Kauli ya Ole Medeye itazamwe

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
JANA chombo kimoja cha habari kilimkariri Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye, akisema kuwa kampuni moja imewahi kumpa dola za Marekani 800,000 (sawa na takriban shilingi bilioni moja) za hongo ikitaka atoe upendeleo katika kugawa eneo.

Kilichotufanya hadi kufikia hatua ya kuandika tahariri hii ni kitendo cha naibu waziri huyo kutoi taja kampuni iliyotaka kumpa hongo hiyo, eneo ambalo lilihusika na hatua ambazo aliichukulia.

Kauli hiyo imetushangaza kwa sababu, Ole Medeye kama kiongozi, anafahamu kwamba kitendo kilichofanywa na kampuni hiyo ni kosa na yeye kukaa bila kuchukua hatua pia ni kosa.

Sisi Tanzania Daima tunajiuliza, kama Ole Medeye ambaye ni mfano wa kuigwa amelichukulia jambo hilo kimzaha, je, anatoa somo gani kwa watu wengine?

Sote tunafahamu ya kwamba kuna migogoro mingi ya ardhi katika nchi yetu ambayo inahitaji mapinduzi ya kweli katika kuishughulikia.

Wakati tukiwa katika wimbi la migogoro hiyo, inashangaza kusikia bado kuna watu ambao wanataka kupitia njia za mkato ili kunyang'anya haki za watu wengine kwa kupewa upendeleo.

Cha ajabu, naibu waziri anayeongoza wizara nyeti ya serikali analiacha jambo hilo lipite hivi hivi bila kuchukua hatua stahiki, ili uwe mfano kwa watu wengine wenye tabia na mwenendo wa kampuni iliyotaka kumpa hongo ya shilingi bilioni moja.

Sisi Tanzania Daima kama chombo huru cha habari, tunaamini njia sahihi ya kuanza kupunguza migogoro ya ardhi inayoikabili nchi yetu sasa hivi ni kuanza kupambana na rushwa.

Tunasema hayo kwa sababu rushwa imekuwa ni kikwazo kikubwa kinachochangia migogoro mingi ya ardhi.

Kuna baadhi ya watu leo hii wamepokonywa haki yao ya kumiliki ardhi kwa sababu tu kuna mtu mwenye pesa aliwarubuni viongozi nao wakabariki dhambi hiyo.

Kutokana na hilo, kwanza, tunamtaka naibu waziri kuiweka hadharani kampuni anayodai kwamba ilitaka kumpa hongo ya sh bilioni moja.

Pili, tunahitaji kusikia hatua ambazo ataichukulia, na asipofanya hivyo tutakosa imani naye kama naibu waziri wa Ardhi ambaye kwa nafasi yake anaweza kushughulikia migogoro ya ardhi kwa mamlaka makubwa, hasa katika eneo la rushwa ambalo limekuwa kikwazo kikubwa.

Tatu, tunaamini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesikia kauli ya naibu waziri huyo wa Ardhi na tunaamini itachukua hatua zinazostahili ili kuisaidia wizara katika kushughulikia migogoro ya ardhi inayoanzia kwenye rushwa.

Tunaamini Naibu Waziri Ole Medeye kama kweli kwa kushirikiana na Waziri wake, Anna Tibaijuka, wanataka kuleta mageuzi katika wizara hiyo ambayo baadhi wanaiita ya migogoro ya ardhi, atoe ushirikiano wake kwa kuitaja kampuni hiyo na nyingine kama zipo ambazo hajazisema, zilizoonesha kutoa hongo kwa nia ya kunyang'anya haki za wengine ili ziweze kuchukuliwa hatua.

Ole Medeye asipofanya hivyo, tutakosa imani na yeye kama kiongozi aliyepewa wadhifa na mamlaka ya kushughulikia mambo ya ardhi na maendeleo ya makazi kutekeleza wajibu wake kwa malengo yaliyokusudiwa.
 
mnaona viongozi wa nchi hii??akiwa kama kiongozi kwa nini asiitaje hiyo kampuni??kama alikuwa hataki kuitaja kampuni kulikuwa na haja ya kuleta uzushi kama huo publick??
 
Inawezekana hawakufikia muafaka kwenye dau ndo maana anabwabwaja ovyo. Kama angekuwa serious angewaripoti TAKUKURU bila kuchelewa ili liwe fundisho kwa kampuni zingine zenye tabia kama hiyo.
 
Angewataja angekuwa ameenda kinyume cha maadili ya Chama na Serikali yetu, maana wangeipa kazi tena serikali kuwashughulikia kitu ambacho ni kigumu sana kwa serikali yetu kutekeleza.
 
Huyu si ndiye yule aliyepewa kichapo na wananchi kule Arumeru mashariki alipokutwa akigawa rushwa kwa wananchi maeneo ya Makiba ili wamchague siyoi!alipatawapi hiyo courage ya kukataa hiyo rushwa wakati yeye mwenye ni mtoaji!Kuna uzi ulishaletwaga hapa JF kuwa Medeye alikuwa anauza Ardhi kwa $50,000 per eka.:A S 39:
 
Wangefikia muafaka wa dau asingesema sasa kwa kuwa hawakukubaliana na alichokuwa anataka ikambidi ajigoshe kuutangazia umma ni walewale.
 
Hofu yangu ni kwamba inawezekana hiyo kampuni ilifanikisha azma yake kupitia mlango mwingine. Hii ni Tz, hakuna kisichowezekana.
 
Nahisi tuna tatizo kubwa sana,kama kiongozi mwandamizi kweli ametoa kauli hii.Nilitegemea kabla ya kusikia kauli hii tungesikia Hosea Dk,ameshapeleka faili kwa Dpp na kesi ishaanza kuunguruma kwani waziri angewasiliana na Takukuru na kumkamata mhusika,lakini kama waziri unapata ujasiri wa kuropoka hadharani kwamba amekataa rushwa lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya mhusika,inawezakana tumekuwa taifa linaloongozwa na "mentally unfit leaders"na hao hao wanasimama majukwaani wanasema rushwa adui wa haki na kutokana kauli kama hizi nadhani rushwa sasa ni sehemu ya posho kama zilivyo posho ndiyo maana hata wale vijana waliotapeliwa rushwa zao pamoja na mke wa changoja takukuru hawajaona kama wanakosa la kujibu kwa sababu ya kutoa rushwa kisha kutapeliwa.
 
Mi nasema kwa hapa ccm ilpofika ni wazi wana laana. Inapofika kiongozi anatapika uharo kama huu hadharani inaonyesha kabisa hawa jamaa walivyo wachafu na wananuka.

Watanzania tuwaondoeni madarakani hawa watu wapate na muda wa kufanya toba pengine watakufa wakiwa japo wamepunguza dhambi zao.

Hili genge la ccm majambazi halitaiacha salama hii nchi. Na wanayo mengi mno wameyaficha, siku tukiwaweka pembeni ndo wataanza kutajana mmoja baada ya mwingine na namna walivyoiibia hii nchi.
 
Ndugu mtoa mada haina haja ya kuwa na imani na Ole Medeye,kwani anawatesa sana watu anaowawakilisha bungeni,
Tangia awe mbunge hajawahi kutembelea kisongo/Ngorbob ambacho inazaniwa kuwa ni sehemu/kijiji/kata yenye utajiri zaid hasa wa ardhi,na rasilimali nyingi sana mfano:
Kisongo kina kiwanda A to Z na kimeajiri watu 10,000 = lakini hakuna maji kwa wakazi = Ole medeye 0%
Kisongo kina viwanda vingi vya wachina na wazawa =hakuna polisi = Ole medeye 0%
Kisongo kuna soko la mnada ambalo ni kubwa kwa ar = sokoni hakuna choo = Ole medeye 0%
Kisongo kuna wakazi wengi sana wenyeji na wakuja = hakuna saccos =Ole medeye 0%
Kisongo wakati wa mvua hakupitiki na = hakuna makalavati/daraja =Ole medeye 0%
Kiwanda cha A to Z Kimehamishiwa manispaa = mateves/kisongo hakuna walichopata =Ole medeye 0%
Kuna international school kwa mfano breaburn = waajiriwa wengi wa nje ispokuwa ulinzi = ole medeye 0%
Serikari imeshindwa jenga/kurepea bara bara kisongo = Anayejenga ni nabii Geo Davis =ole medeye 0%
Huyu jamaa ana msaada kabisa just imagine hii ni mifano michache ambayo ameshindwa hata kutengeneza barabara hata futi moja kwa wananchi wa kisongo ambao kila muekezaji anataka kuhamia huku na kama uliwahi sikia kuhusu satelite city ya Kigamboni ingine itakuja jengwa kisongo na nafikiri ndo maana hawa jamaa wakataka mpa rushwa

Sasa hii ni report kidogo tu ya kisongo sasa kama nikiandika maeneo mengine si hata hii dunia haitatosha kwa utendaji wake,
Mr.Godluck Ole Medeye lazima tukungoe tu,kama uliwekwa na lowassa mbona yeye anafanya maendeleo monduli? kwa nini usimuige!!!!!???? kama waarusha hawawezi kusaidia waarusha wenzao basi acha watawaliwe na wa meru na wachagga
 
Sina Imani na ushirikina lkn huyu baba alinifanya niamini kama ushirikna upo pale alipokuwa anafanya kazi TCRA anagomabania cheo na mwenzake Ole Kambaine analala ofisini bila sababu na anamwaga madawa wazi wazi na mabaya zaidi anajifanya kaokoka. Ni Mnafiki sana huyo mzee. Kweli hatufai kuwa waziri. Nachukia kukaa katika nchi ambayo waziri mmojawapo ni Medeye...
 
Katibu huyu amekuwa akijiingiza katika malumbano na baadhi ya watu Mkoani Arusha msimamo wake ukiwa kuna ubaya gani kama Naibu Waziri akikataa kutaja aliyetaka kumpa mlungula huo. Kauli hii imeshabihiana na ya Boss wake ila vile vile yaweza kuwa hapo ndipo mwisho wa mawazo yake. Pamoja na kauli yake hii mimi labda nianze hivi;

Mara nyingi Viongozi hupimwa kwa matamko yao na namna ambavyo wanaweza kutumia ndimi zao. Mhe Kikwete hivi majuzi alisema watu wenye ndimi mbili hawafai kuwa ndani ya Ccm! Na mojawapo wa watu wa namna hiyo ni huyu Naibu Waziri.

Naibu Waziri ni mmoja kazi ya viongozi waandamizi serikalini na ni wenye jukumu la kulinda, kutetea na kuheshima Katiba pamoja na Sheria nyinginezo za Nchi kama ambavyo wameapa. Sasa moja ya Sheria tulizo nazo Nchini ni ile ya PCCB ni sheria halali iliyotungwa na Bunge letu na moja kati ya Sheria ambazo Mhe. Raisi amekuwa akitamani isimamiwe ipasavyo.

Lakini mimi na watanzania wenzangu tumestaajabu pale Naibu Waziri anapotoa kauli na matamshi ya hovyo akidhani ni kinga ama sifa kwake kumbe ni kujidhalilisha yeye mwenyewe, Serikali yake, Chama chake, Boss wake na Watanzania kwa ujumla wake.

Naibu Waziri huwezi kupewa hongo/rushwa halafu eti ukatae na kama haitoshi huyo aliyekupa uache kumchukulia hatua stahiki kwa kufuata sheria, na taratibu za Nchi huo ni uhuni, unafiki na kutokujua mipaka ya kazi na vile vile kutopenda Taifa letu.

Yatosha kusema kuwa

Mosi; Naibu Waziri hana guts hata kidogo za kukataa Mlungula huo na kutokana na kauli za Katibu wake yaelekea kuwa Goodluck si kwamba alikataa bali kiasi alichohitaji hakikufikiwa. Lakini pili huo uadilifu anaodhani kuwa anao hakupaswa atuambie Watanzania ila angetuacha wenyewe tulione hilo.

Ukweli ni kwamba Mhe. Pro. Anna Kajumulo Tibaijuka hana msaidizi na nimjuavyo huyu mama kauli hii itakuwa imemuudhi sana na itaigharimu sana Wizara anayoiongoza. Kama Goodluck anadhani ana uwezo wa kukataa fedha hizo basi aseme hadharani mtu aliyemwonga ama amfikishe kwa Dr. Hosea Edward mara moja.

Akishindwa awe tayari kuwajibishwa ama awajibike.
 
Huu ndo utendaji wa magamba hatakiwi kumtaja mtoa rushwa! Unakumbuka hata Raisi wakati wa fweza ya EPA si aliwaambia wezi warejeshe tu kwa siri atawasamehe. Hivi sisi tutajuaje kama walirejesha hizo pesa kama sio usanii?
 
Ni kweli,kama PCCB wangekuwa wataalamu wa kazi yao wangeaza kumuhoji kwa kina aeleze ilo tukio.
1.Je eneo husika ni wapi?
2.Ni kwanini walitaka kutoa hongo,je ilo eneo ni halali au haramu,lina watu au ni tupu,ni eneo la wazi au la,ni kiwanja cha beach au la ,ni kitalu cha uwindaji au la,ni kitalu cha madini au la?
3.Ni kwanini hao wawekezaji awakutaka kufuata njia za halai kupata eneo ilo?
4.Je baada ya yeye kukataa izo hela walimpelekea nani?na je ilo eneo bado halijachukuliwa?
5.Je hao waliotaka kumpa hongo wanayo maeneo mengine wanayomiliki katika nji hii?
6.Je kama ni mtu mwenye nia nzuri ya kutokomeza rushwa ,ni hatua gani alizochukua baada ya kufuatwa na watu hao?ni kwanini hakutoa taarifa TAKUKURU wakaandaliwa mtego,KWANINI ASUBIRI HADI LEO AANZE KUSIMULIA KAMA STORY
 
Rushwa au hongo kwa watawala wetu wa sasa ni kama kalio na nguo ya ndani. Ni aibu kujitapa ulitaka kupewa rushwa ili utoe upendeleo kutokana na mamlaka yako lakini pia ukashindwa kutumia mamlaka yako kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa watoa rushwa wengine. Ukifanya attempt ya kutoa au kupokea rushwa kuwa siri, unakuwa umejipambanua kidogo sana na yule anayetoa au kupokea rushwa kabisa.
 
Back
Top Bottom