Kauli ya Nassari yampa Nape la kusema

Nape Nauye leo katika Uhuru FM ametema sumu kali juu ya kauli ya Mh. Nassari juu ya Arumeru kuwa nchi. Ameihusisha jambo hilo na sera ya majimbo inayoinadi CDM.

Amesema CDM sera ya ukanda imeitafuna na mwisho kudhihirika siku ya mkutano wao uliofanyika NMC kuwa wanataka kuitenga Tanzania kwa majimbo hasa Kaskazini!!!!

Amekwenda mbali kwa kumponda Dr. Slaa kuwa ndiye anayependa sana siasa rahisi yaani cheap politics na wamemzoea lakini si Mbowe pale tu aliposema kuna wabunge 70 na mawaziri 7 ambao wapo njiani kuja CDM.

Amesema kuwa angesubiri waje na siyo kukurupuka!!!!!

Mwisho aliitaka CDM kutafuta sera maana inaonekana kufirisika. Akakionya chama cha Demokrasia na Maendeleo kuacha kukihusisha CCM au serikali na katika mauaji yaliyojiri hivi kabibuni katika chaguzi mbali mbali.

Source Uhuru FM.

Mytake:

Kwa sumu aliyotema ile Nape kuna haja ya kumjibu maana kakinukisha sana chama.

Someone is trying to create a mountain out of mole hill, and I wonder why? Yaani a dead issue kama hiyo ya Nassari ndio Nape anafanya kuwa mtaji wa kisissa, kweli wanamagamba waCCM wamekuwa muflisi. Kazi ya CCM kudandiadandia mambo tu.Kila hoja inayotolewa na CDM wao waikimbilia na kufanya yao. Angalia suala la Ufisadi, Katiba,etc. Hey Nape and the clan stop being punk heads and be creative for once!
 
SHUZI LIMEPATA MJAMBAJI. Nepi na magamba wenzake ndo wameshafanya wimbo wa taifa.
 
Huyu ni katibu mwenezi wa chama na serikali na ndo maana hana mipaka ya kazi,mambo ya ikulu anasema yeye,hoja za wabunge yeye,kazi za mkuu yeye,kufukuza mawaziri na mafisadi yeye,bado kupanga safari za rais za duniani,Huyu pia tunaweza kumwita gazeti la serikali lisilo na mhariri,akiamka na kitu kichwani anatema.Katolewa kafara huyo!!!mkuu wake (MKAMA) kakaa kimya.huyoooooooooooooooo!!!!anatwanga maji kwenye kinu kama kumpigia mbuzi jtaa.watanzania wameweka pamba maskioni wamechoka na kauli za wenye ccm-ccj,
 
Back
Top Bottom