Kauli ya Nassari yampa Nape la kusema

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Nape Nauye leo katika Uhuru FM ametema sumu kali juu ya kauli ya Mh. Nassari juu ya Arumeru kuwa nchi. Ameihusisha jambo hilo na sera ya majimbo inayoinadi CDM.

Amesema CDM sera ya ukanda imeitafuna na mwisho kudhihirika siku ya mkutano wao uliofanyika NMC kuwa wanataka kuitenga Tanzania kwa majimbo hasa Kaskazini!!!!

Amekwenda mbali kwa kumponda Dr. Slaa kuwa ndiye anayependa sana siasa rahisi yaani cheap politics na wamemzoea lakini si Mbowe pale tu aliposema kuna wabunge 70 na mawaziri 7 ambao wapo njiani kuja CDM.

Amesema kuwa angesubiri waje na siyo kukurupuka!!!!!

Mwisho aliitaka CDM kutafuta sera maana inaonekana kufirisika. Akakionya chama cha Demokrasia na Maendeleo kuacha kukihusisha CCM au serikali na katika mauaji yaliyojiri hivi kabibuni katika chaguzi mbali mbali.

Source Uhuru FM.

Mytake:

Kwa sumu aliyotema ile Nape kuna haja ya kumjibu maana kakinukisha sana chama.
 
Mi ni mfuasi wako dogo janja lakn kwa hili kaka umetumia kauli tata sana.ona sasa umewapa la kusema....dah...angalia wakat mwingine bro
 
Nape ndiye cheap mind person,mbona haongei kabla mpaka atembelee wazo la mtu kwa critics zisizo na mashiko?namshauri ajipange sana aache kubwatuka na kutoa povu tu,aje na hoja makini
 
Kwani hakuna nchi ambazo zimewahi kujitenga na maendeleo yakawepo? Hatuwezi kuishi maisha ya kuhofia hata mambo ambayo yanaweza kuwa mema! Nape ni kupe tu hana msaada kwa wanyonge hata
 
Mini nataka kuwaambia hao CCM kama hawawezi kutatatua matatizo ya wananchi, kuendeleza sera za Undugu kama ilivyoonyeshwa kwenye uteuzi wa wakuu wapya wa wilaya...

Ikifika hatua ya wakuu wa wilaya wanatokana na ushauri wa Mtoto wa Rais unategemea nini?
 
Wenye masikio na wasikie,

Wenye macho na waone,

Yaliyo vifuani mwa wanasiasa ni tofauti na wanayoyasema.

Nachukua siasa!
 
Kipimo cha kauli ya Nape tutaona kama wanaCCM wanaovaa Magwanda watakosekana wiki hii. Kama hama hama itaendelea basi tutajua ni mwendelezo tu wa vuvuzela la Nepi. Katibu mwenezi wa chama badala ya kwenda kusaka wanachama wapya na kufungua matawi kama wanavyofanya akina Heche yeye anashawishi maandamano ya vijana wachache wenye njaa. Chama kinawafi()a na JK wako.
 
Mi ni mfuasi wako dogo janja lakn kwa hili kaka umetumia kauli tata sana.ona sasa umewapa la kusema....dah...angalia wakat mwingine bro

Kama ni mfuasi wake acha unafiki. Uropokaji wa CCM kupitia Nepi hakuzuii CDM kufuata sera na agenda zake. Ni katika udandiaji wa CCM uliozoeleka hakuna jipya.
 
Nakuhurumia wewe unayepoteza muda wako adhimu kuisikiliza redio uhuru!
Mimi niliacha kuisikiliza tangu mwaka 2005 na sitegemei kuisikiliza.

Btw, sasahivi Chadema na viongozi wake ndio watengeneza habari nchi hii tangu baada ya uchaguzi mkuu 2010, kwahiyo Nape lazima ajiandae kujibu habari toka Chadema kila siku.
 
Nape, anatia huruma! Hivi 2015 ccm itakapokuwa chama cha upinzani cha tatu kwa ukubwa, atapewa kazi gani na minyama uzembe alonayo sasa hivi? Kijana kavimba hata shati hawezi chomekea, kichwani hakuna kitu kabisa. Vuvuzela mkubwa.
 
Ni siku ya pili sasa Nape anashinda kwenye nyumba za habari kupiga kelele kuhusu kauli ya Nassari. Tafsiri ya haraka ni kuwa CCM hawana la kufanya zaidi ya kusikiliza CHADEMA wanasema nini?!

CCM ndiyo yenye madaraka, ndio wenye serikali, ndio wenye jeshi, ndio wanatakiwa wasimamie matibabu, elimu, usafiri na usalama wa raia pamoja na mali zao. Kwa nini Nape na team yake ya CCM hawataki kusema mipango ya serikali ya CCM kuinua elimu nchini? Nape na CCM wanzake wanajuwa Mtwara wanatumia mkokoteni badala ya ambulance? Kwa nini hatusikii mafanikio ya hii serikali badala yake CCM wana-behave kama chama kisichokuwa na serikali?

Nape anasema nini kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM na ahadi Rais? Issue ya Nassari iko polisi, Nape ni msemaji wa polisi? Kwa mtindo huu kuna fair justice kwa Nassari? Kwanini vyombo vya sheria visiachwe vikafanya kazi kwa uhuru badala ya kuingiliwa na CCM?
 
Najiuliza kwa nini Nape anapenda kuzungumzia kila kitu!
Kazunguka nchi nzima kutangaza kaulimbiu ya kuvua gamba,na hakuna kilichotokea!
Juzi kazungumzia ripoti ya CAG!
Hakuna kitu kinachompita!
Ningependa kufahamu majukumu yake.
Kama anao washauri wamweleze ajifunze pia kukaa kimya.
Vinginevyo,kesho anaweza kuzungumzia uteuzi wa wakuu wa wilaya!
 
Ukitafuta kauli za uchochezi ambazo zimetamkwa na viongozi wa ccm na hakuna mtu/watu waliyo toa matamko kama haya utajuliza mara mbilimbili,eg vyama vya upinzani vita leta vita,kwanini vimesajilia?jk.cdm ni chama cha wachaga.nape.lema asiende arumeru mashariki atauwawa.tendwa.lema ni mwizi magari.zombe ukichanganya ya yule kichaa wa kuzaliwa utaona huyu nape amechanganyikia na sasa hajui mipaka ya chama wala serikali.
 
Nape anaropoka tu,...ndugu nape kauli yako ya wazenji wanaotaka kujitenga ni ipi? Mbona ikulu inaendeshwa na watu wa bagamoyo mf.riz na baba yake kumteua ****** mwenzao Makunga ambaye ni kilaza hujaongea? Chadema itakupa BP mwaka huu.
 
Back
Top Bottom