiko kwenye nyumba za ibada kwa sababu wanazozifahamu wahusika.

Bado watawala wetu hawako makini kuongeza hatua za udhibiti hii inasikitisha sana.

Sasa ndio tunaona uwezo halisi wa viongozi wetu kuongoza nchi.
 
Rais kama anaweza aje asali kwenye hiyo mikusanyiko aone jinsi watu wanavyopumliana hewa chafu na ushuzi

Yaani watu weusi uwa wanaamini Rais akiongea hawezi kosea ila ukweli Magufuli anabugi sana. na j3 maambukizi yatakuwa maelfu.

Rais mshaurini vizuri.
 
Hao watumishi wa Mungu wanaoonekana kuitumia hii nafasi ya siku tatu za maombolezo kwa upande wangu siwezi kuwalaumu, kwasababu hiyo ndio kazi yao, hivyo tuwaache tu watekeleze wajibu wao.

Hapa ni vyema serikali ingeweka hata condition moja kwa waumini wanaoenda misikitini na makanisani, ni vyema kila mmoja awe na mask ili kujilinda yeye na kumlinda jirani yake wakati wa ibada.

Kusema watu wahudhurie ibada ila muda wa ibada ndio umepunguzwa hili kwangu halina maana, kwasababu sidhani kama huyo virus wa Corona anahitaji saa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, atakuwa ana -shift kwa muda mfupi zaidi, hivyo kusema tu muda wa ibada upunguzwe bado siioni kama njia nzuri ya kujikinga na maambukizi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu barafu umeandika vizuri sana...
Mi niongezee tu kuwa ni muda muafaka kwa Serikali kutoa tamko la kuzuia mashirika ya mifuko ya hifadhi ya jamii kupokea michango mipya ya wanachama wao... Bali michango hiyo ibaki sehemu ya mishahara ili kutunisha vipato vya wanachama hadi hapo hali itakapokuwa shwari...!!
Hii iende sambamba na kuizuia TRA kutoza kodi biashara au mishahara ambayo uingiza chini ya 2M kwa mwezi!
Hali ni mbaya sana!!
Kuhusu rais kuhutubia Taifa...
Nadhani ni muhimu sana lakini tumeshachanganywa vya kutosha... Bora aje mganga mkuu wa serikali aongee na taifa kitaalamu!!
Kusali na kuomba bila kuchukua tahadhari kwa matendo ni kupiga makelele tu!!
Kujikinga ni jukumu letu; serikali ifanye makubwa zaidi!!
 
barafu,

..kauli za bwana mkubwa siku zote huwa zina utata.

..pia bwana mkubwa hakutakiwa awaingilie viongozi wa DINI ktk masuala ya kuswali au kusali.

..bwana mkubwa alitakiwa abakie kuongoza serikali na kudili na suala hili kwa taratibu za kiserikali.
Tumefikisha maambukizi zaidi ya mia moja lakini bado hatuko makini kabisa, sijajua kuna ugumu gani kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima.
 
Uchambuzi mzuri.

Hii issue ya Corona imekuja ghafla sana, hivyo kuna mipango kadhaa ambayo kwa mtazamo wangu ni migumu.

Mfano. hapo ulipoitaka serikali iwalinde wafanyakazi wa sekta rasmi hasa binafsi, sijajua unazungumzia angle ipi, but kama ni serikali ku-provide stimulus package kwa wafanyakazi waliopoteza/kusitishiwa ajira zao sababu ya hili janga la Corona, sidhani kama serikali itaweza tekeleza hilo.


Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchambuzi mzuri.

Hii issue ya Corona imekuja ghafla sana, hivyo kuna mipango kadhaa ambayo kwa mtazamo wangu ni migumu.

Mfano. hapo ulipoitaka serikali iwalinde wafanyakazi wa sekta rasmi hasa binafsi, sijajua unazungumzia angle ipi, but kama ni serikali ku-provide stimulus package kwa wafanyakazi waliopoteza/kusitishiwa ajira zao sababu ya hili janga la Corona, sidhani kama serikali itaweza tekeleza hilo.


Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app

Serikali ikiamua haishindwi!
Tafuta comments zangu hapo juu uone wanavoweza kufanya na hali ikawa nafuu!!
 
Mkuu acha uvivu,utakufa kwa njaa shauri yako,manabii na wachungaji na maskofu kazi ya ni kuomba hivyo acha wachape kazi haka ka ugojwa ka corona ni kadogo sana
 
Back
Top Bottom