Kauli ya Rais kusali siku tatu imetafsiliwa kinyume,Makanisa yanafurika na kuongeza maambukizi. Serikali ichukue hatua

barafu ahsante kwa somo lililojaa tahadhari mkuu, najua hata kwenye hili bandiko watu wataleta siasa kama ambavyo kauli ya mheshimiwa inatumika ndivyo sivyo na hakuna wa kurekebisha.

Pia ikiwezekana wafanyakazi wa hospitali zote wapewe au kuwezeshwa vifaa vya kujikinga na maambukizi pale wanapohudumia wagonjwa wa aina zote hata kama sio kituo cha kukabiliana na Covid 19. Kama tunavyojua dalili hazionekani kusnzia siku 14 na wakati huo mgonjwa anaambukiza wengine. Inamaana endapo huyo mgonjwa asiye na dalili za moja kwa moja akienda kituo au hospitali yeyote anahatarisha watakaomhudumia na wagonjwa wa maradhi mengine.

Pia sijui watatumia njia gani kuoulizia vyombo vya usafiri hasa mabasi na boat kabla ya abiria kupanda na abiria kutumia vitakasa mikono wakati wa kuingia kwenye vyombo.

Tuendelee kuchukua tahadhari.
 
Bila shaka hata sisi raia wa kawaida ni haki yetu kushauri chochote juu ya janga la korona.

Rais katuambia tumwombe Mungu ni sawa na siyo tu siku tatu, nashauri hata kwa miezi sita.

Hata hivyo wakubwa wanaposema tuendelee kuchapa kazi na kuchukua tahadhari, hiyo ya kunawa mikono na kuepuka misongamano inatosha?

Nadhani serikali ina wajibu wa kuzalisha barakoa kwa wingi na kuzigawa bure kwa kila kaya kwa kuanzia miji yote ya mikoa na wilaya nchini.

Jinsi tahadhari zinavyotolewa ni kama kila mtu ajiongeze. Watu watajiongeza kwa kuikimbia miji, serikali izuie watu kuikimbia miji. Heri nusu shari kuliko shari kamili.

Raia tuelekezwe kutengeneza barakoa zetu wenyewe za ki sidosido kama inasaidia chochote. Isifike mahali wakubwa wakachanganyikiwa sisi waongozwa tutachanganyikiwa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana jamvi...Tuepushwe na janga hili.

Huko Korea Kusini,nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi mapema tu baada ya China,kuna mji wa Daegu,huu ni mji wa nne kwa ukubwa huko Korea Kusini,unapatikana Kusini mwa Korea Kusini.Hapa ndio alipatikana mgonjwa wa 31 kati ya wagonjwa wa mwanzo kugundulika na Corona.Mama huyu muumini wa (Huduma za Kiroho) wa kanisa la Shincheonji aligundulika baada ya kuwa amehudhuria kanisani zaidi ya mara 5 katika mlolongo wa majuma mawili.

Mji wa Daegu ikawa ndio "epicentre" ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona Korea Kusini.75% ya wagonjwa wote Korea kusini walitokea mji wa Daegu na 73% toka katika kanisa hili.

Hata baada ya Mama huyu,ambaye vyombo vya habari vimempa jina la "SuperSpreader Woman" kugundulika na dalili za Corona,bado aligoma kuchukuliwa vipimo,akazidi kwenda kanisani na kuambukiza wengine.Na waumini wengine walipotakiwa kwenda kupima,walikaidi kwa kuamini kuwa "Maombi na damu ya Yesu vitawaokoa".

Walizidi kwenda kanisani na kuambukizana.Baada ya mgonjwa huyu wa 31(Superspreader Woman),serikali iliamua kufunga makanisa,sehemu za starehe,massage centres na mahali pote pa mkusanyiko.Hii ikawa ni pamoja na kuufunga mji wa Daegu kwa kuzuia watu kuingia na kutoka.Mji huu kama ilivyo Wuhani China na Meli ya Diamond kule Japan,ukafungwa na watu wakabaki ndani bila kutoka nje.

Serikali ikatoa tamko kali kwa wote watakaokusanyika kwa ibada au mambo mengine,haikuzuia watu kusali ila ilisisitiza watu wasali wakiwa katika familia zao ndani ya nyumba.

Kiongozi wa Kanisa hili la maambukizi alipoona hali mbaya na watu wanakufa,akatoka kuomba radhi raia,akitoa mchango wa $10 milioni kama sehemu ya kusaidia kukabiliana na gonjwa hili.Serikali ikazikataa na ikaamua kumfungulia mashitaka kwa uzembe na kusababisha hatari ya uhai wa watu.

Tumeanza siku tatu za kusali na kuliombea Taifa,hali hii imepokewa kwa namna tofauti na mtazamo tofauti.Wale wenye huduma za kiroho wameanza kusema wanamuunga mkono Rais kuliombea Taifa,na wanatangaziana ratiba za mikesha na mfungo katika mkusanyiko wa makanisa yao.Huko Twitter na Instagram,Manabii na Mitume wameanza kutuma video wakiwa wamesongamana wakiomba na kusema wanamuunga mkono Rais.

Sasa Manabii na Mitume,wameanza kukusanya watu makanisani kwa kufuata kauli ya kuomba siku 3 aliyotoa Rais,na uinjilishaji huu mamboleo,wengi wanatuma kwenye mitandao na kum-tag msemaji wa Ikulu ili aone juhudi zao kuwa wanamuunga Rais.

Hili ni janga jingine.Huu ni mtihani mwingine ambapo kauli ya Rais inaweza kuchukuliwa kwa namna ya kuongeza misongamano.

Kama wenzetu walichukua hatua kali baada ya mgonjwa wa 31 tu,sisi mpaka sasa wagonjwa ni 140+ kwanini tusichukue hatua muhimu?

Hawa Manabii na Mitume wao hawaangalii sana taratibu za afya na kanuni zake,wao wanatazama mambo kwa imani na miujiza.Katika hili hatuitaji miujiza na maombi tu,tunapaswa kufuata kanuni zote za afya na kuheshimu ushauri wa wataalamu na si Wanasiasa.

Wengine wanadhani kufunga makanisa ni kuzuaia uhuru wa kuanudu...BIG NO!Na wengine wanaona kufunga makanisa na kuondoka uwezekano wa makusanyiko ya watoa sadaka na malimbuko!Ukisisitiza mkusanyiko wa ibada katikati ya janga hili,ni uuwaji!Pepo mchafu wa aina hii awatoke manabii na mitume wanaotazama sadaka na sio uhai wa waumini wao.Nyakati hizi ndio tunaweza kujua rangi halisi ya Mitume na Manabii wetu.

USHAURI:

(a)Kama ambavyo wenzetu waliifunga miji yenye maambukizi makubwa kusiwe na kuingia wala kutoka,sasa ni rasmi Mji kama Dsm unapaswa kuwa na "half lockdown".Kuruhusu magali ya chakula na mizigo tu.Mgonjwa alipatikana Lindi,ametokea Dsm na aligundulika ndani ya Basi.

(b) Mamlaka kuu itoe tamko kuzipumzisha sehemu za ibada,starehe na mikusanyiko katika miji mikubwa na hasa mji wa Dar es Salaam,sababu tuna case study kuwa nchi moja athirika,75% ya wagonjwa walitokea kanisani.Kufunga sehemu za ibada sio kuzuia uhuru wa kuabudu bali ni kuongeza nafasi ya watu kuwa na uhuru wa kuabudu katikati ya majanga yanayoweza kuwaangamiza watu sababu ya mikusanyiko.Pale Roma,Vatican,sasa hata Pope na Maaskofu pamoja na Mapadre hawatumii kikombe kimoja cha divai,maana mapadre wengi Italia wamekufa kwa Utamaduni wa kanisa wa kutumia Chalice moja na Chibolio moja kwenye misa,kumbe wakagundua Corona inaambukiza hata kwenye kikombe cha divai ambacho kiimani ndani yake ipo damu na mwili wa Yesu Kristo...Hii Corona inasambaa hata katika vyombo vilivyobeba mambo matakatifu(kiimani).

(c)Serikali kwa kutumia vyombo vyake Vikuu vya Habari kama Tv na Radio,viunde vipindi maalumu vya kimasomo kwa Watoto wa Chekechea mpaka Sekondari ya Upili na kuvirusha kila siku ili kufanya muendelezo wa kielimu kwa watoto wanapokuwa nyumbani.Huku kwenye nchi zilizoendelea,watoto wanaendelea kupata mafunzo kwa njia ya "Online" ili kufanya wasijisahau.Kwetu huko nyumbani teknolojia hii ni ngumu kutekelezeka vijijini.Radio na Tv vinaweza kuwa mbadala...Hii ndio kazi ya Wizara ya Elimu na Taasisi zake.

(d)Eneo la Chakula,ni muda wa serikali kuitoa hifadhi ya Chakula hasa mahindi,ambayo kwa Takwimu tulizokuwa tunapewa kuwa tuna chakula cha ziada cha kutosha,kutolewa kwa mahindi kutafanya unafuu katika baadhi ya vyakula hasa katika wakati huu ambao hali ni mbaya.Ili bei za vyakula zisiwe juu sababu ya kisingizio cha Corona

(e)Hii ni kama Vita,ni wakati sasa wa Amiri Jeshi mkuu kuwa hadharani,kuongea na Taifa mara kwa mara na moja kwa moja.Kutumia Twits au njia nyingine ambayo si ya moja kwa moja ya wananchi kuona na kusikia sauti ya hisia za Amiri Jeshi mkuu,inaongeza kutokutilia mkazo kwa raia.Rais awe na kauli zisizoegemea sana mambo ya kiroho,bali kitaalamu na kiafya.Tunamuhitaji Mungu sana wakati huu,lakini kwa kutupa akili na utashi,Mungu alikwisha toa nafasi ya kuepukana na majanga kwa kuwasikiliza wataalamu aliowapa talanta mbalimbali katika sekta ya afya.

(f)Serikali itazame na kuwalinda wafanyakazi wa sekta rasmi,na hasa sekta binafsi katika mashule na makampuni,serikali itazame wafanyabiashara wenye anuani kamili walio na mikopo katika mabank,kusitishiwa madai ya mikopo kwa muda ambao biashara zao zimelala.

(g)Mwisho ni kwa Watanzania wote.Tujue kuwa ugonjwa huu upo,unauwa...Tusiwe na tamaa ya pesa na kupuyanga kwa kisingizio cha umasikini na kutafuta chakula.Hakuna umasikini mkubwa kama maradhi, Maradhi huleta dhiki na taabu.Tutoke na kuzunguka pale inapobidi...Tuwalinde wengine na tujilinde wenyewe.

Tulio ughaibuni na mahali gonjwa hili lilipoanzia kabla ya kufika Afrika,tumejilaumu sana kutokuchukua tahadhari ambazo tunadhani nyie mnayo nafasi ya kuzichukua sasa.Binafsi nimepoteza "co-workers" wanne na rafiki mpendwa mmoja,ambaye sikuweza hata kusema "Farewell thee",sababu amezikwa kama nguruwe aliyekufa kibudu.

Tujilinde na Tuwalinde wengine,COVID-19 inaweza kupiga kambi Afrika na kutuuwa kama kuku wa mdondi.
Ninatamani watanzania wote wanaofahamu kusoma wangesoma hili andiko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hamna kwenda kwenye nyumba yoyote ya ibada, hakuna mtu yoyote aliyewahi kupona ugonjwa wowote kwa kwenda kwenye nyumba ya ibada, na hakuna yoyote atakayeweza kuponywa na hayo maombi. Hizo nyumba za ibada ni sehemu ya kuwaweka waumini vizuri kisaikolojia na sio zaidi ya hapo. Hakuna Mungu yoyote anayeweza kuwasikiliza wala kutoa msaada kwa wazembe.
Kumbuka nyumba za ibada zipo siku zote, na sio wote wanaokwenda huko shida yao ni Corona, wengine wana matatizo yao binafsi.

Hivyo hata hao bado wanaihitaji hiyo "pschological relief" unayoizungumzia, japo ni vyema wakienda huko kanisani wachukue tahadhari za kujikinga dhidi ya Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja yako mkuu!!

Inaonekana kama serikali inaogopa kusitisha mikusanyiko kwenye nyumba za ibada kwa sababu wanazozifahamu wahusika.

Bado watawala wetu hawako makini kuongeza hatua za udhibiti hii inasikitisha sana.

Sasa ndio tunaona uwezo halisi wa viongozi wetu kuongoza nchi.
Kiongozi bora uwa anaonekana kwenye matatizo, huyu wetu toka lile tetemeko la kagera mpama hili la corona anasikitisha sana, huyu endapo angekua kiongozi kipindi cha vita dhidi ya nduli amini nadhani leo tungekua koloni la uganda
Leo ktk habari ya tbc nimemsikia sheikh mmoja uko tanga anasema eti jiwe ni chaguo la mungu, nikacheka peke angu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana jamvi...Tuepushwe na janga hili.

Huko Korea Kusini,nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi mapema tu baada ya China,kuna mji wa Daegu,huu ni mji wa nne kwa ukubwa huko Korea Kusini,unapatikana Kusini mwa Korea Kusini.Hapa ndio alipatikana mgonjwa wa 31 kati ya wagonjwa wa mwanzo kugundulika na Corona.Mama huyu muumini wa (Huduma za Kiroho) wa kanisa la Shincheonji aligundulika baada ya kuwa amehudhuria kanisani zaidi ya mara 5 katika mlolongo wa majuma mawili.

Mji wa Daegu ikawa ndio "epicentre" ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona Korea Kusini.75% ya wagonjwa wote Korea kusini walitokea mji wa Daegu na 73% toka katika kanisa hili.

Hata baada ya Mama huyu,ambaye vyombo vya habari vimempa jina la "SuperSpreader Woman" kugundulika na dalili za Corona,bado aligoma kuchukuliwa vipimo,akazidi kwenda kanisani na kuambukiza wengine.Na waumini wengine walipotakiwa kwenda kupima,walikaidi kwa kuamini kuwa "Maombi na damu ya Yesu vitawaokoa".

Walizidi kwenda kanisani na kuambukizana.Baada ya mgonjwa huyu wa 31(Superspreader Woman),serikali iliamua kufunga makanisa,sehemu za starehe,massage centres na mahali pote pa mkusanyiko.Hii ikawa ni pamoja na kuufunga mji wa Daegu kwa kuzuia watu kuingia na kutoka.Mji huu kama ilivyo Wuhani China na Meli ya Diamond kule Japan,ukafungwa na watu wakabaki ndani bila kutoka nje.

Serikali ikatoa tamko kali kwa wote watakaokusanyika kwa ibada au mambo mengine,haikuzuia watu kusali ila ilisisitiza watu wasali wakiwa katika familia zao ndani ya nyumba.

Kiongozi wa Kanisa hili la maambukizi alipoona hali mbaya na watu wanakufa,akatoka kuomba radhi raia,akitoa mchango wa $10 milioni kama sehemu ya kusaidia kukabiliana na gonjwa hili.Serikali ikazikataa na ikaamua kumfungulia mashitaka kwa uzembe na kusababisha hatari ya uhai wa watu.

Tumeanza siku tatu za kusali na kuliombea Taifa,hali hii imepokewa kwa namna tofauti na mtazamo tofauti.Wale wenye huduma za kiroho wameanza kusema wanamuunga mkono Rais kuliombea Taifa,na wanatangaziana ratiba za mikesha na mfungo katika mkusanyiko wa makanisa yao.Huko Twitter na Instagram,Manabii na Mitume wameanza kutuma video wakiwa wamesongamana wakiomba na kusema wanamuunga mkono Rais.

Sasa Manabii na Mitume,wameanza kukusanya watu makanisani kwa kufuata kauli ya kuomba siku 3 aliyotoa Rais,na uinjilishaji huu mamboleo,wengi wanatuma kwenye mitandao na kum-tag msemaji wa Ikulu ili aone juhudi zao kuwa wanamuunga Rais.

Hili ni janga jingine.Huu ni mtihani mwingine ambapo kauli ya Rais inaweza kuchukuliwa kwa namna ya kuongeza misongamano.

Kama wenzetu walichukua hatua kali baada ya mgonjwa wa 31 tu,sisi mpaka sasa wagonjwa ni 140+ kwanini tusichukue hatua muhimu?

Hawa Manabii na Mitume wao hawaangalii sana taratibu za afya na kanuni zake,wao wanatazama mambo kwa imani na miujiza.Katika hili hatuitaji miujiza na maombi tu,tunapaswa kufuata kanuni zote za afya na kuheshimu ushauri wa wataalamu na si Wanasiasa.

Wengine wanadhani kufunga makanisa ni kuzuaia uhuru wa kuanudu...BIG NO!Na wengine wanaona kufunga makanisa na kuondoka uwezekano wa makusanyiko ya watoa sadaka na malimbuko!Ukisisitiza mkusanyiko wa ibada katikati ya janga hili,ni uuwaji!Pepo mchafu wa aina hii awatoke manabii na mitume wanaotazama sadaka na sio uhai wa waumini wao.Nyakati hizi ndio tunaweza kujua rangi halisi ya Mitume na Manabii wetu.

USHAURI:

(a)Kama ambavyo wenzetu waliifunga miji yenye maambukizi makubwa kusiwe na kuingia wala kutoka,sasa ni rasmi Mji kama Dsm unapaswa kuwa na "half lockdown".Kuruhusu magali ya chakula na mizigo tu.Mgonjwa alipatikana Lindi,ametokea Dsm na aligundulika ndani ya Basi.

(b) Mamlaka kuu itoe tamko kuzipumzisha sehemu za ibada,starehe na mikusanyiko katika miji mikubwa na hasa mji wa Dar es Salaam,sababu tuna case study kuwa nchi moja athirika,75% ya wagonjwa walitokea kanisani.Kufunga sehemu za ibada sio kuzuia uhuru wa kuabudu bali ni kuongeza nafasi ya watu kuwa na uhuru wa kuabudu katikati ya majanga yanayoweza kuwaangamiza watu sababu ya mikusanyiko.Pale Roma,Vatican,sasa hata Pope na Maaskofu pamoja na Mapadre hawatumii kikombe kimoja cha divai,maana mapadre wengi Italia wamekufa kwa Utamaduni wa kanisa wa kutumia Chalice moja na Chibolio moja kwenye misa,kumbe wakagundua Corona inaambukiza hata kwenye kikombe cha divai ambacho kiimani ndani yake ipo damu na mwili wa Yesu Kristo...Hii Corona inasambaa hata katika vyombo vilivyobeba mambo matakatifu(kiimani).

(c)Serikali kwa kutumia vyombo vyake Vikuu vya Habari kama Tv na Radio,viunde vipindi maalumu vya kimasomo kwa Watoto wa Chekechea mpaka Sekondari ya Upili na kuvirusha kila siku ili kufanya muendelezo wa kielimu kwa watoto wanapokuwa nyumbani.Huku kwenye nchi zilizoendelea,watoto wanaendelea kupata mafunzo kwa njia ya "Online" ili kufanya wasijisahau.Kwetu huko nyumbani teknolojia hii ni ngumu kutekelezeka vijijini.Radio na Tv vinaweza kuwa mbadala...Hii ndio kazi ya Wizara ya Elimu na Taasisi zake.

(d)Eneo la Chakula,ni muda wa serikali kuitoa hifadhi ya Chakula hasa mahindi,ambayo kwa Takwimu tulizokuwa tunapewa kuwa tuna chakula cha ziada cha kutosha,kutolewa kwa mahindi kutafanya unafuu katika baadhi ya vyakula hasa katika wakati huu ambao hali ni mbaya.Ili bei za vyakula zisiwe juu sababu ya kisingizio cha Corona

(e)Hii ni kama Vita,ni wakati sasa wa Amiri Jeshi mkuu kuwa hadharani,kuongea na Taifa mara kwa mara na moja kwa moja.Kutumia Twits au njia nyingine ambayo si ya moja kwa moja ya wananchi kuona na kusikia sauti ya hisia za Amiri Jeshi mkuu,inaongeza kutokutilia mkazo kwa raia.Rais awe na kauli zisizoegemea sana mambo ya kiroho,bali kitaalamu na kiafya.Tunamuhitaji Mungu sana wakati huu,lakini kwa kutupa akili na utashi,Mungu alikwisha toa nafasi ya kuepukana na majanga kwa kuwasikiliza wataalamu aliowapa talanta mbalimbali katika sekta ya afya.

(f)Serikali itazame na kuwalinda wafanyakazi wa sekta rasmi,na hasa sekta binafsi katika mashule na makampuni,serikali itazame wafanyabiashara wenye anuani kamili walio na mikopo katika mabank,kusitishiwa madai ya mikopo kwa muda ambao biashara zao zimelala.

(g)Mwisho ni kwa Watanzania wote.Tujue kuwa ugonjwa huu upo,unauwa...Tusiwe na tamaa ya pesa na kupuyanga kwa kisingizio cha umasikini na kutafuta chakula.Hakuna umasikini mkubwa kama maradhi, Maradhi huleta dhiki na taabu.Tutoke na kuzunguka pale inapobidi...Tuwalinde wengine na tujilinde wenyewe.

Tulio ughaibuni na mahali gonjwa hili lilipoanzia kabla ya kufika Afrika,tumejilaumu sana kutokuchukua tahadhari ambazo tunadhani nyie mnayo nafasi ya kuzichukua sasa.Binafsi nimepoteza "co-workers" wanne na rafiki mpendwa mmoja,ambaye sikuweza hata kusema "Farewell thee",sababu amezikwa kama nguruwe aliyekufa kibudu.

Tujilinde na Tuwalinde wengine,COVID-19 inaweza kupiga kambi Afrika na kutuuwa kama kuku wa mdondi.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, .
Wanna siasa wanapoamuwa kujivika koti la waana taaluma mtokeo yake itakuwa Ni msiba wanchi nzima
 
Bams,
Pangekuwepo na wasaidizi wa rais, wakasoma hii kitu uliyoweka hapa, na wao wakaichukua na kumpelekea na kumsihi wayajadili yaliyomo...

Sina la zaidi ya hapo. Nitachafua uzi mzuri kabisa.
 
Pandemics huwa hazichagui kama hii ya ugonjwa wa ndui Afrika Asia na Ulaya. mwanadamu bado anayo kumbukumbu yake, sasa ukiziona nchi zinachukua tahadhari ya hali ya juu usidharau tunakuomba Mkuu wetu wa Nchi usidharau hatujui na hili janga la Corona nalo litatufikisha sehemu gani.

smallpox_orig_high.jpg
Child_with_Smallpox_Bangladesh.jpg
VZ3UKQDZ3JHNTCMDBXBS36F5GU.jpg
 
Jamani rais hajakosea, yeye sio wakwanza kutoa wito, hata Trump alitoa...kilichokosekana ni namna bora ya kufanikisha maombi yaani kuepuka mikusanyiko
barafu,

..kauli za bwana mkubwa siku zote huwa zina utata.

..pia bwana mkubwa hakutakiwa awaingilie viongozi wa DINI ktk masuala ya kuswali au kusali.

..bwana mkubwa alitakiwa abakie kuongoza serikali na kudili na suala hili kwa taratibu za kiserikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said barafu for a very useful post.It has became rare nowdays to find a thread well narrated,analysed and arranged like this here in JF...Still few credible people can make JF reputation to rise again..
 
Back
Top Bottom