Kauli ya Rais kusali siku tatu imetafsiliwa kinyume,Makanisa yanafurika na kuongeza maambukizi. Serikali ichukue hatua

Wasalaam wana jamvi...Tuepushwe na janga hili.

Huko Korea Kusini,nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi mapema tu baada ya China,kuna mji wa Daegu,huu ni mji wa nne kwa ukubwa huko Korea Kusini,unapatikana Kusini mwa Korea Kusini.Hapa ndio alipatikana mgonjwa wa 31 kati ya wagonjwa wa mwanzo kugundulika na Corona.Mama huyu muumini wa (Huduma za Kiroho) wa kanisa la Shincheonji aligundulika baada ya kuwa amehudhuria kanisani zaidi ya mara 5 katika mlolongo wa majuma mawili.

Mji wa Daegu ikawa ndio "epicentre" ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona Korea Kusini.75% ya wagonjwa wote Korea kusini walitokea mji wa Daegu na 73% toka katika kanisa hili.

Hata baada ya Mama huyu,ambaye vyombo vya habari vimempa jina la "SuperSpreader Woman" kugundulika na dalili za Corona,bado aligoma kuchukuliwa vipimo,akazidi kwenda kanisani na kuambukiza wengine.Na waumini wengine walipotakiwa kwenda kupima,walikaidi kwa kuamini kuwa "Maombi na damu ya Yesu vitawaokoa".

Walizidi kwenda kanisani na kuambukizana.Baada ya mgonjwa huyu wa 31(Superspreader Woman),serikali iliamua kufunga makanisa,sehemu za starehe,massage centres na mahali pote pa mkusanyiko.Hii ikawa ni pamoja na kuufunga mji wa Daegu kwa kuzuia watu kuingia na kutoka.Mji huu kama ilivyo Wuhani China na Meli ya Diamond kule Japan,ukafungwa na watu wakabaki ndani bila kutoka nje.

Serikali ikatoa tamko kali kwa wote watakaokusanyika kwa ibada au mambo mengine,haikuzuia watu kusali ila ilisisitiza watu wasali wakiwa katika familia zao ndani ya nyumba.

Kiongozi wa Kanisa hili la maambukizi alipoona hali mbaya na watu wanakufa,akatoka kuomba radhi raia,akitoa mchango wa $10 milioni kama sehemu ya kusaidia kukabiliana na gonjwa hili.Serikali ikazikataa na ikaamua kumfungulia mashitaka kwa uzembe na kusababisha hatari ya uhai wa watu.

Tumeanza siku tatu za kusali na kuliombea Taifa,hali hii imepokewa kwa namna tofauti na mtazamo tofauti.Wale wenye huduma za kiroho wameanza kusema wanamuunga mkono Rais kuliombea Taifa,na wanatangaziana ratiba za mikesha na mfungo katika mkusanyiko wa makanisa yao.Huko Twitter na Instagram,Manabii na Mitume wameanza kutuma video wakiwa wamesongamana wakiomba na kusema wanamuunga mkono Rais.

Sasa Manabii na Mitume,wameanza kukusanya watu makanisani kwa kufuata kauli ya kuomba siku 3 aliyotoa Rais,na uinjilishaji huu mamboleo,wengi wanatuma kwenye mitandao na kum-tag msemaji wa Ikulu ili aone juhudi zao kuwa wanamuunga Rais.

Hili ni janga jingine.Huu ni mtihani mwingine ambapo kauli ya Rais inaweza kuchukuliwa kwa namna ya kuongeza misongamano.

Kama wenzetu walichukua hatua kali baada ya mgonjwa wa 31 tu,sisi mpaka sasa wagonjwa ni 140+ kwanini tusichukue hatua muhimu?

Hawa Manabii na Mitume wao hawaangalii sana taratibu za afya na kanuni zake,wao wanatazama mambo kwa imani na miujiza.Katika hili hatuitaji miujiza na maombi tu,tunapaswa kufuata kanuni zote za afya na kuheshimu ushauri wa wataalamu na si Wanasiasa.

Wengine wanadhani kufunga makanisa ni kuzuaia uhuru wa kuanudu...BIG NO!Na wengine wanaona kufunga makanisa na kuondoka uwezekano wa makusanyiko ya watoa sadaka na malimbuko!Ukisisitiza mkusanyiko wa ibada katikati ya janga hili,ni uuwaji!Pepo mchafu wa aina hii awatoke manabii na mitume wanaotazama sadaka na sio uhai wa waumini wao.Nyakati hizi ndio tunaweza kujua rangi halisi ya Mitume na Manabii wetu.

USHAURI:

(a)Kama ambavyo wenzetu waliifunga miji yenye maambukizi makubwa kusiwe na kuingia wala kutoka,sasa ni rasmi Mji kama Dsm unapaswa kuwa na "half lockdown".Kuruhusu magali ya chakula na mizigo tu.Mgonjwa alipatikana Lindi,ametokea Dsm na aligundulika ndani ya Basi.

(b) Mamlaka kuu itoe tamko kuzipumzisha sehemu za ibada,starehe na mikusanyiko katika miji mikubwa na hasa mji wa Dar es Salaam,sababu tuna case study kuwa nchi moja athirika,75% ya wagonjwa walitokea kanisani.Kufunga sehemu za ibada sio kuzuia uhuru wa kuabudu bali ni kuongeza nafasi ya watu kuwa na uhuru wa kuabudu katikati ya majanga yanayoweza kuwaangamiza watu sababu ya mikusanyiko.Pale Roma,Vatican,sasa hata Pope na Maaskofu pamoja na Mapadre hawatumii kikombe kimoja cha divai,maana mapadre wengi Italia wamekufa kwa Utamaduni wa kanisa wa kutumia Chalice moja na Chibolio moja kwenye misa,kumbe wakagundua Corona inaambukiza hata kwenye kikombe cha divai ambacho kiimani ndani yake ipo damu na mwili wa Yesu Kristo...Hii Corona inasambaa hata katika vyombo vilivyobeba mambo matakatifu(kiimani).

(c)Serikali kwa kutumia vyombo vyake Vikuu vya Habari kama Tv na Radio,viunde vipindi maalumu vya kimasomo kwa Watoto wa Chekechea mpaka Sekondari ya Upili na kuvirusha kila siku ili kufanya muendelezo wa kielimu kwa watoto wanapokuwa nyumbani.Huku kwenye nchi zilizoendelea,watoto wanaendelea kupata mafunzo kwa njia ya "Online" ili kufanya wasijisahau.Kwetu huko nyumbani teknolojia hii ni ngumu kutekelezeka vijijini.Radio na Tv vinaweza kuwa mbadala...Hii ndio kazi ya Wizara ya Elimu na Taasisi zake.

(d)Eneo la Chakula,ni muda wa serikali kuitoa hifadhi ya Chakula hasa mahindi,ambayo kwa Takwimu tulizokuwa tunapewa kuwa tuna chakula cha ziada cha kutosha,kutolewa kwa mahindi kutafanya unafuu katika baadhi ya vyakula hasa katika wakati huu ambao hali ni mbaya.Ili bei za vyakula zisiwe juu sababu ya kisingizio cha Corona

(e)Hii ni kama Vita,ni wakati sasa wa Amiri Jeshi mkuu kuwa hadharani,kuongea na Taifa mara kwa mara na moja kwa moja.Kutumia Twits au njia nyingine ambayo si ya moja kwa moja ya wananchi kuona na kusikia sauti ya hisia za Amiri Jeshi mkuu,inaongeza kutokutilia mkazo kwa raia.Rais awe na kauli zisizoegemea sana mambo ya kiroho,bali kitaalamu na kiafya.Tunamuhitaji Mungu sana wakati huu,lakini kwa kutupa akili na utashi,Mungu alikwisha toa nafasi ya kuepukana na majanga kwa kuwasikiliza wataalamu aliowapa talanta mbalimbali katika sekta ya afya.

(f)Serikali itazame na kuwalinda wafanyakazi wa sekta rasmi,na hasa sekta binafsi katika mashule na makampuni,serikali itazame wafanyabiashara wenye anuani kamili walio na mikopo katika mabank,kusitishiwa madai ya mikopo kwa muda ambao biashara zao zimelala.

(g)Mwisho ni kwa Watanzania wote.Tujue kuwa ugonjwa huu upo,unauwa...Tusiwe na tamaa ya pesa na kupuyanga kwa kisingizio cha umasikini na kutafuta chakula.Hakuna umasikini mkubwa kama maradhi,Maradhi huleta dhiki na taabu.Tutoke na kuzunguka pale inapobidi...Tuwalinde wengine na tujilinde wenyewe.

Tulio ughaibuni na mahali gonjwa hili lilipoanzia kabla ya kufika Afrika,tumejilaumu sana kutokuchukua tahadhari ambazo tunadhani nyie mnayo nafasi ya kuzichukua sasa.Binafsi nimepoteza "co-workers" wanne na rafiki mpendwa mmoja,ambaye sikuweza hata kusema "Farewell thee",sababu amezikwa kama nguruwe aliyekufa kibudu.

Tujilinde na Tuwalinde wengine,COVID-19 inaweza kupiga kambi Afrika na kutuuwa kama kuku wa mdondi.
Nyerere hakukoseaga aliposemaga moja ya maadui wa taifa ni ujinga. Sasa hao wanaoenda kanisani, dah!
 
Mkuu barafu umeandika vizuri sana...
Mi niongezee tu kuwa ni muda muafaka kwa Serikali kutoa tamko la kuzuia mashirika ya mifuko ya hifadhi ya jamii kupokea michango mipya ya wanachama wao... Bali michango hiyo ibaki sehemu ya mishahara ili kutunisha vipato vya wanachama hadi hapo hali itakapokuwa shwari...!!
Hii iende sambamba na kuizuia TRA kutoza kodi biashara au mishahara ambayo uingiza chini ya 2M kwa mwezi!
Hali ni mbaya sana!!
Kuhusu rais kuhutubia Taifa...
Nadhani ni muhimu sana lakini tumeshachanganywa vya kutosha... Bora aje mganga mkuu wa serikali aongee na taifa kitaalamu!!
Kusali na kuomba bila kuchukua tahadhari kwa matendo ni kupiga makelele tu!!
Kujikinga ni jukumu letu; serikali ifanye makubwa zaidi!!
Ndio maana naona ni ngumu, kwasababu ukisema serikali izuie hayo makato ya hayo mashirika, usije shangaa serikali nayo inalia njaa siku sio nyingi, kwasababu mara nyingi tumeona hizo pesa zikitumika kwa matumizi ambayo hayakukusudiwa, hii inaonesha serikali nayo inategemea pata kitu toka kwenye hayo makato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia wasemaji wachujwe, angalau wapewe kipaumbele wenye fani husika tofauti na wanasiasa,kwa mfano Mganga mkuu wa Mkoa,Mganga Mkuu wa Wilaya etc.
Harafu naibu rais afanye kazi gani?
 
Umeongea mambo ya muhimu sana ambayo viongozi wetu wakizingatia tunaweza nusuru taifa na hili janga.
 
Ndio maana naona ni ngumu, kwasababu ukisema serikali izuie hayo makato ya hayo mashirika, usije shangaa serikali nayo inalia njaa siku sio nyingi, kwasababu mara nyingi tumeona hizo pesa zikitumika kwa matumizi ambayo hayakukusudiwa, hii inaonesha serikali nayo inategemea pata kitu toka kwenye hayo makato.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hela zipo in Magufuli voice
 
Umetoa ushauri mzuri.

Sasa wanadamu tunakula jeuri na kiburi chetu. Akili zimefika mwisho, matumaini hatuyaoni kabisa. Hata dalili ya tiba ya Corona hakuna!

Kiburi cha uzima wetu dunia nzima tumenywea.
Ugonjwa unatuchekecha tu ila hata waliobakia hawako salama! Na roho zao ziko juu juu!

Raisi kaongea jambo jema sana sana. Busara zimetumika sana kwake kutangaza watu wazidi kumlilia Mungu tu.

Uovu wetu ni mkubwa sana mbele za Mungu. Naamini wanaoamini katika dini zetu wanajua hilo. Heri kama ni kufa tufe ila tukiwa salama mbele za Mungu wetu. Tuombe toba ya kweli na tuzinawe dhambi zetu na si kunawa mikono tu.
Kwasababu ya uovu wetu, ndiyo maana unaona hofu na woga vimetawala dunia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akina gwajima wanataman siku za maombi ziongezwe angalau Kwa wiki 2 ili waendelee kupiga mpunga,Kwa kifupi hili tamko la maombi ya siku3 ni fursa kubwa Kwa manabii na mitume kwasabb MH magufuli hajasema tuombee taifa tukiwa Kwenye nyumba za ibada Bali tunaweza kufanya ibada hata Nyumbani...

Kwa kifupi hawa matapeli wa Imani wamegeuza kauli ya magufuli na kuwakusanya watu Kwenye nyumba za ibada
 
Ukifuatilia takwimu za Uganda ukalinganisha na za hapa kwetu, utaona umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti mapema kama walivyofanya waganda.

Mungu atusaidie. Huu ugonjwa sio kama homa ya dengue
 
UKO SAHIHI KABISA,NASHANGAA VIONGOZI WA DINI KUSHANGILIA

Viongozi wa dini wanashangilia kwakuwa wao wanategemea sadaka, hivyo wanaona wanasiasa wamewahakikishia kuendelea kupata sadaka, lakini kiukweli wanasiasa wanatoa nafasi kwa hao viongozi wa dini kama sehemu ya kuwaziba midomo viongozi wa dini, pindi watakapochezea katiba viongozi wa dini nao wakae kimya. Nyumba za ibada ni kwa ajili ya imani, lakini hakuna dini au dhehebu lolote linaloweza kutibu ugonjwa wowote. Nawashangaa sana viongozi wa dini kuendelea na ibada za kitapeli wakati wanajua fika hawana uwezo wa kutibu au kuongea na huyo Mungu kuzuia ugonjwa au tatizo lolote.
 
Viongozi wa dini wanafurahia sadaka nyingi waumini wakijaa. Hii sadaka itawatokea puani.
 
Hao watumishi wa Mungu wanaoonekana kuitumia hii nafasi ya siku tatu za maombolezo kwa upande wangu siwezi kuwalaumu, kwasababu hiyo ndio kazi yao, hivyo tuwaache tu watekeleze wajibu wao.

Hapa ni vyema serikali ingeweka hata condition moja kwa waumini wanaoenda misikitini na makanisani, ni vyema kila mmoja awe na mask ili kujilinda yeye na kumlinda jirani yake wakati wa ibada.

Kusema watu wahudhurie ibada ila muda wa ibada ndio umepunguzwa hili kwangu halina maana, kwasababu sidhani kama huyo virus wa Corona anahitaji saa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, atakuwa ana -shift kwa muda mfupi zaidi, hivyo kusema tu muda wa ibada upunguzwe bado siioni kama njia nzuri ya kujikinga na maambukizi.


Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hamna kwenda kwenye nyumba yoyote ya ibada, hakuna mtu yoyote aliyewahi kupona ugonjwa wowote kwa kwenda kwenye nyumba ya ibada, na hakuna yoyote atakayeweza kuponywa na hayo maombi. Hizo nyumba za ibada ni sehemu ya kuwaweka waumini vizuri kisaikolojia na sio zaidi ya hapo. Hakuna Mungu yoyote anayeweza kuwasikiliza wala kutoa msaada kwa wazembe.
 
Naomba nianze kwa kukupongeza kwa kueleza tatizo hili la ugonjwa wa COVID19 na usaambaaji wa virusi hivi kwa lugha nzuri kabisa na yenye kueleweka

Ujumbe huu unafaa kuwa copy pasted na kuwa shared kwa magroup ya whatsapp ili watu waelewe ukubwa wa tatizo na kuchukua hatua za kujikinga
Tatizo letu watanzania ni wagumu sana wa kuelewa na kuchambua mambo. wengi wetu hatutumii common sense na learned experience kuweza kutatua matatizo yanayotukabili. bado watu wengi wanadharau huu ugonjwa na ndio maana unaona huko mitaaani kumejaa business as usual, yaani hamna hata kujiongeza. watu tuna akili za kushikiwa mpaka tuje shikiwa bakora na mitutu kulinda uhai wetu wenyewe , au mtu afiwe na mtu wake wa karibu kwa tatizo hili ndio akili zinatukaa sawa...
tunahitaji watu kuelimishwa sana sana sana, na kuomba viongozi wetu wasitume meseji zenye kuleta mikanganyiko na kudogosha ukubwa wa tatizo
CORONA IS REAL
COVID 19 IS REAL

TUSISUBIRI KUZIKA WAPENDWA WETU NDIO TUSTUKE.. TUCHUKUE HATUA SASA!!
 
Viongozi wa dini hasa wa kikristu wamegeuza waumini wao kuwa watumwa wa nyumba za ibada hata pale hatari ya dhahiri inapotokea. Ni wachumia tumbo wanaojali sadaka kuliko uhai wa mtu. Usiombe mtu anazikwa bila hata taarifa zake kujulikana. Na mwanzoni kabisa niliwaonya watu kupitia humu Jf kuwa ugonjwa huu ukiamua kuweka kambi kwenye mji basi mnazika watu hadi mnachoka kuzika mnaanza kufukia halaiki kwenye shimo. Nikawaambia kuwa huu ugonjwa ukiudharau na kuudhihaki hadharani nao unakutenda vilivyo hadharani.

Kiukweli baadhi ya maneno aliyoongea Rais Magufuli kuhusu huu ugonjwa ni ya kufedhehesha mno na yanashangaza kutamkwa na kiongozi mkuu wa nchi ambaye kwa makusudi ameamua kujifungia na kuwaacha watu wake.
 
Back
Top Bottom